Kadi ya mpiga kura - Hakiki taarifa kupitia simu yako

LazyDog

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
2,473
189
Piga namba *152*00# na ufuate maelekezo. Au Bonyeza HAPA Kuhakiki


Mimi napata ujumbe ufuatao kila mara:
"Tumeshindwa kuitambua namba ya kadi, tafadhali jaribu tena au fika na kitambulisho chako wakati wa zoezi la uhakiki taarifa katika kata uliyojiandikisha."

Huenda taarifa za mkoa nilipo bado hazijaingizwa kwenye daftari kuu.
Ni mikoa gani usajili haujakamilika?

Imetumika gharama kubwa ya walipa kodi kuileta hii system ya BVR - ili kuona kama mfumo huu unafanya kazi kama wanavyotaka tuamini, jaribu na wewe kupiga namba iliyopo hapo juu tafadhali.

UPDATE - Agosti 1
Kwa kuwa wengi wametahadharisha kuhusu jambo hili (mimi sina shaka bado) mwenye wasiwasi asubiri kwa muda ajiridhishe kwamba haina madhara.

Taarifa ya namba tajwa hapo juu, aliitoa Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Dr. Sisti Cariah (mwenye tai pichani) kwenye taarifa ya habari ya ITV ya saa mbili na ya saa tano usiku juzi Alhamisi, Julai 30.
Itawezekanaje tume wenyewe watumie njia ndefu kukusanya namba kupitia simu au website ilhali namba zote tayari wanazo?
(Utaratibu wa kuhakiki taarifa upo pia kwenye website ya tume).

ANGALIZO:
Kabla ya kusambaza taarifa yoyote itakayokufikia leo, kesho au baadae, jiulize, Je, chanzo cha habari uliyotumiwa kinaaminika? Mimi siamini taarifa yoyote ya kuambiwa mpaka niione ITV. Hata hao ITV nawaamini kwa asilimia 95 tu, sio mia kwa mia.

Mwisho ndugu zangu, kama kuna habari ya kusambazia wengine, ni kuwaeleza umuhimu wa zoezi la kuhakiki taarifa zao mapema kabla ya siku ya kupiga kura. Zoezi hili ni muhimu kuliko kikadi ulicho nacho mkononi.
Usipuuze kwenda kuhakiki taarifa kwenye daftari litakapoletwa kituo ulipojiandikisha.

Dr. Sisti ameeleza kwamba, kura tutapiga kama tulivyofanya miaka ya nyuma (manually) na sio kielektroniki na alieleza kwanini manually.

Naamini tutachovya kidole kwenye wino, utaratibu ambao umekuwa ukitumika kujua nani kapiga kura au nani bado. Ameeleza pia kwamba mikoa tisa tayari madaftari yamefika.

Kwenye kipima joto nilijifunza kwamba, kama tume walishindwa kukuandikisha kwa kisingizio chao chochote cha hovyo, hujachelewa. Unayo fursa ya kupiga kelele taasisi za kiraia zijue. Mwananchi wa kawaida au kwa makundi au kwa kuwakilishwa, wanaweza kuiburuza tume mahakamani na kushinda.


UPDATE - Agosti 11
Sasa napata taarifa za usajili wa kadi yangu vizuri tu tofauti na nilivyoelezea awali hapo juu. Taarifa nazipata kwa kupiga namba *152*00#, hali kadhalika kwa kutumia website ya tume. Ukipata error meseji, subiri kwa muda na ujaribu tena.

Jana ndio nimesikia kwenye TV kwamba kwa mkoa nilipo, siku ya mwisho ya kuhakiki ni leo.

Uhakiki wa Taarifa Katika kurahisisha uhakiki wa taarifa,

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeweka Mfumo utakaowarahisishia Wapiga Kura kukagua taarifa zao. Mfumo huu umekuwa ukitumika tangu mwaka 2005 na Umetumika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Mfumo huu SIYO MFUMO WA UPIGAJI KURA NA HAUNA UHUSIANO NA UPIGAJI KURA kwani Upigaji wa Kura utafanyika kama chaguzi zilizopita kwa kutumia Karatasi za Kura (Ballot Paper) ambazo huesabiwa katika Vituo vya Kupigia Kura (Polling Stations) na matokeo yake kubandikwa katika Vituo hivyo vya Kupigia Kura.

Mfumo unamwezesha Mpiga Kura kuhakiki taarifa zake au kujua kituo chake cha kupigia kura popote Mpiga Kura alipo badala ya kwenda katika Ofisi za Kata kufanya Uhakiki. Mpiga Kura mwenye simu ya aina yeyote au anayeweza kutumia Tovuti ataweza kuhakiki taarifa zake mahali popote atakapokuwa kwa njia zifuatazo.

1. Ujumbe mfupi kwa njia ya simu (SMS)

2. Tovuti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi

(a) UJUMBE MFUPI KWA NJIA YA SIMU YA MKONONI (SMS) Njia hii ni ya kutumia simu za Mkononi (Cellular Phones).

Mpiga Kura ataingiza namba iliyochapishwa katika Kadi yake ya kupigia kura katika simu na taweza kuhakiki taarifa zake. Maelekezo ya kutumia njia ya SMS kuhakiki taarifa ni kama ifuatavyo;

I. Bonyeza namba *152*00#

II. Chagua namba 2 inayoonyesha "Uchaguzi mkuu 2015"

III. Baada ya hapo chagua namba (1) Kuhakiki taarifa au namba (2) kutoa taarifa ya kitambulisho chenye kasoro

IV. Iwapo namba 1 itachaguliwa yaani uhakiki wa taarifa, utatakiwa kuingiza namba ya iliyochapishwa katika Kadi ya Mpiga Kura bila kuandika T au alama (-) mfano T-1001-2692-028-9 itaandikwa 100126920289 hivyo bonyeza kitufe reply ili kuingiza namba hiyo

V. Baada ya hatua hiyo utatakiwa kuingiza namba 1 kukubali au namba 2 kughahiri 5

VI. Ukichagua namba (1) Ujumbe utapelekwa katika Mfumo na utapatiwa ujumbe wa kusubiri taaarifa zako iwapo zipo katika Daftari. Ukichagua namba 2 utaondoka katika Mfumo.

