Kafulila: IMF wamethibisha bajeti ya 2017/2018 haitekelezeki kama ilivyokuwa ya 2016/2017

IFM ifike wakati katika taarifa zenu za uchumi mchanganye na haya majipu tunayotumbuwa ili kuongeza figures
 
China kuna chama kimoja tu cha siasa Na Hakuna demokrasia lakini huwezi kusikia marekani wala vibaraka wa marekani akina kafulila,tundu lisu na chadema hutasikia wakiongea chochote. Kafulila akiona mzungu kaongea anatamani hadi amwabudu.mzungu Akiongee kafulila Na akina lisu na chadema wao watakenua meno yote huku wakiongea kuwa umesikia mzungu alivyosema?
Cha ajabu mwaka 1961 Tz na China zilikua zinalingana Kimaendeleo lkn leo hii ni mbingu na ardhi sijui ni kwanini.
 
Acha usenge hako kaden kadogo mnoo zikiingia za makenikia tunakalipa na kuwakopasha na wao
 
Kwa nini, au kwa sababu ya siasa za vyama??
Hakuna siasa bali hakuna fedha za kutosha kukamilisha bajeti, nyingi wanategemea mikopo na msaada, vikikosekana ndio basi, mwaka ukiisha wanakuja na bajeti mpya na ajabu hakuna anaedai hela za mwaka uliopita wala hawaulizi, ni shughuli ya kupitisha bajeti hewa kila mwaka, upuuzi mtupu.
 
IMF ya Kibondo au Ujiji?
Hivi unadhani nchi hii ikipata matatizo ya uchumi wewe utapona!!!

Kwa nini usilete hoja zako makini , dhidi ya hoja za Kafulila.

Watu waliposema kuwa madini yetu yanaibiwa na wazungu ,mkaanza kejeli kama unavyofanya sasa hivi, mkawabeza wote walioikosoa serikali juu ya usimamizi mbovu wa haya madini.

Juzi kiongozi fulani amekuja kuthibitisha kuwa ni kweli madini yetu yalikuwa yakiibiwa , ni nyinyi tena mmegeuka kuwa washangiliaji na kumuona huyo kiongozi kama malaika vile.
Je huu ni ushabiki wa kichama peke yake? au pia mnasumbuliwa na kokosa marifa ya msingi?
 
Cha ajabu mwaka 1961 Tz na China zilikua zinalingana Kimaendeleo lkn leo hii ni mbingu na ardhi sijui ni kwanini.
China ipi unayoiongelea? Hii ninayoifahamu ilitujengea reli ya tazara miaka hiyo au?
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Kafulila swala la zenji ni out. Namna unavyofikiri wewe ni tofauti na mawazo yao. Hauoni wanavyplishughulikia kwa njia ya lile lipropumbavu? Hata hivyo mimi ninaipenda sana jinsi wanavyovuana nguo hadharani halafu wanawaambia watu wasiwachungulie waliovuliwa nguo. Zaidi ya hayo hii ni dalili njema kwa sababu waliokuwa hawajui kitu sasa wanaelewa. Mungu ibariki Tanzania
Hakuna siasa bali hakuna fedha za kutosha kukamilisha bajeti, nyingi wanategemea mikopo na msaada, vikikosekana ndio basi, mwaka ukiisha wanakuja na bajeti mpya na ajabu hakuna anaedai hela za mwaka uliopita wala hawaulizi, ni shughuli ya kupitisha bajeti hewa kila mwaka, upuuzi mtupu.

Hahaha. Duu hii ni hatari sana!!
 
Hivi unadhani nchi hii ikipata matatizo ya uchumi wewe utapona!!!

Kwa nini usilete hoja zako makini , dhidi ya hoja za Kafulila.

Watu waliposema kuwa madini yetu yanaibiwa na wazungu ,mkaanza kejeli kama unavyofanya sasa hivi, mkawabeza wote walioikosoa serikali juu ya usimamizi mbovu wa haya madini.

Juzi kiongozi fulani amekuja kuthibitisha kuwa ni kweli madini yetu yalikuwa yakiibiwa , ni nyinyi tena mmegeuka kuwa washangiliaji na kumuona huyo kiongozi kama malaika vile.
Je huu ni ushabiki wa kichama peke yake? au pia mnasumbuliwa na kokosa marifa ya msingi?

