Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,306
- 25,929
CHADEMA naitafsiri kama taasisi ya wathubutu,wakosoaji kwa kutumia hoja mujarabu na wapambanaji dhidi ya ufisadi na wizi wa mali za umma. Ni taasisi iliyojengwa na kuheshimika,kwa kuzoa maelfu ya wanachama kwa namna hiyo
CHADEMA ilipendwa na vijana makini na wasomi kwakuwa waliiona Tanzania waitakayo kupitia chama hicho kikuu cha upinzani nchini. CHADEMA ilikuwa taasisi ya kuwasemea wanyonge;kuwaumbua mafisadi;kuwakemea viongozi na kuandaa viongozi wajao. Ilikuwa CHADEMA ya kupigiwa mfano na kuaminika.
CHADEMA imebadilika baada ya kuhamia humo kwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu,Edward Ngoyai Lowassa. Sasa,imeanza kupoteza-tena kwa kasi sifa na vivutio nilivyovieleza hapo mwanzo. Lowassa alihamia CHADEMA na watu wake. Kwa maneno mengine,alihamia na 'chama chake'. Tayari yeye na watu wake wameshachomoza na kushika nafasi mbalimbali ndani ya CHADEMA.
Kadiri Lowassa anavyojikita na kujiimarisha,ndivyo 'ile CHADEMA' inavyopotea. Kilele cha kupotea kwa CHADEMA ile kitakuwa wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani ya CHADEMA. Hapo patakuwa ni kati ya chama cha Lowassa na chama cha CHADEMA!
Kwaheri 2016,karibu 2017!