Kafulila awalipua Wabunge wa CCM!

mjunguonline

Member
Mar 10, 2011
73
5
MBUNGE wa Kigoma Kusini (NCCR Mageuzi), David Kafulila jana jioni alichafua hali ya hewa bungeni baada ya kuwataja wabunge wawili wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) kwa kuomba rushwa katika halmashauri ambayo hakuitaja.

Akichangia Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano, Kafulila aliwataja Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi na Mbunge wa Bahi, Omary Badwel wote wa CCM akidai kwamba aliwakamata wakiomba rushwa kwa viongozi wa halmashauri.

Wakati akitaja majina hayo, Kafulila nusra aingie katika mgogoro na Mwenyekiti wa Bunge, George Simbachawene ambaye alikuwa akimwamuru kukaa chini kutokana na muda wake wa kuchangia kumalizika.

Kafulila alikuwa akiendelea kuzungumza bila kujali kengele ya pili iliyopigwa kuashiria kwamba muda wake wa kuzungumza ulikuwa umekwisha.

"Mheshimiwa Mwenyekiti kwa wakati wa sasa ni vigumu kusimamia matumizi kwani mfumo wetu wa uongozi unaruhusu ufisadi, wapo viongozi, mawaziri, wabunge wanaomba rushwa...." alisema Kafulila na kuamsha zogo ambalo liliambatana na sauti zisizo rasmi katika ukumbi wa Bunge zikiuliza ".....wapo humu humu?" Kafulila alijibu "Ndiyo..." Sauti moja ilisema wataje, hapo ndipo aliposema ".... Wapo kina Zambi, Badwel,Â* nimewakamata na nimechukua hatua, hatuwezi kuendelea namna hii," kisha akaketi.
 
Katika mjadala wa kuchnngia mpango mkakati wa maendeleo ya taifa,mh.kafulila aliwataja live bila kumung'unya maneno kuwa aliwakamata mh. G.zambi mbunge wa ccm mbozi na bedwell mbunge wa ccm bahi wakiomba rushwa mkoani tanga,mweshimiwa zambi aliposimama alimtaka mh.kafulila athibitishe kauli yake kupitia spika na akasema hili ndio tatizo la kujiiita wabunge vijana na kutafuta umaarufu wa kulipuka,akaendelea kusema mh.kafulila ndio maana hata chadema walimfukuza kutokana na tabia yake ya kusema vibaya wenzie ndani ya chama,sasa mh.kafulila mwaga data juu ya ukweli wa shutuma hizi,mrema m/kiti wa kamati kamati yako inapambana na rushwa au inaboresha rushwa?maana wote hao wako kwenye kamati yako
 
nampongeza kafulila kwa ujasiri wake wa kuwataja hadharani kina zambi, yeye kaona hilo na kulisema, laiti kama wafanyakazi wa mawizara na halmashauiri wakiiga hili na kuweka waomba rushwa hadharani, itasaidia sana punguza rushwa. wakiongezeka mashujaa kama hawa wataanza jitokeza wapya wa kuwafungulia kesi waomba rushwa. hao wakishindwa kazi wananchi watakuwa na uelewa uliofikiwa na wana wa egypt. ipo siku kitaeleweka tu.....
 