VII. Iwapo Upo katika Daftari taarifa zako zitarudishwa kama zilivyoingizwa katika Daftari hivyo unatakiwa kuzihakiki kama zipo sahihi. Iwapo zipo sahihi unaweza tu kuondoka katoka mfumo. Iwapo zitakuwa zimekosewa unatakiwa kuonyesha na kwenda katika Kata au Halmashauri yako na kuzirekebisha na kupatiwa kitambulisho kingine wakati wa zoezi la kuweka wazi Daftari.
 

Attachments

  • NEC.jpg
    NEC.jpg
    43.2 KB · Views: 1,099
  • akl.jpg
    akl.jpg
    43.1 KB · Views: 3,584
Hata mie nimejaribu ya kwangu imeniambia hivyo ila natoa angalizo yoyote atakayenizuia kupiga kura kwa sababu yeyote ile ajiandae matachimbwa shimo kubwa sana kituoni na ama zangu ama zake mmoja lazima atarest in peace.
 
Kuweni makini,hiyo ni plan ya ccm,watachukua number za kitambulisho,siku unaenda kupiga unaambiwa mbona ulishapiga tayari
 
Ujumbe huo ni silaha ya maangamizi ya CCM jihadhari nao.


Jamaa wa NEC walitoa ufafanuzi ya Jana kwenye kipindi cha kipima joto ITV ya ya kwamba , unaweza kucheki taarifa zako pale utakaposikia nkoa wako umetajwa ya kwamba wameshabandika daftari na sio vinginevyo. Pili walisema namba hii inasaidia kuondoa usumbufu wa kwenda kwenye ofisi uliyojiandikisha kuangalia kama jina lako lipo. Wewe usipohakiki taarifa zako unaweza ukajikuta hupigi kura kwani mamifumo hua hayatabiriki. Kingine walichosema nikutotumika kwa upigaji kura kwa njia ya kieletroniki kwa hiyo ni kama awali upigaji kura utafanyika. Na mwisho walisema hii namba itatumika baadae kujua kituo cha kupiga kura, usipotaka kuitumia uende kwenye ofisi za kata au mtaa ukasome jina lako kujua kituo chako....haya hapa nimepita tuu...mengine hao waseme wenyewe....
 
Piga namba *152*00# na ufuate maelekezo.


Mimi napata ujumbe ufuatao kila mara:


Huenda taarifa za mkoa nilipo bado hazijaingizwa kwenye daftari kuu.
Ni mikoa gani usajili haujakamilika?

Imetumika gharama kubwa ya walipa kodi kuileta hii system ya BVR - ili kuona kama mfumo huu unafanya kazi kama wanavyotaka tuamini, jaribu na wewe kupiga namba iliyopo hapo juu tafadhali.
Pole ndugu yangu tayari umeshaliwa huu ni wizi sawa na wizi mwingine wa mitandaoni, sawa na kutoa particulars zako za kibenki ikiwemo namba ya siri kwa mtu usiyemjua.

Lubuva amesema Tume itatoa maelekezo ya jinsi ya kuhakiki kadi yako kwenye kituo ulichojiandikisha na sio vinginevyo, kasema kwa sasa wanaotuma hizo meseji ni matapeli.
 
Acheni kutapeliwa na namba za wezi wa mitandaoni ili kufanikisha goli la mkono, km umejiandikisha una wasiwasi gani subiri tarehe ukapige kura yako. Au nenda kituo uicjoandikisha ukuhakiki hapo kwenye daftari. Msije juta bure.
 
Yani kadi yangu nimeivundika kwenye kabati mbali sana yani nitaitoa october 24 kama mwali kwa sherehe kubwa .. october i love u
 
Mimi nilijiandikisha Mbeya, na sasa nipo Kilimanjaro hadi hyo october wakati wa kupiga kura, vipi nitaruhusiwa kupiga kura hukuhuku? Maana naona kama ntaikosa haki yangu hivihivi mwaka huu.
 
Subiri utahakikisha kwenye daftari.
Vinginevyo utajikuta 'umeshapigishwa kura' na magamba.
 
TAHADHARI/ONYO USIPIGE NAMBA HIYO. Hizo Ni Mbinu Za Goli La Mkono. SIKU YA UCHAGUZI UKIENDA AMA UTAAMBIWA UMESHAPIGA KURA AMA KITAMBULISHO CHAKO HAKIONEKANIKI KWENYE SYSTEM. Ulipoenda Kujiandikisha Taarifa Zako Uliwapa Wewe Mwenyewe Na Walikuwa Wanakuuliza Mara Mbili Kuwa Hz Taarifa Zako Ni Sahihi.Ukathibitisha Ni Sahihi Kwa Kuweka Saini, Sasa Iweje Tena Leo Wakwambie Upige Namba Hiyo Ili Uhakiki Taarifa Zipi Wakati Ulihakiki Palepale Wakati Ulipokuwa Unajiandikisha? MSIPIGE HY NAMBA KISHA UKAWAPA NAMBA YAKO YA MPIGA KURA TAMBUA HAYO NI MAANDALIZI YA GOLI LA MKONO.
 
Back
Top Bottom