KISHINDO
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 2,202
- 1,957
Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bw. Frank Kanyusi ameivunja Bodi ya Wadhamini ya Kanisa la Wadiventista Wasabato Tanzania kufuatia ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG kubaini Bodi hiyo kushindwa kusimamia ipasavyo mali na majukumu yake na hivyo kutoa siku saba kwa uongozi wa kanisa hilo kuwasilisha majina kumi (10) ya waumini watakaopendekezwa kuwa wajumbe wapya wa kamati ya mpito itakayosimamia mali za kanisa hilo hadi itakapopatikana Bodi mpya ya Wadhamini.
Bw. Kanyusi ametoa agizo hilo hii leo Februari 24, 2026 Jijini Dar es salaam wakati wa kupokea ripoti ya ukaguzi maalum wa kiuchunguzi wa mali za Kanisa la Waadiventista Wasabato Tanzania uliofanywa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG kufuatia malalamiko yalivyowasilishwa na baadhi ya waumini wa kanisa hilo katika ofisi ya kabidhi Wasii Mkuu na Msajili wa Jumuiya za Kiraia Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi wakilalamika kuwepo kwa ubadhirifu wa mali za kanisa na matumizi mabaya ya madaraka.
Bw. Kanyusi amebainisha kuwa, taarifa hiyo ni hatua muhimu iliyochukuliwa kwa kushirikiana na Msajili wa Jumuiya za Kiraia Bw. Emmanuel Kihampa kutoka wizara ya mambo ya ndani kuamua kufanyika kwa ukaguzi maalum wa kiuchunguzi ili kujiridhisha na usahihi na ukweli wa malalamiko yaliyowasilishwa na waumini wa kanisa hilo.
Bw Kanyusi ameongeza kuwa, taarifa hiyo itafanyiwa kazi kwa haraka na kuwasilishwa kwa vyombo vingine vya kiuchunguzi ili wale wote waliobainika katika taarifa ya CAG kuhusika na ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka na mali za taasisi hiyo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake Msajili wa Jumuiya za Kiraia Bw. Emmanuel Kihampa amesema kuwa ofisi yake ilipokea malalamiko kuhusu viongozi wa kanisa hilo kutowajibika katika kusimamia majukumu yao hivyo kuwasiliana na Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu ili kuchukua hatua za haraka kwa upande wa wajumbe wa bodi za wadhamini na viongozi watendaji wa Kanisa la Waadiventista Wasabato Tanzania.