Kadiri Lowassa anavyojiimarisha CHADEMA, ndivyo chama kinavyofifia na kupotea

Alipigiwa kura na watu wanaoviunga mkono vyama vyote vilivyounda UKAWA. Dr Slaa alikuwa akipigiwa kura na watu wenye kuinga mkono CHADEMA pekee. Kwenye suala la substance kichwani mzee wa karatu yupo juu sana kumlinganisha na mzee wa mvua ya Thailand.
Lakini slaa aliondoka na wapiga kura wake(wafata mtu na sio itikadi za chama),so mamvi alipigiwa kura na wapya
 
Tatizo linavyovikabili vyama vya Upinzani Tanzania kwa sasa(CHADEMA kikiwemo), ni kunyimwa fursa ya kufanya shughuli zao za kisiasa.

Sio Lowassa wala Sumaye.

Tusitafutane Uchawi.
Vinanyimwa fursa na nani? endapo vyama vya upinzani nchini vinategemea fursa hizo kwa kupewa iwe kikatiba au vyovyote vile basi iko shida na hasa ukizingatia mazingira yanayotawala siasa za nchi za kiafrika, vyama vyote pinzani vilivyofanikisha malengo yake (Afrika) ni vile vilivyolazimisha watawala kuachia fursa ya wao(wapinzani) kufanya shughuli za siasa kwa mujibu wa hiyo katiba.
 
Hivi Tanzania bado shughuli za kisiasa zinaruhusiwa? Au mimi nipo nchi nyingine? Maana nijuavyo kwa sasa shughuli za kisiasa Tanzania zimesimamishwa na zinaelekea kuuawa. Na mimi napendekeza wapinzani wanyamaze tu wala wasihangaike na siasa maana kila wakati wakitaka kufanya siasa wanaumizwa tu na vyombo vya dola wakati akina Mselewa wakidunda ofisini. Huwa nawashangaa sana watanzania wanapoona kama vile uwepo wa wapinzani ni faida ya wapinzani wenyewe badala ya kujua kuwa ni faida kwa Taifa na serikali iliyopo madarakani. Hivi kweli unafikiri bila upinzani kuna kila cha maendeleo kitafanyika? Kwa kawaida mwanasiasa na serikali huwajibika kwa kuogopa kunyimwa kura tu na si vinginevyo. Sasa kama mwanasiasa aliyepo madarakani hana mpinzani ataogopa nini? Utamnyima kura halafu umpe nani? Watanzania hata 'waliosoma' ni shida tu. Hivi ni kwa nini? Natamani zije zile zama za kupigia kura mtu na kivuli ili wanasiasa watuadabishe watanzania labda akili zitakuja.
Kwani China kuna upinzani gani kule. Mbona wapo vizuri kuliko ugiriki kwenye huo upinzani?
 
Mbowe ni tatizo jumlisha na lowassa unakuwa mzigo mkubwa wenye ufundo wa kutosha.
Ni muda wa kufanya mabadiliko ndani ya CHADEMA , vijana makini wako ndani ya Chama lakini awatumiwi.
[HASHTAG]#malisa[/HASHTAG]
[HASHTAG]#yericko[/HASHTAG]
Na hata Ben asiye julikana aliko sasa, hawa wamekuwa wapiga debe tu mtandaoni lakini ndani ya Chama nafasi yao ni finyu sana.

#Mabadiliko_yaanzie_ndani_ya_chama_kwanza.

#Mbowe_ni_tatizo_ndani_ya_chama.
Unajua tusiongopeane hapa, kwani lazima wote wawe viongozi au? Huko keingine nitajie vijana waliopewa uongozi zaidi ya CDM tuache kulete mada zisizo na mashiko.
 
Siasa za boys to men zimepita. Jk na lowasa wastaafu siasa. Jk kastaafu, kafanya makubwa ndani ya serikali na chama chake. Lowasa naye kafanya makubwa ndani serikali na Ccm na pia kaisaidia chadema kupata wabunge wengi. Lowasa staafu siasa baba yetu. Tunaitaka chadema ya awali. Tunamtaka Mnyika yule..tunamtaka mnyika yule.. Yule mnyika. Siyo huyu. Siwezi kumlaumu mbowe, mbowe hajawahi kuwa mwanasiasa mzuri but ni kiongozi / management mzuri but not charismatic leader.
Unamuongelea Mbowe, basi basi hujui kariba za viongozi wewe. Bila uthubutu wa FM, kungekuwa hakuna upinzani TZ, kwa taarifa yako Mbowe ndio upinzani.
 