Unajua sifa moja kuu ya chama cha mapinduzi ni kuchelewa kuelewa. Sio kwamba hawaelewi la, bali wanachelewa sana kuelewa. Jambo ambalo wengine wanaliona leo wao wataliona na kulikubali baada ya miaka kuanzia kumi hadi ishirini ila hawataki kabisa kuachia nchi. Hawa wanaamini chama chao kimewekwa na Mungu madarakani.
 
Habari mbaya hii kwa MACCM mkubali mkatae ila mwenyekiti wenu nchi imemshinda hii mazuzu ndo wataamini kwamba mwenyekiti wenu anaipeleka TZ kwenye neema ila waapi alishachemka kitambo sasa anaenda kwa mwendo wa matukio
 
Unajua sifa moja kuu ya chama cha mapinduzi ni kuchelewa kuelewa. Sio kwamba hawaelewi la, bali wanachelewa sana kuelewa. Jambo ambalo wengine wanaliona leo wao wataliona na kulikubali baada ya miaka kuanzia kumi hadi ishirini ila hawataki kabisa kuachia nchi. Hawa wanaamini chama chao kimewekwa na Mungu madarakani.
Hawa watu, kama ni ujinga basi umefika kiwango cha juu kabisa, sijui baada ya hapa tutauita nini.

Matatizo ya nchi yetu kwa sasa yako wazi mno, hata watoto wadogo wa darasa la saba wanayaona. halafu anakuja mtu mzima humu kuzungumza mambo ambayo ni aibu sana kwake yeye hata kwa taifa zima.
 
Kafulila anafaa ajue sisi kama tanzania hivi karibuni tu tutapata pesa nyingi tu zaidi ya trilioni 104 Rais ALITUAMBIA ZITATOLEWA na wale jamaa wa makinika,so tutaanza kula asali na maziwa kila siku ya mungu hadi mwisho wa enzi
 
Hawa watu, kama ni ujinga basi umefika kiwango cha juu kabisa, sijui baada ya hapa tutauita nini.

Matatizo ya nchi yetu kwa sasa yako wazi mno, hata watoto wadogo wa darasa la saba wanayaona. halafu anakuja mtu mzima humu kuzungumza mambo ambayo ni aibu sana kwake yeye hata kwa taifa zima.
MKUU USIWAZE Acacia wakitulipa tu zile trilion 104 zetu ,wala hatutalia lia tena
 
Cha ajabu mwaka 1961 Tz na China zilikua zinalingana Kimaendeleo lkn leo hii ni mbingu na ardhi sijui ni kwanini.
Jiulize wewe Kibinafsi mbona hujafikia kiwango cha wachina binafsi una tatizo gani? Upo upo tu
 
Anaandika David Kafulila

REPOTI YA IMF KUHUSU UCHUMI WETU JANA INATHIBITISHA KUWA BAJETI YA 2017/18 HAITEKELEZEKI KAMA ILIVYOKUWA 2016/17

Baada ya kusoma ripoti ya IMF kuhusu mwenendo wa uchumi na Bajeti Tanzania niligundua kitu kimoja muhimu kwamba bajeti ya 2017/18 haitekelezeki kama nchi itaendelea kukosa mikopo nje kutekeleza miradi mikubwa iliyopangwa tangu bajeti ya 2016/17 na sasa 2017/18.

Kwa muda sasa kama nchi imekuwa ngumu kupata mikopo nafuu (concessional loans) kutokana na masharti yake ya demokrasia na utawala bora. Zaidi sasa mikopo ya kibiashara toka nje imebaki kuwa migumu kutokana na taasisi za kimataifa kuanza kuisoma serikali kuwa 'anti business'.na mbaya zaidi hatujafanya credit rating ili kuhakikishia wawekezaji na banks kwa maana ya kupata mikopo kama ilivyokwishafanya Kenya na Rwanda kwa upande wa Africa Mashariki.

Lakini mazingira yalivyo ningumu kupata mkopo kuendesha bajeti. Ndio maana serikali imezidi kukopa ndani na kufanya deni la ndani kwenda juu na kuvunja rekodi tangu awamu ya tatu.Awamu ya tatu iliacha deni la ndani likiwa 1.7trilion, miaka10 ya awamu ya nne deni la ndani lilifikia 7.5trn mwaka 2015, sasa miaka miwili tu, deni limefika zaidi ya 11trilion.sawa na nyongeza ya 3.5trilion kwa miaka2tu.Hii ni hatari sana kwenye nchi ambayo mzunguko wa fedha ndani upo chini mno (tight liquidity ).

Hali ikibaki ilivyo nchi itazidi kuzama kiuchumi kwa kushindwa kugharamia mahitaji ya afya , maji na elimu kwasababu ukiangalia deni lililoiva mwaka jana ilikuwa 8trilion wakati mwaka huu ni 9trilion.sasa wakati deni liloiva mwaka huu ni 9trilion bado mshahara (wagebill) ni 7.6trilion.

Hii maana yake mshahara na deni peke yake ni 16.6trilion. Katika mazingira ya sasa ambayo kodi inayokusanywa kwa mwezi TRA ni wastani wa 1.1-1.2trilion, kwamba sio zaidi ya 14trilion kwa mwaka.

Hii maanake ni kwamba makusanyo yetu ya kodi hayatoshi japo kumudu deni la mshahara.kwamba tunakopa kulipa mshahara.hatujazungumza gharama zingine za kuendesha Serikali achilia mbali miradi ya maendeleo.

Tuna njia mbili za kufanya; 1.Lazma Seriakali ishughulikie mgogoro wa Zanzibar na isitishe ukandamizaji demokrasia ili iendelee kupata mikopo nafuu kwani kwa vigezo vya mikopo nafuu Tanzania inaweza kupata mikopo nafuu (concessional loans) kufikia $2.5bn sawa Tsh6tn.kwa mwaka, hiki nikiasi ambacho kinatosha sana kwa serikali kumudu miradi yake ya kimkakati (flagship projects) kama ujenzi wa reli, umeme, Bandari nk 2.

Lazma Serikali ikae na wafanyabiashara na kuwahakikishia kwamba Tanzania ni sehemu Salama kuwekeza na hivyo waweze kuingiza mtaji zaidi kwani hatuwezi kujenga uchumi wa viwanda kama hatupati mtaji toka nje (FDI ), China tunayoitazama leo kama Taifa la pili kwa ukubwa wa uchumi duniani baada ya USA, pamoja na msimamo wake wa ujamaa imefika hapo kuwa nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi duniani baada ya kuwekeza zaidi kwenye elimu, ufundi na technology lakini zaidi kuvutia mitaji toka nje hususan USA.

Lazma tujenge uchumi wakisasa kwa kuangalia dunia yaleo imefika wapi.tukirekebisha mazingira hayo ya kibiashara kwa kujenga imani kwa uwekezaji na biashara tutapata mitaji zaidi na zaidi mikopo ya kibiashara (commercial loans).

Lazma tufanye hivyo ili tuelekee ndoto ya Dira ya Taifa ya 2025, ambayo Kwa mujibu wa Poverty&Human Development Report 2014 inasema ili tufikie dira hiyo lazma pamoja na mambo mengine tuajiri walimu900,000 sawa na wastani wa walimu 90,000 kila mwaka. Leo ajira za walimu tumeajiri sana mwaka2015 hawakuzidi 30,000.Kilimo kinachoajiri 70% sasa kinakua kwa1.7% , kiasi ambacho nichini kupata kutokea tangu Uhuru.

David KAFULILA
Juni27,2017
Kweli mkuu,hakuna muwekezaji atakayekuja wakati anaona wenzake wanasumbuliwa usiku na mchana,tumeacha kufata sheria kwa kigezo eti tunanyooshana,yaani unawanyoosha waliokuwa hawafati sheria kwa wewe kutofata sheria katika kuwanyoosha

Time will tell,hawa wanaoshangilia sekta binafsi kufutwa Tanzania hawajui kwamba kuna wazee wameilea na kuitunza lakini bado changa kiasi kwamba ni vigumu kufungua tawi la benki kenya au biashara lakini wakenya wana mabenki yao zaidi ya moja Tanzania,hata ka sekta binafsi tulikonako tunataka kukauwa kakiwa bado njiti,
 
Back
Top Bottom