TUKUTUKU
JF-Expert Member
- Sep 14, 2010
- 11,763
- 4,039
Suala la kuanzisha Mahakama ya kadhi limekuwa gumzo kubwa nchini kwetu katika miaka ya hivi karibu.Waislamu wanataka chombo hichi kitambuliwe na serikali. Vilevile, gharama za uendeshaji wake zibebwe na serikali.Kuhusu suala la gharama la uendeshaji wa chombo hichi kugharamiwa na serikali. mimi linanishangaza sana,kwa sababu hili haliendani na misingi ya dini ya kiislamu.Fedha za serikali zinapatikana kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato,ambavyo kimsingi haviendani na imani ya dini ya kiislamu.Kwa mfano dini ya kiislamu hairuhusu hutozaji wa riba,na pato lolote linalotokana na riba ni haramu.Hapa ukichunguza kwa makini utagundua mojawapo ya chanzo cha mapato ya serikali ni utozaji wa riba,je hili linarususiwa na imani ya dini ya kiislamu?Mfano mwingine ni kuhusu suala la pombe.Misingi ya dini ya kiislamu inakataza unywaji na utengenezaji wa pombe kama njia ya kujipatia fedha.Pombe katika nchi yetu ni mojawapo ya chanzo cha mapato ambayo huingizwa kwenye mfuko mkuu wa serikali, ili kuendesha shughuli za serikali.Je waislamu hawaoni kugharamia shughuli za mahakama ya kadhi kwa kutumia fedha hizi ni harama?Mfano mwingine ni suala la hulaji na ufugaji wa nguruwe,hii ni haramu kwa uislamu,lakini hukichunguza kwa makini hutagundua mojawapo ya chanzo cha mapato ya serikali ni ushuru unaotozwa kutokana na ufugaji na huuzaji wa nyama ya nguruwe,mapato haya yote hupelekwa kwenye mfuko wa serikali ili kugharamia shughuli mbalimbali za serikali.Je waislamu hawaoni fedha hizi kugharamia shughuli za mahakaha ya kadhi ni haramu?Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na jitihada mbalimbali za uanzaishwaji wa Islamic banking wing katika benki za biashara mbalimbali hapa nchini kwa mfano banki ya biashara ya taifa(NBC) na Benki ya biashara ya Kenya(KBC),yote haya yamefanyika ili kuwawezesha waislamu kuepukana na mfumo wa kawaida wa kibenki(conventional banking system) ambayo ni dhambi kuutumia kwa kuwa utatoza na kutoa riba.
Fedha chafu kama hizi kwa nini zitumike kuendesha shughuli halali za mahakama ya kadhi, ambayo itakuwa inaheshimika kidini?Naomba waislamu wafanya uchunguzi wa kina kabla ya kukubali kutumia fedha chafu kiasi hiki na hasa zile zinazotoka kwa makafiri,ili kuiwezesha mahakama yao kuwa takatifu.
Nawasilisha!
Fedha chafu kama hizi kwa nini zitumike kuendesha shughuli halali za mahakama ya kadhi, ambayo itakuwa inaheshimika kidini?Naomba waislamu wafanya uchunguzi wa kina kabla ya kukubali kutumia fedha chafu kiasi hiki na hasa zile zinazotoka kwa makafiri,ili kuiwezesha mahakama yao kuwa takatifu.
Nawasilisha!