Kaburi lafukuliwa, maiti yaibwa

Kaburi lafukuliwa, maiti yaibwa

Rebo Tz

Senior Member
Joined
Sep 26, 2016
Posts
169
Reaction score
125
Chunya.
Wakazi wa kitongoji cha Malangamilo kwenye mji mdogo wa Makongolosi wilayani hapa, wameingiwa kiwewe baada ya kubaini kaburi la mtu waliyemzika limefukuliwa na mwili kuibwa.

Maiti ya Elias Baswedi (33) iliyozikwa kwa taratibu zote kwenye mji huo, imefukuliwa na kuibwa kabla ya kupatikana baadaye porini ikiwa imekatwa mguu.
Baswedi alifariki dunia baada ya kupigwa na kuchomwa moto na watu wasiojulikana Ijumaa usiku na alizikwa na ndugu zake baada ya kupata kibali cha polisi.
Siku mbili baada ya maziko, baadhi ya wakazi waliopita eneo alipozikwa walishangaa kuona kaburi likiwa limefukuliwa na ndani yake hakukuwamo maiti na vitu walivyomzika navyo kama vile sanda na mkeka.

Pangapanga Baswedi ambaye ni kaka wa marehemu, amesema tukio hilo liliwaongezea uchungu na walitoa taarifa polisi kwa ajili ya kuwasaka waliotoweka na maiti hiyo.
Mwili huo baadaye ulipatikana porini ukiwa umekatwa mguu.
 
Sasa hao waliokata mguu wake sijui ndo wanaenda kuutumia kwa kazi ipi! Makubwa haya. Poleni kwa wafiwa.
 
Kweli huu ndio utofauti uliopo baina yetu wanadamu, yaani maamuzi hayo yanawezekanaje? Poleni wafiwa!
 
Sasa hao waliokata mguu wake sijui ndo wanaenda kuutumia kwa kazi ipi! Makubwa haya. Poleni kwa wafiwa.
Kwanisi chunya wanachimba madini?

Wachimba madini ni watu qenye imani za ajab sana*!
 
Adui ujinga bado anaendelea kutesa wananchi, mbona wazungu ni wachimba madini na upuuzi huo hakuna?
 
Kuna watu wana imani ya ajabu sana...

Ova
 
Siku ya hukumu Mungu ataweka screen kubwa alafu kila mtu ataonyeshwa matendo yake yote.
 
Halafu ndio mkoa wenye makanisa mengi.

Hapo ni Imani za kishirikina zimehusika.

Mguu wapeleke kwa mganga ukafanyiwe dawa ya kufanyia biashara.
 
Back
Top Bottom