Vyama vya upinzani vyote vimefifia si kwa sababu ya lowassa ni kwa sababu ya hali ya kisiasa ilivyo CHADEMA wasitetereke na maneno ya ngedere juu ya Lowasa coz Lowasa bado ni powerful and popular too ndo maana akidondoka popote hata saizi lazima watu fulani wajambe jambe kwa sababu anasepa na kijiji.
 
Kuluka luka kwa maharage ndio kulainika na kulegea kwake sisiem inalainika na kulegea kila Siku mwisho itabaki mchuzi tuu.
 
Mwambieni Pombe aruhusu mikutano kama ya enzi ya JK kisha mrudi kujadili kuimarika na kutoimarika kwa siasa za upinzani... Katikati ya msoto huu wa demokrasia mnaleta habari za kijinga namna hii tena mnaojiita wasomi? Hiki ni kinyaa!!
Mikutano pekee ndio siasa? Acheni visingizio mkuu...enzi za JK mikutano iliruhusiwa? au ilifika mahali Chadema walikuwa wanalazimisha kwa nguvu ya umma ....umesahau Arusha watu kufa kwa mabomu ....akina Dr Slaa kupigwa virungu .....umesahau Mwangosi nini kilitokea kwake wakati wanachadema wanasambaratishwa? Acheni kumsingizia JPM ....hiyo mikwara ipo awamu zote ila kubalini sasa hivi hamna tena ushawishi ....mbaya zaidi hata Arusha watu wanawapotezea .....alafu mkuu najua ulikuja na mafuriko ya kuzungurusha mikono ....hujui harakati za upinzani .....ulizoea good times huko chama tawala ....sasa pambana mzee ...
 
Miongoni mwa watu jinsi waheshimu sana humu kwa hoja na jina lako pia lipo, sina hakika kama utafiti wako hu uliangalia au kulinganisha siasa za JK na za Magi, JK aliruhusu mikutano ya kisiasa wakati Magu hataki so inakua ngumu kusema kupotea kwa Chadema kunatokana na ujio Wa Lowassa au kupigwa marufuku kwa mikutano ya kisiasa na hata kuto onekana kwa binge then wnanchi nao hawajui wawakilishi wao wameongea nini? Jaribu kuziangalia haki hizo kwanza then ndio hoja yake inaweza jengeka vizuri.
 
Kumpokea mamvi ilikuwa bonge la kamari.....ku refresh chama mbowe akae pembeni na mamvi astaafu kwa heshima.
 
CHADEMA naitafsiri kama taasisi ya wathubutu,wakosoaji kwa kutumia hoja mujarabu na wapambanaji dhidi ya ufisadi na wizi wa mali za umma. Ni taasisi iliyojengwa na kuheshimika,kwa kuzoa maelfu ya wanachama kwa namna hiyo

CHADEMA ilipendwa na vijana makini na wasomi kwakuwa waliiona Tanzania waitakayo kupitia chama hicho kikuu cha upinzani nchini. CHADEMA ilikuwa taasisi ya kuwasemea wanyonge;kuwaumbua mafisadi;kuwakemea viongozi na kuandaa viongozi wajao. Ilikuwa CHADEMA ya kupigiwa mfano na kuaminika.

CHADEMA imebadilika baada ya kuhamia humo kwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu,Edward Ngoyai Lowassa. Sasa,imeanza kupoteza-tena kwa kasi sifa na vivutio nilivyovieleza hapo mwanzo. Lowassa alihamia CHADEMA na watu wake. Kwa maneno mengine,alihamia na 'chama chake'. Tayari yeye na watu wake wameshachomoza na kushika nafasi mbalimbali ndani ya CHADEMA.

Kadiri Lowassa anavyojikita na kujiimarisha,ndivyo 'ile CHADEMA' inavyopotea. Kilele cha kupotea kwa CHADEMA ile kitakuwa wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani ya CHADEMA. Hapo patakuwa ni kati ya chama cha Lowassa na chama cha CHADEMA!

Kwaheri 2016,karibu 2017!
Umesema vyema kabisa
 
Watu wanaotetea nafasi ya Lowassa ndani ya Chadema wanashindwa kuelewa kwamba tatizo siyo Lowassa kutokuwa na hatia kisheria kwa makosa ya kimaadili aliyoyafanya wakati akiwa Waziri Mkuu ambayo yalipelekea kujiuzulu. Tatizo la Lowassa ni hadhi yake chafu mbele ya jamii, ambayo inamtambua kama fisadi. Hiyo tu inatosha kukiua chama ambacho kilijinadi kama chama kinachotetea wanyonge dhidi ya "mafisadi CCM".
 
