Kadiri Lowassa anavyojiimarisha CHADEMA, ndivyo chama kinavyofifia na kupotea

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,174
25,446
CHADEMA naitafsiri kama taasisi ya wathubutu,wakosoaji kwa kutumia hoja mujarabu na wapambanaji dhidi ya ufisadi na wizi wa mali za umma. Ni taasisi iliyojengwa na kuheshimika,kwa kuzoa maelfu ya wanachama kwa namna hiyo

CHADEMA ilipendwa na vijana makini na wasomi kwakuwa waliiona Tanzania waitakayo kupitia chama hicho kikuu cha upinzani nchini. CHADEMA ilikuwa taasisi ya kuwasemea wanyonge;kuwaumbua mafisadi;kuwakemea viongozi na kuandaa viongozi wajao. Ilikuwa CHADEMA ya kupigiwa mfano na kuaminika.

CHADEMA imebadilika baada ya kuhamia humo kwa Waziri Mkuu aliyejiuzulu,Edward Ngoyai Lowassa. Sasa,imeanza kupoteza-tena kwa kasi sifa na vivutio nilivyovieleza hapo mwanzo. Lowassa alihamia CHADEMA na watu wake. Kwa maneno mengine,alihamia na 'chama chake'. Tayari yeye na watu wake wameshachomoza na kushika nafasi mbalimbali ndani ya CHADEMA.

Kadiri Lowassa anavyojikita na kujiimarisha,ndivyo 'ile CHADEMA' inavyopotea. Kilele cha kupotea kwa CHADEMA ile kitakuwa wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani ya CHADEMA. Hapo patakuwa ni kati ya chama cha Lowassa na chama cha CHADEMA!

Kwaheri 2016,karibu 2017!
 
Inasikitisha sana lakini ndio hivyo tumeweka pamba masikioni.

NCCR ile ya wasomi hadi akina Tundu Lissu kujiunga ilianza kupotea kidogo kidogo hadi kufikia hatua hii. Msisubiri Chadema ifike huko ....tukiendelea kukejeliana tunaoikosoa mwelekeo wa Chadema hii ya sasa ....hatutajenga ufa bali ukuta.
 
Mbowe ni tatizo jumlisha na lowassa unakuwa mzigo mkubwa wenye ufundo wa kutosha.
Ni muda wa kufanya mabadiliko ndani ya CHADEMA , vijana makini wako ndani ya Chama lakini awatumiwi.
[HASHTAG]#malisa[/HASHTAG]
[HASHTAG]#yericko[/HASHTAG]
Na hata Ben asiye julikana aliko sasa, hawa wamekuwa wapiga debe tu mtandaoni lakini ndani ya Chama nafasi yao ni finyu sana.

#Mabadiliko_yaanzie_ndani_ya_chama_kwanza.


#Mbowe_ni_tatizo_ndani_ya_chama.
 
Siasa za boys to men zimepita. JK na Lowassa wastaafu siasa. JK kastaafu, kafanya makubwa ndani ya serikali na chama chake. Lowassa naye kafanya makubwa ndani serikali na Ccm na pia kaisaidia chadema kupata wabunge wengi. Lowassa staafu siasa baba yetu. Tunaitaka CHADEMA ya awali.

Tunamtaka Mnyika yule..tunamtaka Mnyika yule.. Yule mnyika. Siyo huyu. Siwezi kumlaumu Mbowe, mbowe hajawahi kuwa mwanasiasa mzuri but ni kiongozi / management mzuri but not charismatic leader.
 
Kazi ya wataalam ni kuchambua hali halisi na kazi ya watendaji ni kuandaa sera na kutekeleza. Huu uchambuzi uko vizuri sana.

Ila wasiwasi wangu ni wale wanaoona kila uchambuzi ni kinyume na chama au kiongozi fulani hasa wa upinzani.

Nafikiri CHADEMA inaweza okolewa na sisi tusiotaka vyeo na tunataka chama kisimame kabla ya kusimamia.

Tunahitaji fikra mbadala za chama na kuwaambia kwa uwazi Mbowe na EL wasitafute vyeo tena humo ndani, maana walipofikisha chama 2015 inaonyesha ni hatua za mwisho kabisa za ukuaji wa upinzani Tanzania.

Tunahitaji viongozi watakaofikiri tofauti na kwenda na changamoto mpya na mawazo mapya.

Heri ya mwaka mpya wote.
 
Mkuu nyabhingi kipi ni bora kati ya kura za Lowassa na kuimarika kwa CHADEMA?
Kwani indicator(s) ya kuimarika kwa chama ni zipi? Nilidhani mojawapo ni kuongezeka kwa kura(urais na wabunge+madiwani na wenyeviti wa mitaa).

I can agree with you tokea Lowassa ajiunge CHADEMA na huyu Mashinji kuwa Katibu Mkuu chama kimedoda sana,wamekuwa waoga na serikali hii haiwaogopi kabisa. Unaweza kufikiri Lowassa katumwa kufifisha harakati. Magamba hayahitaji siasa za kiustarabu kabisa,ni mpelampela wa Lissu na Lema ndio unaotakiwa,yani hadi Salum Mwalimu kawa mdogo!!!
 
Inasikitisha sana lakini ndio hivyo tumeweka pamba masikioni. NCCR ile ya wasomi hadi akina Tundu Lissu kujiunga ilianza kupotea kidogo kidogo hadi kufikia hatua hii. Msisubiri Chadema ifike huko ....tukiendelea kukejeliana tunaoikosoa mwelekeo wa Chadema hii ya sasa ....hatutajenga ufa bali ukuta.
Haha usingetokea kwenye Uzi huu ningeghairi kuingia 2017.....
 
Umenikumbusha mbali sana...!!wako wapi makamanda wa vita vya UFISADI.!Wako wapi waliokuwa wakidai katiba mpya wakimaanisha..!Aah siwaoni bali nawaona wamejaa ndumila kuwili ..!
BYE BYE 2016! Muwe na mwaka mpya 2017 wenye mafanikio Lakini sio kwa mafisadi!!!
 
Hakuna chami kinaweza imarika kwa itikadi na wanaharakati, kama huamin muulize Malema wa SA.
Btw siasa bila pesa, connection na ujanja kwa Africa ni kutwanga maji kwenye kinu. ..Muulize Brother Zitto. ....
 
32 Reactions
Reply
Back
Top Bottom