maringeni
JF-Expert Member
- Oct 8, 2013
- 3,198
- 3,894
Wanajamvi,
Yupo dogo ananisumbua kwa kutaka ushauri nami nimeona nimlete huku tumshauri kwa pamoja. Ni habari ya kweli.
Jamaa kaoa japo hajamaliza taratibu za mahari nk. Keshapata watoto kadhaa ndani ya ndoa yake. Alikuwa anaishi mitaa ya wazazi wake akijishuhulisha na kazi zake na za familia upande wa babake.
Kulitokea kutoelewana na babake japo hajataka kuwa wazi haswa shida ilikuwa nini. Alilazimika kuishi mbali na eneo na shuhuli za wazazi.
Mambo yalipokuwa magumu akaondoka kwenda kwa wakwe na familia yake akajisalimisha kwa mamamkwe maana babamkwe alitimka kamwachia mji mamamkwe.Nilikuja kugundua kuwa muda wote alikuwa akitoa sapoti kubwa kwa mama mkwe.
Sasa mapenzi yamepungua manamkwe kawa mbogo anamwambia aondoke akatafute mkwanja.Jamaa analalamika na anataka ushauri afanyeje.
Hebu tumshauri.