WAKATI tuhuma za rushwa dhidi ya wabunge wawili wa CCM zilizotolewa na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, zikisubiri kutolewa uamuzi na mamlaka husika, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), Dk Edward Hosea, amesema ofisi yake haijapata taarifa hizo.
Tuhuma hizo zilitolewa na Kafulila Dodoma kwenye mkutano wa Bunge unaoendelea, kwa kuwatuhumu Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi na Mbunge wa Bahi, Omary Badwel, wote wa CCM kuwa walikuwa wakiomba rushwa kutoka viongozi wa halmashauri.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Dk Hosea alisema siyo yeye binafsi au ofisi zake zilizopata tuhuma hizo za Kafulila.Hata hivyo, Dk Hoseah alibainisha kuwa inawezekana Kafulila alipeleka ushahidi au malalamiko yake kwenye ofisi za Takukuru jimboni kwake.Kuhusu jitihada na mafanikio ya Takukuru kupambana na rushwa, Dk Hosea alisema taasisi yake imepiga hatua kwenye vita hiyo, ikilinganishwa na awali.
Aaliongeza kuwa Takukuru inapofanya kazi zake, haiogopi wala kupendelea mtu yeyote na kwamba, wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria.Kauli hiyo ya Dk Hosea ilifuatia maoni ya wadau wa kongamano hilo, waliodai kuwa taasisi hiyo imekuwa ikiwafumbia macho watuhumiwa wakubwa wa rushwa na kuishia kushughulikia kesi ndogo za rushwa.
“Hakuna ambaye tunamuonea haya katika hili, nchi hii inaendeshwa kwa utawala wa sheria, kunapotolewa malalamiko yeyote, tunafanya uchunguzi kwanza na kupeleka faili la kesi hiyo kwa DPP (Mkurugenzi wa Mashitaka), yeye akiridhika kuwa kuna kesi, basi atapeleka mahakamani,” alisema Dk Hosea.
Kwa mujibu wa Dk Hosea, watu wamekuwa wakilalamika kuwa kuna watu wanahusika na rushwa bila ushahidi wa wanayozungumza.Kuhusu kesi za kampuni tata ya Kagoda na watuhumiwa wa kesi ya EPA, Dk Hosea alisema; “Hakuna anayeogopa kuchunguza Kagoda, tuleteeni ushahidi na sisi tutachunguza, hakuna aliye juu ya sheria katika nchi hii,”alisema.
Akifungua kongamano hilo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe alisema mapambano dhidi ya rushwa ni ya jamii yote, hivyo ili kushinda inatakiwa kuwa na nguvu ya pamoja.Mwisho

 

wakati tuhuma za rushwa dhidi ya wabunge wawili wa ccm zilizotolewa na mbunge wa kigoma kusini (nccr-mageuzi), david kafulila, zikisubiri kutolewa uamuzi na mamlaka husika, mkurugenzi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (takukuru), dk edward hosea, amesema ofisi yake haijapata taarifa hizo.
Tuhuma hizo zilitolewa na kafulila dodoma kwenye mkutano wa bunge unaoendelea, kwa kuwatuhumu mbunge wa mbozi mashariki, godfrey zambi na mbunge wa bahi, omary badwel, wote wa ccm kuwa walikuwa wakiomba rushwa kutoka viongozi wa halmashauri.
Akizungumza dar es salaam jana, dk hosea alisema siyo yeye binafsi au ofisi zake zilizopata tuhuma hizo za kafulila.hata hivyo, dk hoseah alibainisha kuwa inawezekana kafulila alipeleka ushahidi au malalamiko yake kwenye ofisi za takukuru jimboni kwake.kuhusu jitihada na mafanikio ya takukuru kupambana na rushwa, dk hosea alisema taasisi yake imepiga hatua kwenye vita hiyo, ikilinganishwa na awali.
Aaliongeza kuwa takukuru inapofanya kazi zake, haiogopi wala kupendelea mtu yeyote na kwamba, wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria.kauli hiyo ya dk hosea ilifuatia maoni ya wadau wa kongamano hilo, waliodai kuwa taasisi hiyo imekuwa ikiwafumbia macho watuhumiwa wakubwa wa rushwa na kuishia kushughulikia kesi ndogo za rushwa.
"hakuna ambaye tunamuonea haya katika hili, nchi hii inaendeshwa kwa utawala wa sheria, kunapotolewa malalamiko yeyote, tunafanya uchunguzi kwanza na kupeleka faili la kesi hiyo kwa dpp (mkurugenzi wa mashitaka), yeye akiridhika kuwa kuna kesi, basi atapeleka mahakamani," alisema dk hosea.
Kwa mujibu wa dk hosea, watu wamekuwa wakilalamika kuwa kuna watu wanahusika na rushwa bila ushahidi wa wanayozungumza.kuhusu kesi za kampuni tata ya kagoda na watuhumiwa wa kesi ya epa, dk hosea alisema; "hakuna anayeogopa kuchunguza kagoda, tuleteeni ushahidi na sisi tutachunguza, hakuna aliye juu ya sheria katika nchi hii,"alisema.
Akifungua kongamano hilo, waziri wa nchi, ofisi ya rais (utawala bora), mathias chikawe alisema mapambano dhidi ya rushwa ni ya jamii yote, hivyo ili kushinda inatakiwa kuwa na nguvu ya pamoja.mwisho


ccm ni janga la kitaifa
 
Back
Top Bottom