Galacha Maestro
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 1,353
- 2,216
KABLA HUJAFUNGUA MDOMO WAKO , SHIRIKISHA AKILI YAKO
Kabla hujafungua mdomo wako, kwanza shirikisha akili yako.
Kufungua mdomo kabla ya kushirikisha akili ni chanzo kikubwa cha matatizo yako na watu wengine.
Kabla ya kufungua mdomo ni vizuri ukafikiri kwa kina, ili kile unachokwenda kuzungumza kiwe bora.
Baadhi ya maswali unayoweza kujiuliza kabla ya kufungua mdomo wako;
1. Je hiki ninachokwenda kusema ni muhimu?
2. Je kinaweza kumsaidia mtu ambaye atakisikia?
3. Je kina mchango chanya kwa kila atakayekisikia?
Kama majibu ni ndio kwenye maswali yote, basi unaweza kusema kitu hiko, na hakika kitakuwa msaada kwa wengine.
Ila kama utaongea tu bila ya kufikiri, utajikuta unaongea vitu ambavyo sio muhimu, au visivyo na msaada wowote kwa wengine na mbaya zaidi vinakuwa na mchango hasi.
Na pia unapoongea bila ya kufikiri utajikuta unaongea sana, na ukishakuwa muongeaji sana, jua wewe ndiye utakayepoteza. Wanaopata zaidi ni wale wanaosikiliza na kuangalia zaidi ya wanavyoongea.
Na kumbuka neno likishatoka kwenye mdomo wako huwezi kulirudisha tena. Ni vyema ukaongea kile ambacho unaweza kukisimamia.
Kabla hujafungua mdomo wako kuongea, shirikisha akili yako na hakikisha unaongea kitu chenye mchango mkubwa. Hii ni muhimu sana kwa kupata na kuendelea kuwa na mafanikio makubwA.