Kadiri Lowassa anavyojiimarisha CHADEMA, ndivyo chama kinavyofifia na kupotea

Chadema inakufa kifo cha mende kabisa ... tamaa ndio zinaponza chama hicho
 
Ulaya unaifananisha na hii bahari ya laana na upumbavu? Ulaya kuna fair ground ya politics sio hizi za dola kulinda wahuni kama akina Lipumba na kuiba kura!!!

Usiifananishe ulaya na wajalaana wenu!!
 
Lowasa yeye hana muda na chama yeye anatafuta mashabiki, yaani uchaguzi utajapofika atakuwa kama mgombea binafsi ndani ya chama
 

Hapo ndipo shida ilipo kwa tulioangukia kwenye "Great Dissapointment"
Wale tuliojua tunaitafuta Tanzania mpya yenye mtazamo mpya na attitude mpya, hatukujua kuwa lengo ni kupata tu kura na kushika madaraka. Hiyo ni sawa tu na zama za Afrika kudai uhuru kutoka kwa mkoloni ni kisha uongozi mpya wa kiafrika ukagawana keki ya Taifa kwa itikadi ya "Wakati wetu kula".

Wale tulioamua kukaa pembeni kwa sasa (Tuko wengi sana, hata huko juu kwenye uongozi wa Chadema tupo) hatukuwahi kutarajia Chadema ingekuwa ya kutaka madaraka tu na sio kuibadili Tanzania.
 
ngoja waje akina mwahabari huru,nibozali,erythrocity,kisu cha ngariba na vijana wengine toka ufipa wamwage povu .
 
Mimi ningeku
Mimi ningekukubalia kama fursa zote zingetolewa sawa kwa vyama vya siasa halafu ndio tuone huo ufhaifu.
Lkn huwezi kumjaji mwenzako wakati wewe anatumia jeshi, polisi, viongozi wa serikali ktk kuidhibiti chadema halafu utakuja hapa unasema inafifia.
Ni haina ya mawazo ya MTU muoga, asiependa ushindani, asijiamini na mwenyekupenda kupendelewa.
Ni sawa na bondia atakaejisifu kushinda pambano wakati upinzani wake wamefungwa MIKONO.
 
Mkuu naona umeamua kujiunga Mtaa ule kiFIKA....ili chama...kisike ..lazima kifanye Siasa jiulize Baada ya Uchaguzi uliisiikia Chadema.kwenye Jukwaa..gani ingekuwa hivyo unavyoamini mtukufu angeshatengeu...kauli yake
 
Tatizo linavyovikabili vyama vya Upinzani Tanzania kwa sasa(CHADEMA kikiwemo), ni kunyimwa fursa ya kufanya shughuli zao za kisiasa.

Sio Lowassa wala Sumaye.

Tusitafutane Uchawi.

Umenena kweli, bunduki na mabomu yanapotumika kufinya demokrasia ndiyo tatizo
 
Natamani mbowe angesoma ulichokiandika hapa
Safi sana muraaaaaa
 
Chama kikiimarika,kura huongezeka tu Mkuu. Punguza lugha kali tujadiliane kwa kujenga
Siku hizi mnajitoa akili sanaa,unafikir watu dizain ya kina lipumba wameishaaa.Mpo wengi sana,mmeanza kujilipua taratibu kwa kujidai kuipenda CDM hata kina Machali wamejitoa ufahamu kidogo.Inshort wamekosa dira,kwa sasa hakuna kelele yoyote itayoturudisha nyuma zaid ya 2020 kumuondoa mtu madarakani
 
Hilo lipo dhahiri.

Watu wa Lowassa hawataki kukubali ukweli
Mbowe anaogopa kugeuka jiwe.

CDM mpya lazima iwatose Lowassa na Mbowe. Je inawezekana?
 
Tatizo linavyovikabili vyama vya Upinzani Tanzania kwa sasa(CHADEMA kikiwemo), ni kunyimwa fursa ya kufanya shughuli zao za kisiasa.

Sio Lowassa wala Sumaye.

Tusitafutane Uchawi.
Chama ni vikao,wapi mmenyimwa ruhusa ya kufanya vikao?
 
Umenena vyema, lengo si tu kubadili jina la chama tawala na sura za wanaotawala, tunahitaji mabadiliko ya kweli yanayolenga kumkomboa mtanzania
 
kwa uongozi wa jpm hata dr slaa angekuwepo angeishia kisongo.kwa sasa nchi yetu inaongozwa kwa mkono wa chuma...siasa mpaka 2020.
 
Hivi Tanzania bado shughuli za kisiasa zinaruhusiwa? Au mimi nipo nchi nyingine? Maana nijuavyo kwa sasa shughuli za kisiasa Tanzania zimesimamishwa na zinaelekea kuuawa. Na mimi napendekeza wapinzani wanyamaze tu wala wasihangaike na siasa maana kila wakati wakitaka kufanya siasa wanaumizwa tu na vyombo vya dola wakati akina Mselewa wakidunda ofisini. Huwa nawashangaa sana watanzania wanapoona kama vile uwepo wa wapinzani ni faida ya wapinzani wenyewe badala ya kujua kuwa ni faida kwa Taifa na serikali iliyopo madarakani. Hivi kweli unafikiri bila upinzani kuna kila cha maendeleo kitafanyika? Kwa kawaida mwanasiasa na serikali huwajibika kwa kuogopa kunyimwa kura tu na si vinginevyo. Sasa kama mwanasiasa aliyepo madarakani hana mpinzani ataogopa nini? Utamnyima kura halafu umpe nani? Watanzania hata 'waliosoma' ni shida tu. Hivi ni kwa nini? Natamani zije zile zama za kupigia kura mtu na kivuli ili wanasiasa watuadabishe watanzania labda akili zitakuja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…