Bwana Banzi
JF-Expert Member
- Oct 14, 2014
- 464
- 251
Sawa kutu boyWakutu ni Kabila linalopatikana mpakani mwa mkoa wa Morogoro na Pwani. Kwa mkoa wa Morogoro wanapatilana katika wilaya ya morogoro ( Morogoro vijijini ) katika vijiji vya Dutumi, Mvua, kisaki, Ngerengere, Matuli, Kidunda, Kiwege, Lilongwe,Kongwa, Magogoni, Kilengwe, Kwaba n.k. Katika mkoa wa Pwani wanapatikana katika wilaya ya kibaha( magindu, Dutumi ya kibaha, Chaduma, kisangire na baadhi ya maeneo ya wilaya ya kisarawe na chalinze. Ni Kabila kubwa ila nadra kukutana na watu wa Kabila hili la kikutu, Wakutu wengi wanakopatikana maeneo ya mkoa wa Pwani hujitambulisha kama Wazaramo au wakwere. Na wengine hujitambulisha kama waluguru, hivyo sio rahisi kukutana na mtu wa Kabila la kikutu, japo kuwa ni Kabila kubwa mojawapo kwa mkoa wa Morogoro na Pwani.
Maana ya Kabila la WAKUTU:
Neno Wakutu limetokana na neno la Kiluguru ( wakutuka ), maana yake waluguru waliodondoka au wanaoishi mabondeni. Neno wakutuka ndio limezaa Kabila la Wakutu. Wale wa mlimani ( waluguru ) waliendelea kujiita waluguru na wale wenzao ambao wanaoishi mabondeni waliendelea kuitwa Wakutu na ndugu zao wa mlimani, hiyo ndo chanzo cha Kabila la Wakutu, na mwisho wa siku wakajitenga na kuwa makabila mawili tofauti makubwa.
Zifuatazo ni baadhi ya koo katika Kabila la Wakutu:
1. Wanyange; mwanaume nyanga mwanamke mlanyanga ( kwa waluguru mara chache hutumia nyanga na mlanyanga, waluguru hutumia mkude,au kunga'aro na mwanamke huitwa mwenda )
2. Wanyange; mwanaume huitwa nyange, mwanamke mlanyange.
3. Wa mlali; mwanaume huitwa mlali na mwanamke huitwa mlamlali ( kwa waluguru; mwanaume bwakila , mwanamke mlali au mlamlali).
4. Wabena; mwaume mbena, mwanamke mlambena.
5. Wakiraru; mwanaume kiraru, mwanamke mlakiraru.
6. Wahafigwa; mwanaume mhafigwa, mwanamke mlahafigwa.
7. Mponda; mwanaume mponda, mwanamke mlamponda.
8. Zongo; mwanaume zongo, mwanamke mlazongo.
9. Wa mindu; mwanaume semindu, mwanamke mindu.
10. Wa mng'ango; mwanaume mng'ango, mwanamke mlamng'ango.
11. Wakali; mwanaume mlali, mwanamke mlamlali.
12. Wa chuma; mwanaume chuma, mwanamke mlachuma ( kwa waluguru; mwanaume mponda, mwanamke chuma).
13. Wa kwambe; mwanaume mkwambe, mwanamke mlamkwambe.
14. Wa tebe; mwanamke mlatebe, mwanaume tebe.
15. Wasagara; mwanaume sagara, mwanamke mlasagara.
16. Wahimbwa; mwanaume dihimbwa, mwanamke mladihimbwa.
17. Wa chogeza; mwanaume chogeza, mwanamke mlachogeza.
18. Wakiluwa; mwanaume kiluwa mwanamke mlakiluwa.
19. Wakongela; mwanaume kongela, mwanamke mlakongela.
20. Watonga; mwanaume mtonga, mwanamke mlamtonga.
21. Wa chili; mwanaume mchilo,mwanamke mlamchilo
22. Wa mbali; mwanaume m'bwali, mwanamke mlam'bwali.
Hizo ni baadhi ya koo za Kabila la Wakutu, utaona kwa asilimia zaidi ya tisini zinafanana na koo za waluguru au wazaramo au wakwere.
Lugha ya Wakutu;
Baadhi ya maneno ya kikutu, mfano; aulamke (umeamkaje)? Unajibu anoga ( vizuri), imanye gwegwe ( sijui wewe). Ausindile ( ushindaje)?, Ukae ( nyumbani), ukae kutali ( nyumbani mbali). Kwa ufupi lugha ya kikutu ni sawa na lugha ya kizaramo, kikwere au Kiluguru .
Ngoma za asili za Kabila la Wakutu ni Vanga, mdundiko, n.k. Hayo ni machache yanayohusu Kabila Wakutu, wenyeji wa mkoa wa Morogoro na manispaa ya Morogoro.
Umewahi kuwasikia wamweraNaenda kuzeeka lakini sijawahi kulisikia hili kabila.
Shukrani sana mleta kutujuza.
Yah Wamwera hata nina jamaa zangu wametokana na hii jamii.Umewahi kuwasikia wamwera
Itakuwa kabila jipya townYah Wamwera hata nina jamaa zangu wametokana na hii jamii.
Hao wakutu nimepotea kabisa sijawahi kuwasikia toka nimepata ufahamu hata sikumbuki kuwasoma shule.
Kabisa mkuuTanzania kubwa mno
Hahaha sio Kabila jipya, jamii ya waluguru au wazaramo ndio maana ukiwaona utajua wazaramo,Itakuwa kabila jipya town
Nchi kubwa hii, ni wenyeji wa Morogoro. Ila mara nyingi hujitambulisha waluguru au wazaramo ili mambo yasiwe mengi. Na ni waluguru wa bondeni ila wamesajiliwa kama Kabila tofautiYah Wamwera hata nina jamaa zangu wametokana na hii jamii.
Hao wakutu nimepotea kabisa sijawahi kuwasikia toka nimepata ufahamu hata sikumbuki kuwasoma shule.
Safi, basi kikutu hicho au Kiluguru au kizaramo au kikwere, yote sawa. Yote ni majibuAusindile..... Anoga kuna wimbo hii salamu ilitumikaga.
Asante sanaWakutu ni Kabila linalopatikana mpakani mwa mkoa wa Morogoro na Pwani. Kwa mkoa wa Morogoro wanapatilana katika wilaya ya morogoro ( Morogoro vijijini ) katika vijiji vya Dutumi, Mvua, kisaki, Ngerengere, Matuli, Kidunda, Kiwege, Lilongwe,Kongwa, Magogoni, Kilengwe, Kwaba n.k.
Katika mkoa wa Pwani wanapatikana katika wilaya ya kibaha( magindu, Dutumi ya kibaha, Chaduma, kisangire na baadhi ya maeneo ya wilaya ya kisarawe na chalinze. Ni Kabila kubwa ila nadra kukutana na watu wa Kabila hili la kikutu, Wakutu wengi wanakopatikana maeneo ya mkoa wa Pwani hujitambulisha kama Wazaramo au wakwere. Na wengine hujitambulisha kama waluguru, hivyo sio rahisi kukutana na mtu wa Kabila la kikutu, japo kuwa ni Kabila kubwa mojawapo kwa mkoa wa Morogoro na Pwani.
Maana ya Kabila la WAKUTU:
Neno Wakutu limetokana na neno la Kiluguru ( wakutuka ), maana yake waluguru waliodondoka au wanaoishi mabondeni. Neno wakutuka ndio limezaa Kabila la Wakutu. Wale wa mlimani ( waluguru ) waliendelea kujiita waluguru na wale wenzao ambao wanaoishi mabondeni waliendelea kuitwa Wakutu na ndugu zao wa mlimani, hiyo ndo chanzo cha Kabila la Wakutu, na mwisho wa siku wakajitenga na kuwa makabila mawili tofauti makubwa.
Zifuatazo ni baadhi ya koo katika Kabila la Wakutu:
1. Wanyange; mwanaume nyanga mwanamke mlanyanga ( kwa waluguru mara chache hutumia nyanga na mlanyanga, waluguru hutumia mkude,au kunga'aro na mwanamke huitwa mwenda )
2. Wanyange; mwanaume huitwa nyange, mwanamke mlanyange.
3. Wa mlali; mwanaume huitwa mlali na mwanamke huitwa mlamlali ( kwa waluguru; mwanaume bwakila , mwanamke mlali au mlamlali).
4. Wabena; mwaume mbena, mwanamke mlambena.
5. Wakiraru; mwanaume kiraru, mwanamke mlakiraru.
6. Wahafigwa; mwanaume mhafigwa, mwanamke mlahafigwa.
7. Mponda; mwanaume mponda, mwanamke mlamponda.
8. Zongo; mwanaume zongo, mwanamke mlazongo.
9. Wa mindu; mwanaume semindu, mwanamke mindu.
10. Wa mng'ango; mwanaume mng'ango, mwanamke mlamng'ango.
11. Wakali; mwanaume mlali, mwanamke mlamlali.
12. Wa chuma; mwanaume chuma, mwanamke mlachuma ( kwa waluguru; mwanaume mponda, mwanamke chuma).
13. Wa kwambe; mwanaume mkwambe, mwanamke mlamkwambe.
14. Wa tebe; mwanamke mlatebe, mwanaume tebe.
15. Wasagara; mwanaume sagara, mwanamke mlasagara.
16. Wahimbwa; mwanaume dihimbwa, mwanamke mladihimbwa.
17. Wa chogeza; mwanaume chogeza, mwanamke mlachogeza.
18. Wakiluwa; mwanaume kiluwa mwanamke mlakiluwa.
19. Wakongela; mwanaume kongela, mwanamke mlakongela.
20. Watonga; mwanaume mtonga, mwanamke mlamtonga.
21. Wa chili; mwanaume mchilo,mwanamke mlamchilo
22. Wa mbali; mwanaume m'bwali, mwanamke mlam'bwali.
Hizo ni baadhi ya koo za Kabila la Wakutu, utaona kwa asilimia zaidi ya tisini zinafanana na koo za waluguru au wazaramo au wakwere.
Lugha ya Wakutu;
Baadhi ya maneno ya kikutu, mfano; aulamke (umeamkaje)? Unajibu anoga ( vizuri), imanye gwegwe ( sijui wewe). Ausindile ( ushindaje)?, Ukae ( nyumbani), ukae kutali ( nyumbani mbali). Kwa ufupi lugha ya kikutu ni sawa na lugha ya kizaramo, kikwere au Kiluguru .
Ngoma za asili za Kabila la Wakutu ni Vanga, mdundiko, n.k. Hayo ni machache yanayohusu Kabila Wakutu, wenyeji wa mkoa wa Morogoro na manispaa ya Morogoro.
Tanzania Ina makabila mengi mnoWakutu ni Kabila linalopatikana mpakani mwa mkoa wa Morogoro na Pwani. Kwa mkoa wa Morogoro wanapatilana katika wilaya ya morogoro ( Morogoro vijijini ) katika vijiji vya Dutumi, Mvua, kisaki, Ngerengere, Matuli, Kidunda, Kiwege, Lilongwe,Kongwa, Magogoni, Kilengwe, Kwaba n.k.
Katika mkoa wa Pwani wanapatikana katika wilaya ya kibaha( magindu, Dutumi ya kibaha, Chaduma, kisangire na baadhi ya maeneo ya wilaya ya kisarawe na chalinze. Ni Kabila kubwa ila nadra kukutana na watu wa Kabila hili la kikutu, Wakutu wengi wanakopatikana maeneo ya mkoa wa Pwani hujitambulisha kama Wazaramo au wakwere. Na wengine hujitambulisha kama waluguru, hivyo sio rahisi kukutana na mtu wa Kabila la kikutu, japo kuwa ni Kabila kubwa mojawapo kwa mkoa wa Morogoro na Pwani.
Maana ya Kabila la WAKUTU:
Neno Wakutu limetokana na neno la Kiluguru ( wakutuka ), maana yake waluguru waliodondoka au wanaoishi mabondeni. Neno wakutuka ndio limezaa Kabila la Wakutu. Wale wa mlimani ( waluguru ) waliendelea kujiita waluguru na wale wenzao ambao wanaoishi mabondeni waliendelea kuitwa Wakutu na ndugu zao wa mlimani, hiyo ndo chanzo cha Kabila la Wakutu, na mwisho wa siku wakajitenga na kuwa makabila mawili tofauti makubwa.
Zifuatazo ni baadhi ya koo katika Kabila la Wakutu:
1. Wanyange; mwanaume nyanga mwanamke mlanyanga ( kwa waluguru mara chache hutumia nyanga na mlanyanga, waluguru hutumia mkude,au kunga'aro na mwanamke huitwa mwenda )
2. Wanyange; mwanaume huitwa nyange, mwanamke mlanyange.
3. Wa mlali; mwanaume huitwa mlali na mwanamke huitwa mlamlali ( kwa waluguru; mwanaume bwakila , mwanamke mlali au mlamlali).
4. Wabena; mwaume mbena, mwanamke mlambena.
5. Wakiraru; mwanaume kiraru, mwanamke mlakiraru.
6. Wahafigwa; mwanaume mhafigwa, mwanamke mlahafigwa.
7. Mponda; mwanaume mponda, mwanamke mlamponda.
8. Zongo; mwanaume zongo, mwanamke mlazongo.
9. Wa mindu; mwanaume semindu, mwanamke mindu.
10. Wa mng'ango; mwanaume mng'ango, mwanamke mlamng'ango.
11. Wakali; mwanaume mlali, mwanamke mlamlali.
12. Wa chuma; mwanaume chuma, mwanamke mlachuma ( kwa waluguru; mwanaume mponda, mwanamke chuma).
13. Wa kwambe; mwanaume mkwambe, mwanamke mlamkwambe.
14. Wa tebe; mwanamke mlatebe, mwanaume tebe.
15. Wasagara; mwanaume sagara, mwanamke mlasagara.
16. Wahimbwa; mwanaume dihimbwa, mwanamke mladihimbwa.
17. Wa chogeza; mwanaume chogeza, mwanamke mlachogeza.
18. Wakiluwa; mwanaume kiluwa mwanamke mlakiluwa.
19. Wakongela; mwanaume kongela, mwanamke mlakongela.
20. Watonga; mwanaume mtonga, mwanamke mlamtonga.
21. Wa chili; mwanaume mchilo,mwanamke mlamchilo
22. Wa mbali; mwanaume m'bwali, mwanamke mlam'bwali.
Hizo ni baadhi ya koo za Kabila la Wakutu, utaona kwa asilimia zaidi ya tisini zinafanana na koo za waluguru au wazaramo au wakwere.
Lugha ya Wakutu;
Baadhi ya maneno ya kikutu, mfano; aulamke (umeamkaje)? Unajibu anoga ( vizuri), imanye gwegwe ( sijui wewe). Ausindile ( ushindaje)?, Ukae ( nyumbani), ukae kutali ( nyumbani mbali). Kwa ufupi lugha ya kikutu ni sawa na lugha ya kizaramo, kikwere au Kiluguru .
Ngoma za asili za Kabila la Wakutu ni Vanga, mdundiko, n.k. Hayo ni machache yanayohusu Kabila Wakutu, wenyeji wa mkoa wa Morogoro na manispaa ya Morogoro.
Kabisa, Wakutu ni Kabila kubwa mojawapo Morogoro na PwaniDah!
Tanzania Ina makabila mengi mno