CHADEMA naitafsiri kama taasisi ya wathubutu,wakosoaji kwa kutumia hoja mujarabu na wapambanaji dhidi ya ufisadi na wizi wa mali za umma. Ni taasisi iliyojengwa na kuheshimika,kwa kuzoa maelfu ya wanachama kwa namna hiyo

CHADEMA ilipendwa na vijana makini na wasomi kwakuwa waliiona Tanzania waitakayo kupitia chama hicho kikuu cha upinzani nchini. CHADEMA ilikuwa taasisi ya kuwasemea wanyonge;kuwaumbua mafisadi;kuwakemea viongozi na kuandaa viongozi wajao. Ilikuwa CHADEMA ya kupigiwa mfano na kuaminika.

CHADEMA imebadilika baada ya kuhamia humo kwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu,Edward Ngoyai Lowassa. Sasa,imeanza kupoteza-tena kwa kasi sifa na vivutio nilivyovieleza hapo mwanzo. Lowassa alihamia CHADEMA na watu wake. Kwa maneno mengine,alihamia na 'chama chake'. Tayari yeye na watu wake wameshachomoza na kushika nafasi mbalimbali ndani ya CHADEMA.

Kadiri Lowassa anavyojikita na kujiimarisha,ndivyo 'ile CHADEMA' inavyopotea. Kilele cha kupotea kwa CHADEMA ile kitakuwa wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani ya CHADEMA. Hapo patakuwa ni kati ya chama cha Lowassa na chama cha CHADEMA!

Kwaheri 2016,karibu 2017!
Mkuu asante kwa tafakari mulua,
Lakini je ni nani aliyejiunga kwa mwenzake!
Lowasa alijiunga chadema?
Au chadema ilijiunga kwa Lowasa?
Je Lowasa anafuata masharti ya chadema?
Au chadema inafuata masharti ya Lowasa?
Tukipata majibu ya hayo maswali ndo tutajua kama chadema imeuzwa au LA!
Nawatakia heri 2017
 
CHADEMA naitafsiri kama taasisi ya wathubutu,wakosoaji kwa kutumia hoja mujarabu na wapambanaji dhidi ya ufisadi na wizi wa mali za umma. Ni taasisi iliyojengwa na kuheshimika,kwa kuzoa maelfu ya wanachama kwa namna hiyo

CHADEMA ilipendwa na vijana makini na wasomi kwakuwa waliiona Tanzania waitakayo kupitia chama hicho kikuu cha upinzani nchini. CHADEMA ilikuwa taasisi ya kuwasemea wanyonge;kuwaumbua mafisadi;kuwakemea viongozi na kuandaa viongozi wajao. Ilikuwa CHADEMA ya kupigiwa mfano na kuaminika.

CHADEMA imebadilika baada ya kuhamia humo kwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu,Edward Ngoyai Lowassa. Sasa,imeanza kupoteza-tena kwa kasi sifa na vivutio nilivyovieleza hapo mwanzo. Lowassa alihamia CHADEMA na watu wake. Kwa maneno mengine,alihamia na 'chama chake'. Tayari yeye na watu wake wameshachomoza na kushika nafasi mbalimbali ndani ya CHADEMA.

Kadiri Lowassa anavyojikita na kujiimarisha,ndivyo 'ile CHADEMA' inavyopotea. Kilele cha kupotea kwa CHADEMA ile kitakuwa wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani ya CHADEMA. Hapo patakuwa ni kati ya chama cha Lowassa na chama cha CHADEMA!

Kwaheri 2016,karibu 2017!
Kwa hiyo tatizo ni Lowasa ?? Nafikiri tunahitaji fikra pana zaidi katika hili jambo na tunapozungumzia masuala ya uongozi, na mstakabali wa Nchi yetu tuweke maono sahihi na yenye tija !! Lowasa Ana nafasi yake katika kuijenga Nchi hii kupitia vyama vya siasa, lakini ukumbuke Lowasa amekaa Nje ya uongozi wa awamu ya 4 zaidi ya miaka nane, je una muhukumu kwa Dhambi ipi ?? Tuwe wakweli na tuache kuimba kama kasuku ! Lete hoja za msingi na zaukweli zenye kumuondolea sifa Mh. Lowasa. Acha blaa blaa ... !! Lowasa, Sumae na wengine lazima wawasaidie vijana katika kujenga mageuzi ya kweli katika Nchi hii , Elewa hata Nyerere bila msaada wa wazee wa kipindi kile ingekuwa kazi kubwa kuikomboa Nchi hii , hivyo tuache mawazo mgando ya kukaririwa tuwe na hoja zenye mashiko.
 
  • Thanks
Reactions: bne
Back
Top Bottom