Kabla ya ndoa na kufa ni vizuri sana kujipanga ili kuepuka mambo kama haya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kabla ya ndoa na kufa ni vizuri sana kujipanga ili kuepuka mambo kama haya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Mar 3, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam leo itatoa uamuzi ya sakata la kugombea kuzika mwili wa marehemu Salum Ngindo unaogombewa na mkewe anayetaka uzikwe Kiislamu huku watoto wa marehemu wakitaka azikwe kwa imani ya dini ya Kikristo.

  Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Afumwisye Kibona baada ya mke wa marehemu, Kudra Salum kufungua kesi ya madai dhidi ya watoto watano wa marehemu mumewe aliyefariki Februari 24, mwaka huu katika Hospitali ya Hindu Mandal wakidai kuuzika mwili wa baba yao Kikristo.

  Watoto hao ni Matukuta Ngindo, Rose Ngindo, Nono Ngindo, Matukuta Ngindo na Gloria Ngindo.

  Wakili wa upande wa Mashitaka, Mussa Roma alidai marehemu aliachana na mke wa kwanza ambaye ni mama wa watoto hao, miaka mingi iliyopita na kufunga ndoa ya Kiislamu na mke wa pili ambaye ni mlalamikaji.

  Alidai awali marehemu alifahamika kwa jina la Gerard Ngindo, lakini baada ya kubadili dini alifahamika kwa jina la Salum Ngindo na kufunga ndoa ya Kiislamu na Kudra, Februari 10, 1994 na kuzaa naye watoto.

  Alidai kuwa hata baada ya kuishi pamoja, baadaye marehemu aliugua na mlalamikaji ndiye aliyemuuguza kwa kipindi cha miaka sita na baada ya kufa, alitoa taarifa kwa ndugu na watoto wa marehemu kwa ajili ya msibani.

  Alidai siku waliyopanga kwa ajili ya maziko, walikwenda katika Hospitali ya Hindu Mandal kuuchukua mwili, lakini baada ya kufika walikuta watoto hao wakiwa na kibali cha kuuchukua mwili kwa ajili ya kuuzika.

  Naye Wakili wa utetezi Stephen Tonya alidai marehemu alitumia jina la Salum kama umaarufu, lakini alifahamika kwa jina la Gerard ambalo ni la Kikristo alilozaliwa nalo na hivyo ana wajibu wa kuzikwa Kikristo.

  Wakili wa Mashitaka aliwasilisha cheti cha ndoa kati ya marehemu na mlalamikaji ambapo hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi leo atakapotoa uamuzi wa kuzikwa kwa mwili huo.
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,938
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wazo la kujipanga kabla ya kufa,
  ili kupunguza mifarakano baina ya ndugu utakawo waacha
  Lakini mimi binafsi kila nikitaka kuandika wosia huwa naogopa sana
  nahisi kama najitabiria kifo mapema ingawa sijui nitakufa lini.

  Lakini kwa kesi hii, sidhani kama watoto wana haki ya kuuzika mwili kama wanavyotaka wao
  kwani marehemu hadi anakufa inaonekana alikuwa katika dini yake mpya.
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ishu hiyo nimeisoma nikaona ni nzito sana basi kama mtu utaandika wosia ni muhimu pia kuandika kwamba ukifa uzikwe wapi na kwa dini ya dhehebu gani kwasababu hili ni tukio lapili nadhani kama unakumbuka miezi michache iliyopita kulikuwa na sakata kama hili lililosababisha kaka wa mke kufariki baada ya kudondoka pale mahakama ya kisutu!
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,486
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Yaleyale..mijitu mingine sijui ni vp aisee.
   
 5. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,911
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  Ndugu zanguni wosia ni muhimu hasa pale ambapo umefanya maamuzi makubwa kama haya ya kubadili dini. Hata kwa wale ambao wameoa mke mbali na mila na taratibu za kabila lake ni lazima afafanue wazi azikwe wapi maana imetokea mara nyingi kuwa ndugu wanataka ndugu yao azikwe kijijini kwao huku mke akitakwa azikikwe manispaa wanazoishi. Hii inaleta mzozo na kutokuelewana.

  Kwa upande wa mali na pesa au mafao tunayoacha ndiyo kasheshe kabisa. Hebu tuamke kabisa na kuachana na kasumba kuwa ukiandika wosia eti unakaribisha kifo. Mbona wenzetu wazungu wanaandika wosia na ku-reviw kila jambo jipya au kuiongezeka/kupungua kwa rasilimali zake kwani wameshakufa? Wanaishi so many years na wosia copies kibao na ndipo ile latest ndiyo inatumika katika utaratibu wa urithi. Tuzinduke sasa!! Anza wewe!! Washauri wengine!!!
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Mar 3, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,881
  Likes Received: 4,424
  Trophy Points: 280
  Wosia ni kitu cha muhimu sana, kwani jamaa angekuwa kaandika wosia haya mambo yasingefika hapa yalipo. Tuache kuogopa kuandika wosia ili tutakapokufa tuwaache ndugu zetu waishi kwa amani.
   
 7. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #7
  Mar 3, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  maane nakuunga mkono 100%hoja yako imepita man!
   
 8. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,561
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  kiukweli ni muhimu sana kuandika wosia kuepuka matatizo baada yakwenda kwa baba
   
 9. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #9
  Mar 3, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  hivi ile ya kisutu ni upande gani ulishinda maana nilisikia tu kuwa kaka wa marehemu naye kafa ghafla.
   
 10. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2010
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  Binafsi namfahamu sana Bw Salum Ngindo kama muislam. Ki kweli kabisa ameacha watoto saba. Wa ndoa ni mmoja tu.

  Nyumba yake iliyopo Mikocheni B ipo next to my house. Mwanamke wake wa Kwanza alizaa nae watoto 3 lakini hakuwahi kumuoa naye alikuwa mkristo. Alipokwenda Moshi alizaa na mwanamke mwingine wa kiislam watoto 3. Na nakumbuka 1993 alifanikia kuoa mkewe wa sasa na alibadili dini na kuwa mwislam. Ninavyofahamu alizaa nae huyu mwanamke mtoto mmoja anayeitwa Adam.

  nafikiri kama huyo wakili angewauliza hao watoto walete vyeti vya ndoa vya mama zao kama ushahidi hapo mahakamani.

  Mara nyingi sana nimekuwa naenda kumuona kwake kule tabata Chang,ombe karibu na nyumba ya miss Tanzania. Unaingilia sehemu moja inayoitwa Sanene na kufata njia ya mnara wa voda mpaka kwake.

  Sitaeleza mengi kwa sababu kesi ipo mahakamani.

  Lakini kifupi wanaogombea wanataka mali na si vinginevyo.

  Ina Lillahi wainna Ilaihi rajihunna.

  Wosia ni Muhimu sana.
   
 11. d

  damn JF-Expert Member

  #11
  Mar 3, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Yaani acha tu!!! what does it make a difference kwa maiti akizikwa kwa kiislamu au kikristo. Ni bora kuzikwa na ndugu, marafiki na wapendwa wote waliokuwa karibu nawe bila ya kuwa hotuba zozote za kidini. Ibada iwe ni ya kueleza mazuri au mabaya uliyoyafanya.
  Huu upuuzi unakera sana!
   
 12. d

  damn JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 585
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hivi wosia huwa unaandikwa hata style ya maziko?
   
 13. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hapana wewe unasema tu ikitokea mungu akanipenda zaidi kuliko jamaa zangu basi mali zangu zitakuwa chini ya nani utazikwa wapi nk, huo ni mfano tu ila ukienda kwa wanasheria watakusaidia sana
   
 14. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,308
  Likes Received: 791
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa, tena nadhani nataka style ya kuchomwa "cremation" nadhani hiyo ni lazima niandike somewhere.
   
 15. upele

  upele JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2010
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 364
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hao wote wanataka mali za marehemu kwani alipo kuwa mzima hawakumuona alikuwa anaelekea kanisani au msikitini mambo mengine waswahili tunaendekeza wenyewe kote ni dhiki zetu
  tubadilike
  conquest
   
 16. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #16
  Mar 3, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Kadiri siku zinavyozidi kwenda ndio matatizo haya yanavyoongezeka.
   
 17. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #17
  Mar 3, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,318
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Ndibalema, hilo swala la kutokujua utakufa lini ndo linalosababisha uandike wosia, huna haja ya kuogopa kwani unajua utakufa tu. ni kweli watu wengi wanaogopa kuandika wosia wakidhani kuwa baada ya kuandika wanaweza kufa, hii sio kweli. na kwa kuogopa kuandika, ndo kunasababisha haya matatizo mengi yanayotokea. Mi naona hapa swala ni kubadilika, kwanza tukubali kuwa ipo siku tutakufa (hatujui lini) na hiyo ndo iwe changamoto ya kuandika wosia
   
 18. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,581
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  .........Wanaume kwa nini mnakuwa wagumu kuandika wosia? Ukiandika haina maana kwamba utakufa, kuna watu wameandika wosia wapo wanaishi miaka na miaka hadi pale Mungu atakapoamua kumchukua.
   
 19. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #19
  Mar 4, 2010
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Bi Kudra Salum alishinda kesi na Jana baada swala ya Maghribi (saa kumi na mbili na nusu jioni) Marhum Salum Ngindo tuliuzika katika makaburi ya tabata Chang'ombe.

  Kutakuwa na kisomo kesho baada ya maghribi msikiti wa Mangumi segerea.

  Inna Lillahi wainna Illaihi Rajihunna.
   
 20. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 17,560
  Likes Received: 5,124
  Trophy Points: 280
  Kwa kawaida tunamzika mtu kwa imani aliyokuwa nayo kabla ya kufa..... to me azikwe kiislamu. Cheti cha ndoa hakitaji mtu azikwe vipi..sana sanakinataja dini tuuu...........Na hao watoto wanaodai baba yao azikwe kikristu.......walikuwa wapi kumshawishi baba yao arudi kwenye ukristu kabla ya kufa...??? NIKIONACHO NI KWAMBA HIZO PANDE MBILI INAONYESHA ZILIKUWA NA UGOMVI HATA KABLA HICHO KIFO........... tukio la kifo limetumika tu kukuza tofauti zao........
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...