Kafulila: Bunge limeongeza ufanisi wa serikali

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,450
Reaction score
5,279
Kamishna wa Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi, Davidi Kafulila, ametoa tathmini yake ya Bunge la 12 kuwa lenye mafanikio makubwa kwa kuisimamia Serikali ya Awamu ya Sita kuwa na mafanikio kuliko awamu zilizopita.

Kafulila amesema kuwa moja ya mikakati ya kupunguza umasikini nchini ni kupitia sekta ya kilimo, ambapo Serikali ya Awamu ya Sita kupitia Rais Samia Suluhu Hassan imeongeza ukuaji wa sekta ya kilimo kwa muda mfupi.

"Serikali ya Awamu ya Sita, ndani ya miaka minne, imekuta kilimo kinakua kwa asilimia 2.6, kwa sasa kinakua kwa asilimia 4.2. Hii haijafika asilimia kumi lakini ni shift kubwa sana," amesema Kafulila.

Dah! Watu tuko tofauti sana, aisee.
 
Huyu hua anajificha kwenye data zaidi,

Lakini maisha yetu haya akisi hizo data anazosema
 
Bunge au kikao cha fisiem
Kila kitu ndiooooooooooo
KAZI ni kipimo cha utu
 
Haka nako kamezidi sasa ,hata kama ni uchawa huu umevuka kiwango
Jibuni hoja acheni unyumbu wenu hapa. Najua hamna uwezo wa kujibu hoja za Mheshimiwa Kafulila kwa sababu yeye anaongea kwa takwimu na ushahidi wakati Ninyi mnafanya kazi ya uropokaji na upayukaji tu
 
Huyu hua anajificha kwenye data zaidi,

Lakini maisha yetu haya akisi hizo data anazosema
Na wewe mpinge kwa Data. Dunia ya Leo ni Data tu za kiutafiti na kisayansi na siyo kupiga porojo zako hapa. Mheshimiwa Kafulila anaonyesha usomi wake na kuongea kisomi kabisa na kwa lugha nyepesi kabisa ambayo hata asiye na Elimu kama wewe anaweza kumuelewa kabisa
 
Back
Top Bottom