PreGE2025 Kabudi ahoji Kura ya Ndiyo au Hapana ni 'reform'?

PreGE2025 Kabudi ahoji Kura ya Ndiyo au Hapana ni 'reform'?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Palamagamba Kabudi amesema Tanzania imepiga hatua kubwa chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, kwani kwenye Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Serikali yake imeridhia mabadiliko katika ule utaratibu wa kupita bila kupingwa.

Snapinst.app_486528123_636800042315447_4142732531721408517_n_1080.jpg
Akizungumza Jijini Arusha wakati wa mdahalo katika kongamano la kupongeza miaka minne ya mafanikio ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Waziri Kabudi amesema viongozi hao wote hivi sasa ikiwa akisalia mwenyewe kwenye mchakato wa uchaguzi atapigiwa kura ya ndiyo au hapana jambo linaloifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza duniani ambayo imeruhusu utaratibu huo ili kuimarisha zaidi demokrasia.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Tanzania ndio nchi ya kwanza Duniani ambayo sasa mwenyekiti wa kijiji, kitongoji, diwani, mbunge na Rais akiwa peke yake kwenye uchaguzi anapigiwa kura ya ndiyo au hapana. Uingereza hadi sasa anapita moja kwa moja, sasa watu wanasahau kule kupita bila kupingwa tuliletewa na waingereza lakini sisi tumekwenda mbele ya waingereza kwamba sasa wewe ukibaki peke yako lazima upigiwe kura. Kwa mabadiliko hayo, Je! reform hiyo ni ndogo au kubwa?", amehoji Profesa Kabudi

"Na uchaguzi huu wa viongozi wa vijiji kuna ambao kura za hapana zilikuwa nyingi kuliko ndiyo, Naibu Katibu Mkuu hayo watu waelezwe kuna ambao hapana zilikuwa nyingi na uchaguzi ulirudiwa…Je!, hiyo ni reform au sio reform?". ameendelea kuhoji Profesa Kabudi
 
Nadhani Kabudi atakuwa amevunja rekodi kuwa profesa wa kwanza kuwa mjinga.

Hiyo kura ya NDIYO na HAPANA, mwulizeni huyo mjinga, kura za hapana, wakala wake huwa ni nani?

Hawa ni wale wajinga wanaoamini kuwa wana akili sana. Wanaamini wametumia sana akili kuwahadaa watu.
 
Unawekewa pingamizi na pandikizi la chama kama TPP unaenguliwa anabaki mgombea wa CCM peke yake tume inasema haijaweka pingamizi wakati kiuhalisia ni kitu kile kile.
 
Hawa kina Kabudi wakishaongea mambo kama haya mbele za watu wanaporudi makwao wanasikitika sana kwa damage wanayokuwa wameifanya sema hawana la kufanya.
Nina uhakika hata wakiwa wanakata roho watakuwa wanasikitika mno kwa ujinga walioutete na kuupalilia
 
Sisi sio wajinga, hapo ni unafiki tu.
Nataka mwenye akili aje na suala la uenguaji wa wagombea likoje,
Utekwaji wa wagombea likoje
Kuja na matokeo ya kubumbwa hali ikoje,
Kuandikisha watoto wa shule suala hilo likoje,

Hatutaki mambo ya mapambio asubuhi, mchana na jioni, hao tumewazoea ni walinda matumbo yao na ndio maana kila siku wao ni kusifu tu hata visivyosifika, TUMEWACHOKA, MMETUKINAI
 
Back
Top Bottom