Kafulila na Katambi wanawaambia watanzania, mkafie mbali

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,807
1) Wananchi wa Ubungo walivunjiwa Nyumba, ndani zikiwemo sufuria, sahani vyungu, Vitanda, kabati na Nguo za Watoto na hata Mwanasesere zao! Kisa hasa hawakumpa Kura Magufuli. Kwa wananchi hawa Kafulila na Katambi wanawaambia Mkafie Mbali.

2) Tundu Lissu Alipigwa Risasi na Kuitwa Msaliti Kisa alisema Ukweli uliotakiwa kuwekwa siri na serikali inayotaka masifa na kuepuka lawama na Aibu kwa gharama yoyote! Ndege ikiletwa Makamera ya Kufa Mtu! Ikikamatwa kwa deni la Taifa iwekwe siri na Ikijulikana basi inadaiwa ni njama za Lissu, "Msaliti" na sio Deni kweli. Kwa Familia ya Lissu, Wabunge Wenzake na Wananchi walioumizwa na hili, Kafulila na Katambi Wanaambia Mkafie Mbali

3) Arusha Mnyeti alionekana Wazi akiwahonga na kuwaahidi Rushwa Madiwani waliojifanya kurudi CCM na Kupokelewa na Magufuli! Siku chache Baadaye Mla Rushwa huyu anapewa Ukuu wa Mkoa, ati huko ndiko kupambana na Ufisadi wanakoenda hawa! Kwa wanaoona ile ilikiwa ni Tushwa ya Kiwango cha juu na miscourage ya justice, Kafulila na Katambi wanawaambia Mkafie Mbali.

4) Mdogo wangu Ben Saanane Alipotezwa na Kuangamizwa! Na watu wanaoitwa wasiojulikana, Wazazi, Ndugu na Jamaa Tunalia Watanzania nao kadhalika. Kafulila na Katambi wanatuambia Tukafie Mbali

5) Watu wasio na Vyeti vilivyokamilika au vilivyodhaniwa sio vyao kwa Maelfu walifukuzwa kazi, Wengine wakiwa wamebakisha Muda Mchache kustaafu wakapoteza kila Kitu, Ila Viongozi walitakiwa wawe Mfano wa Uwajibikaji, Magufuli akamwacha Daudi Bashite kwa Jina la Kugushi Makonda yeye asiguswe! Watanzania walioona huu ni uonevu na Double standard. Kafulila na Katambi wanawaambia Mkafie Mbali.

6) Magufuli anamtumia Lipumba kihuni na Kihalifu kuvuruga CUF, Wanaoshangaa kioja hiki. Ha Lawlessness, Kafulila na Katambi wanawaambia Mkafie Mbali

7) Serikali ya Magufuli ilichukua Fedha za Wahanga Bukoba ikazitumia kwa Budgeti ya Serikali, Ikawapa Majani ya chai na Biskuti, walioshangaa Kiroja Kile Kafulila na Katambi wanawaambia Mkafie Mbali.

8) Kumekuwepo Kukamatwa kwa wapizani, Kupigwa, Kufungwa bila Kesi kuzuiwa kufanya Mikutano, Wanaoona huu ni Uvunjifu wa Katiba na Haki za Kiraia, Kafulila na Katambi wanawaambia Mkafie Mbali.

9) Nape aliyechunguza Uhuni wa Makonda wa kuvamia clouds kwa SMG au AK47 akiwa na dhamana kama waziri wa habari, Yeye akafukuzaa kama Mbwa ila Jambazi akaambiwa Piga Kazi, Nyie hayo ndio mnayofuata na Walioshangaa Kioja kile Mnawaambia wakafie mbali

10) Mnaohoji Matumizi Makubwa ya Mabilioni bila hata Budget wala Zabuni, Uwanja wa Ndege Nkandla au Gbadolite ya Magufuli kule Chato, Uwanja wa Ndege ambao labda ni kunguru watakuwa wanatua na Taa za Barabarani za Kuongozea Punda! Kafulila na Katambi wanawaambia Mkafie Mbali.

11) Walioshangaa Magufuli kukwapua Bil 2.7 Hazina na Kuzitumia Kuhonga wabunge wa CCM mil 10@ ili waipitishe sheria ya kikoloni ya habari! Ati Kafulila na Katambi wanawaambia Mkafie Mbali.

12) Wanaoshangaa Uhuru wa Bunge Kuingiliwa, Majengo ya Mawakili Kupigwa Mabomu, Wanao omboleza Miili inayoopolewa fukweni mwa bahari imefungwa viroba, kazi ya wasiojulikana! Kafulila na Katambi wanawaambia Mkafie Mbali!

Ati Kuyafuata haya na mengine mengi niliyoyasema huko CCM ya Magufuli, ati Ni kwenda Kupinga Ufisadi! The hell let these Scavengers give me a break!

Mifano ni Mingi. Mimi swali langu ni moja tuu! Chadema hawasimamii serikali, hata kama wameshindwa kuwa Wakali sana kwa Ufisadi, Je Ufisadi ndio Tatizo Pekee linaloihatarisha Tanzania, Vipi Mauaji! Vipi Utekaji Nyara, Vipi utawala wa vitisho na Uonevu? Vipi Matumizi mabaya ya Fedha za Umma nje ya Budget, ie Chato airport na Bombardier, vipi mipango mibovu ya uchumi, Vipi selective application ya sheria kuhujumu haki eg, kufukuza kazi hawa na kumwacha huyu, Kuvunjia nyumba za unaodhani waliokunyima kura na Kuwaacha za unadhani walikupigia kura?

Kafulila na Katambi Ukweli ni Kuwa Mnachotafuta ni Shibe ya Matumbo yenu! Nyie ndio Mkafie Mbali! Am sory to say this!
 
Umeeleza vizuri sana. Yote tisa, lakini kumi - hawa 'wazalendo' wangekuwa na akili timamu, angaa wangefanya sarakasi hizi baada ya Tundu Lissu kuruhusiwa kutoka hospitali akiwa na afya yake!! Ili kuonesha kwamba pamoja na 'kumuunga mkono' mtukufu katika kunyoosha nchi, vitendo vya kuwamiminia Watanzania wenzako risasi kwa sababu tu mna mitazamo tofauti havikubaliki!
 
1) Wananchi wa Ubungo walivunjiwa Nyumba, ndani zikiwemo sufuri, sahani vyungu, Vitanda, sahani na Nguo za Watoto na hata Mwanasesere zao! Kisa hasa hawakumpa Kura Magufuli. Kwa wananchi haya Kafulila na Katambi wanawaambia Mkafie Mbali.

2) Tundu Lissu Alipigwa Risasi na Kuitwa Msaliti Kisa alisema Ukweli uliotakiwa kuwekwa siri na serikali inayotaka masifa na kuepuka lawama na Aibu kwa gharama yoyote! Ndege ikiletwa Makamera ha Kufa Mtu! Ikikamatwa kwa deni la Taifa iwekwe siri na Ikijulikana basi inadaiwa ni njama za Lissu, "Msaliti" na sio Deni kweli Kwa Familia ya Lissu, Wabunge Wenzake na Wananchi walioumizwa na hili, Katulila na Katambi Wanaambia Mkafie Mbali

3) Arusha Mnyeti alionekana Wazi akiwahonga na kuwaahidi Rushwa Madiwani waliojifanya kurudi CCM na Kupokelewa na Magufuli! Siku chache Baadaye Mla Rushwa huyu anapewa Ukuu wa Mkoa, ati huko ndiko kupambana na Ufisadi wanakoenda hawa! Kwa wanaoona ile ilikiwa ni Tushwa ya Kiwango cha juu na miscourage ya justice, Kafulila na Katambi wanawaambia Mkafie Mbali.

4) Mdogo wangu Ben Saanane Alipotezwa na Kuangamizwa! Na watu wanaoitwa wasiojulikana, Wazazi, Ndugu na Jamaa Tunalia Watanzania nao kadhalika. Kafulila na Katambi wanatuambia Tukafie Mbali

5) Watu wasio na Vyeti vilivyokamilika au vilivyodhaniwa sio vyao kwa Maelfu walivukuzwa kazi, Wengine wakiwa wamebakisha Muda Mchache kustaafu wakapoteza kila Kitu, Ila Viongozi walitakiwa wawe Mfano wa Uwajibikaji, Magufuli akamwacha Daudi Bashite kwa Jina la Kugushi Makonda yeye asiguswe! Watanzania walioona huu ni uonevu na Double standard. Kafulila na Katambi wanawaambia Mkafie Mbali.

6) Magufuli anamtumia Lipumba kihuni na Kihalifu kuvuruga CUF, Wanaoshangaa kioja hiki. Ha Lawlessness, Kafulila na Katambi wanawaambia Mkafie Mbali

7) Serikali ya Magufuli ilichukua Fedha za Wahanga Bukoba ikazitumia kwa Budgeti ya Serikali, Ikawapa Majani ya chai na Biskuti, walioshangaa Kiroja Kile Kafulila na Katambi wanawaambia Mkafie Mbali.

8) Kumekuwepo Kukamatwa kwa Aapizani, Kupigwa, Kufungwa bila Kesi kuzuiwa kufanya Mikutano, Wanaoona huu ni Uvunjifu wa Katiba na Haki za Kiraia, Kafulila na Katambi wanawaambia Mkafie Mbali.

9) Nape aliyechunguza Uhuni wa Makonda wa kuvamia clouds kwa SMG au AK47 akiwa na dhamana kama waziri wa habari, Yeye akafukuzaa kama Mbwa ila Jambazi akaambiwa Piga Kazi, Nyie hayo ndio mnayofuata na Walioshangaa Kioja kile Mnawaambia wakafie mbali

Mifano ni Mingi. Mimi swali langu ni moja tuu! Chadema hawasimamii serikali, hata kama wameshindwa kuwa Wakali sana kwa Ufisadi, Je Ufisadi ndio Tatizo Pekee linaloihatarisha Tanzania, Vipi Mauaji! Vipi Utekaji Nyara, Vipi utawala wa vitisho na Uonevu? Vipi Matumizi mabaya ya Fedha za Umma nje ya Budget, ie Chato airport na Bombardier, vipi mipango mibovu ya uchumi, Vipi selective application ya sheria kuhujumu haki eg, kufukuza kazi hawa na kumwacha huyu, Kuvunjia nyumba za unaodhani waliokunyima kura na Kuwaacha za unadhani walikupigia kura?

Kafulila na Katambi Ukweli ni Kuwa Mnachotafuta ni Shibe ya Matumbo yenu! Nyie ndio Mkafie Mbali! Am sory to say this!

Povuuuu, heri ungepata usingizi tu!!!
 
Umeeleza vizuri sana. Yote tisa, lakini kumi - hawa 'wazalendo' wangekuwa na akili timamu, angaa wangefanya sarakasi hizi baada ya Tundu Lissu kuruhusiwa kutoka hospitali akiwa na afya yake!! Ili kuonesha kwamba pamoja na 'kumuunga mkono' mtukufu katika kunyoosha nchi, vitendo vya kuwamiminia Watanzania wenzako risasi kwa sababu tu mna mitazamo tofauti havikubaliki!
Tofauti za kugombea uenyekiti wa chama??
 
Alipohama Nyalandu, tuliambiwa ni matokeo ya Albadir.Well, naona sasa hivi inafanya reverse reaction.
 
Lini unarudi nchini kufanya unayoona yatapendeza zaidi .. na sio kujidai maneno mengi kwa sababu upo huko?
 
Alipohama Nyalandu, tuliambiwa ni matokeo ya Albadir.Well, naona sasa hivi inafanya reverse reaction.
Nyalandu Kaacha Mshahara na Magari na Mafao, Amehamia kwenye Mateso Kudai Haki, Huwezi Kumlinganisha na Scavengers wanaofuata Mizoga na Maiti zilizokwisha oza na zimejaa harufu ya hila na Kila Uovu. Give me a break!
 
KWELI VITA IMEPAMBA MOTO...... BORA HII VITA INGEKUWA HAO DEFECTORS WANGEKUWA SI WASOMI... WENGI WAO NI DEGREE HOLDERS... SIJUI WALISOMA KITU GANI HUKO WALIPOSOMA
Kuwa na Madigree kunaweza kuwa ni indicator ya Good memory pekee na sio a squat of Wisdom!
 
Back
Top Bottom