Kabla ya kufikiria harusi, weka haya akilini!

Na huu ndio ukweli wengi ukiwauliza atakwambia anataka apate vyombo & vitu mbalimbali vya kuanzia maisha...ni uboya uboya!
 
 

Attachments

  • Things I Wish I’d Known Before We Got Married ( PDFDrive.com ).pdf
    1.2 MB · Views: 9
Mbona mtoa mada kasema hapo juu kama umejaaliwa kipato ama una marafiki wasio na pesa ya mawazo si mbaya kufanya sherehe kubwa tunachokikataa wengi wetu ni mtu kuanza kusumbua ilhali starehe ni yake mm nilifanya sherehe simpo tu kulingana na bajeti yangu sitaraji mtu kuja kunisumbua eti anaoa nimchangie sababu mimi sikuchangiwa na yeyote ukiwa na uwezo fanya ndugu ndio matumizi ya pesa tena mi nitakuona wa ajabu hela ipo halafu unajibana bana?
 
Ndoa Ina thamani zaidi ya sherehe lakini hii haimzuii mtu kufanya sherehe kubwa.
Kila mtu yupo na interest zake ..kuna wengine wanapenda sherehe,Kuna wengine hawapendi.
Cha muhimu watu wafanye wanavyotaka.
Hujakatazwa ndugu ila uwezo unao? au una kampani ya maana? Tunachokataa watu usumbufu mnaandaa bajeti ya Sherehe milioni 5 bwana harusi una 170,000 tu mfukoni si u*##@nge huu?
 
Hizo hela ugharamie wewe mwenyewe, usichangishe hata wana kamati.

Money is too important to be wasted in such manner!
 
Wanawake hawawez kuelewa ...
Mfano
Mi nilimweleza ishu kama uliyeisema ..
Jibu nililopewa
Linafurahisha sana ...
Acha ttu hawa wanawake hawa...
Nikaambiwa ivii
Iyoo hafla fupi itakuwaje ..na wale watyu wanaokuja kutunza zawadi itakuwaje ...
kwaiyoo yeye hatopokea zawadi ??
Aliniuliza kaswalii ...
Aahh nikabaki nafurahi tyuu
Ikabidi nami nimchokoze
Kwani zawadi zinamchango gani kweny harusi ...au umuhimu wake ni nn ??
Nikajibiwa ...
Zinafariji piah zinasaidia kunenepa
Daaa ..nilichoka sana
Ikabidi nikubali tyuu yaishee
Tuishi nao kwa akili kwa kweli...
 
Alafu mwanamke aje apa aanze kupinga haya akitaka sherehe kubwa badala ya kushukuru Mungu amepata Mume na Ndoa imetimia anaanza kuwaza Sherehe za Gharama reaaly!!?

Yani mimi kwa mawazo niliyo nayo ingewezekana siku ya Kuoa Muhimu ni Kanisani tu ndoa ifungwe baada ya apo nimchukue Wife twende ata sehemu hoteli ya standard na Ndugu wachache kutoka pande zote as you said 100 ivi wanatosha tukafanya ka party kadogo maisha yakaendelea hayo mamilioni si bora wangepewa wana ndoa wakaanzie maisha!!
 
Hahah mstari wa mwishk nimeupenda, ndugu mpo whatsapp. Mnaangaliana status tu no salam wala kutumiana video!! Watu kama hawa tuwa handle je mkuu?
 
Mimi harusi yangu ntafunga asubuhi jumuiyani ntamwita padri kwenye jumuiya itashereheshwa na wanajumiya na ndg wachache wa pande mbili. Jambo hilo nimeshamweleza ila anasema ati simpendi.!
Ukweli ni kwamba mimi nimechangia watu wengi sana ikafika mahali nikaacha.

Ukiniambia nifunge harusi ya ukumbini Mzee wangu hataudhuria (ninavyojua) sasa yanini ufanye Harusi uibue hoja za watu kukujadili kuhusu wazazi wako? Haina maana.
 
Mimi nilikuwa na sherehe ya harusi kipindi naoa kama ifuatavyo.
Baget =1000000(nilikuwa nayo)

Watu =50 mchanganuo uko Kama ifuatavyo
mchungaji na wasaidizi wake -5,
Majirani=10
Ndugu =20
Wakwe =10
Marafiki=5

Matumizi
Chakula =250000
Vinywaji=300000(bia zilikuwepo)
Mziki =150000
Mapambo =100000
Keki=50000
Mengineyo=150000
Mc (mshikaji wangu)

Watu walikula adi wakasaza bila kuchangia ata shilling moja ila walikuja na Zawadi za kutosha.

Mpaka nacomment hapa kuna shati nimevaa nilipewa kama Zawadi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…