Kabla ya kuumba ulimwengu Mungu alikua anafanya nini?

Mpaka sasa kuna mabillion ya sayari lakini kile kifaa kinaitwa 'Kepler space craft' kishavumbua sayari kama 100 hivi ambazo zina size ya dunia na zenye uwezekano wa kuwa na maisha, wanaenda mbali zaidi na kusema kuna 'civilization' huko na ndio maana wanasisitiza kuwa 'we have been visited'.

Sielewi vizuri Quran inasema nini juu ya sayari zingine lakini kwenye Biblia Takatifu kuna sehemu Yesu alisema kuwa "Katika Nyumba ya Baba yangu kuna malimwengu (dunia) mengi" uthibitisho kwamba maisha hayako duniani tu.

Kama watu walioishi miaka 700 iliyopita waliamini kuwa dunia ndio kila kitu ni wazi watakaoishi miaka 600 ijayo wataweza kufanya maisha kwenye Mars au hata shemu nyinginezo!
 
"Hapo mwanzo mungu aliumba mbingu na nchi" na tumefundishwa Mungu hana mwanzo.

Sasa kabla ya kuumba ulimwengu mungu alikua anafanya kazi gani?
Fungua akili yako nikupe mfano.......
Chukua tone la mchanga ndio hii dunia(tuliyomo)
Matone yote ya mchanga duniani yako mangapi????
.............infinity............................
 
No one can tell with certainty what He was doing by then but,
Kabla shughuli nyingine hazijaanza huko peponi ilikuwa ni 'kuserebuka' tu, na Shetani ndiye aliyekuwa malaika anayegawa dozi ya burudani na mshika maiki kiongozi.

Kwa sasa tungeweza kusema alikuwa na umaarufu kama mzee Komba (rip) kwenye fani ya uimbishaji mpaka pale alipoharibu na kutumbuliwa jipu...
 
Unaweza ukajiuliza kuwa kabla ya wanadamu kujua kuwa dunia ilikuwa ikizunguka jua kwa siku 365 au kujizungusha kwa masaa 24 kwenye mhimili wake hizo events hazikuwepo!? Jibu litarahisisha swali lako.

NASA's Kepler mission Monday announced the discovery of 461 new planet candidates. Four of the potential new planets are less than twice the size of Earth and orbit in their sun's "habitable zone," the region in the planetary system where liquid water might exist on the surface of a planet.
kepler.jpg
 
"mimi ni ALPHA NA OMEGA mwanzo na mwisho" haya si maneno yangu bali ya BABA mwenyeenzi muumba "MUNGU"

INAMAANISHA;Mungu ndiye "mwanzo" sasa turudi katika hiyo nukuu ya biblia
"Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi"
inamaana kama Mungu ndiye mwanzo na hapo mwanzo ndipo alipoumba MBINGU Na nchi.......
ni kwamba hizo ndizo kazi zake za kwanza na bila yeye mwanzo usingekuwepo kwani mwanzo u ndani yake
KWA KUMALIZIA : Mungu ndiye mwanzo na hapo mwanzo aliumba mbingu na nchi...
maswali yanakaribishwa!!!!
 
"Hapo mwanzo mungu aliumba mbingu na nchi" na tumefundishwa Mungu hana mwanzo.

Sasa kabla ya kuumba ulimwengu mungu alikua anafanya kazi gani?
hatujaambiwa hicho kitu kutokana hatukuwepo
tabu kwa wale wanaoongelea mambo ya kale kwa uchunguzi wa kufanya leo
 
Nafikiri alikua vacation.... Somewhere in heaven's coco beach,relaxing and having some fun like let there be light.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom