Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini ameishauri serikali kupitia upya uamuzi wa kuyafutia msamaha mashirika ya dini na asasi za kiraia. Akizungumza jana na gazeti dada la Daily News, alisema taasisi hizo hazitengenezi faida na badala yake, zipo kwa ajili ya kuwainua watu wa kawaida ambao ni masikini. Alitoa mfano wa huduma za afya zinazotolewa hususan maeneo ya vijijini, ambazo nyingi hutolewa na taasisi za dini.
Serikali ilipaswa kukaa na wadau kwa ajili kupata ushauri juu ya hasara na faida ya kuondoa msamaha huo kabla ya kutangaza bajeti yake, alisema Kilaini. Wakati huo huo, Naibu Katibu Mkuu (masuala ya dini) wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA), Mohamed Khamis alisema uamuzi huo unakwamisha sera ya Taifa ya kuwapa maisha bora wananchi.
Hii hisije kuwa ni hasira ya kuondolewa ulaji wa kusamehewa kodi.
HabariLeo | Viongozi wa dini waomba msamaha wa kodi upitiwe
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-na-mashehe-wanafiki-mmevuna-mlichopanda.html
He needs to walk the talk kama mwenzake wa Zimbabwe alivyofanya. Kamkemea nani kwa jina katika hii martyrdom anayoitafuta? Na wengine wanaotuhumiwa si kondoo wake?
Amandla............
Ok, lets say Pengo hana nia blah blah blah na ni msanii.
Now lets talk sense and straight..ulitaka afanye kitu gani ili wewe roho yako iridhike kuwa si msanii? Je alikuahidi nini ambacho hajakitekeleza? Ni wajibu upi ambao ninyi msio waumini mlimpa mpaka mumdai kuwa hajafanya a,b,c na hivyo kustahili kuitwa msanii?
Naomba majibu mujarabu
anatuzuga, nguvu aliyonayo ni kubwa sana, akiwapa modality mapadri, CCM inang'oka..
Mhashamu Cardinal Pengo, nashukuru sana kwa yeye kuamua kuwa shahidi wa watanzania na kuamua kumwaga damu yake kwa ajili yetu, good move.
sasa haya ndiyo anatakiwa ayakabili, aseme wazi Mkapa alitumia madaraka yake vibaya na amelisababishia taifa hasara kubwa hivyo anatakiwa apandishwe kizimbani.
Pili Msiminary Chenge kalitia aibu kanisa kwani wizi anaoufanya haundani na mafundisho ya kanisa anatakiwa apandishwe kizimbani bila ya kuonewa huruma.
tatu atengue kauli yake kwamba Kikwete ni chagua la mungu na aweke wazi kuporomaka kwa maadili ya uongozi wizi na rushwa iliyokithiri ni matokeo ya uongozi mmbovu wa rais J. Kikwete kwani wanaoharibu ni watu aliowachagua.
Tatu aitishe kikao na viongozi wengine wa dini mbali mali na wazungumzia mustakabali wa nchi na kila mmoja kwa uwazi ajadili na kuweka mikakakti ya kuwaeleza waumini wao nini wanatakiwa kufanya.
Atuambie nini wakikutana na Kikwete huwa wanamwambia na atuambie ni kitu gani kilimsukuma kwenda kufungua kitabu cha fisadi Lowassa akitumia jina la mkewe.
Unafiki ndio unatumaliza tanzania.
Tatizo letu humu JF wengi wetu ni kutoatu lawama zisizo na kichwa wala miguu. Huku tunataka viongozi wa dini wasiguse mambo ya 2010 kuhusu kuwahamasisha wananchi wajiandikishe na kupiga kura kwa makini, at the same time tunawalalamikia eti ni ufisadi umeshamiri.
Sasa wewe unasema akiwapa modality ya kuing'oa CCM, huoni huku ndio kuchanganya siasa na dini?