Kada wa CCM lupango kwa kubaka

Mtu

JF-Expert Member
Feb 10, 2007
469
42
Kada wa CCM afungwa kwa kubaka


na Charles Ndagulla, Moshi

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mfanyabiashara maarufu mjini Moshi, Fred Minja (60), amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa darasa la nne.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkuu Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Mkoa, Geni Dudu, baada ya kuridhika na ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo.

Sambamba na hukumu hiyo, Hakimu Dudu aliamuru mshitakiwa huyo kuchapwa viboko 12.

Hata hivyo, mahakama hiyo haikumuona na hatia mshitakiwa huyo katika shitaka la kumwingilia mwanafunzi huyo kinyume cha maumbile.

Kwa mujibu wa ushahidi uliowasilishwa mahakamani hapo, siku ya tukio mshitakiwa huyo alimkamata mwanafunzi huyo aliyekuwa ametumwa dukani na kumwingiza ndani kwake na kumbaka na kupewa vitisho kuwa atauawa iwapo angepiga kelele.

Wazazi wa mwanafunzi huyo waligundua hilo baada ya kushindwa kufanya kazi za kuinama kama kufanya usafi wa ndani.

Akitoa utetezi wake mshitakiwa huyo alikiri kumfahamu mtoto huyo kama ndugu, na mtoto wa jirani yake na kwamba wakati tukio likitendeka alikuwa kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.
Source:Tanzania daima


Hii wanayofanya ni huwa wamezidiwa au kuna masharti kutoka kwa "Babu"? haingilii akilini kummuingilia mtoto wa darasa la 4
 
kampeni ya uchaguzi 2005 ilikuwa ya vyama vingi. sasa u ccm unatoka wapi hapo jameni. tuwe objective.

macincus
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom