Kaberuka: Africa's needed pressure lies not on its oil, gas, even its minerals...

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,883
2,763
but its youths. its demographic dynamic. In Southern Asia between 1970's and 2000 much of the economic growth was driven by the same demographic dynamic.

Hayo ni maneno ya Rais wa Benki ya Afrika. Vijana ndio gurudumu la maendeleo. Hata pakiwepo rasilimali zingine, kama rasilimali watu (vijana) haitumiki ni kazi bure.


Jana akifungua mkutano wa mwaka wa Magavana wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Jijini Arusha, Rais Kikwete alisema moja ya sababu kuu ya machafuko yanayoshuhudiwa sasa kwenye ukanda wa nchi za Kiarabu, ni matokeo ya ukosefu wa ajira kwa vijana na watu kukata tamaa.

“Siyo kweli kwamba machafuko yanayoshuhudiwa kwenye nchi za Kiarabu ni matokeo ya Serikali za nchi hizo kukaa madarakani kwa kipindi kirefu kama wengi wanavyodhani. Ukweli ni kwamba hayo ni matokeo ya ukosefu wa ajira na watu kukata tamaa ya maisha,” alisema Rais Kikwete.

Alisema bila kutafutia ufumbuzi wa haraka, tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana ambao wengi hukimbilia mijini kusaka hali bora ya maisha, hata nchi zenye kuongozwa kidemokrasia, zinaweza kukumbwa na machafuko na uasi wa umma.

Rais alitumia fursa hiyo kuishukuru Denmark kwa kutoa fedha za kusaidia Mfuko wa Ajira kwa Vijana barani Afika, akisema ni moja ya mapendekezo kadhaa yaliyotolewa na kamati maalum ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya kiuchumi barani Afrika ambayo yeye na Rais wa AfDB, Dk Donald Kaberuka, walikuwa wajumbe.

Mapema Rais wa Ivory Coast, Allasane Ouattara aliyehudhuria mkutano huo aliunga mkono kauli hiyo ya Rais Kikwete kwa kusisitiza kuwa vijana lazima wawekewe mazingira mazuri na kuwezeshwa kukabiliana na kumudu changamoto za kiuchumi, kitamaduni na kiteknolojia wanazokabiliana nazo.

“Lazima wasaidiwe na wawekewe mazingira bora ya kupata fursa za ajira na kujiajiri, bila kufanya hivyo ni kukaribisha matatizo na machafuko yanayotokana na ongezeko la mahitaji na kukata tamaa katika miji yetu inayokua kila kukicha kutokana na ongezeko la vijana wanaosaka ajira na maisha bora,” alisema Rais Ouattara.

Rais Ouattara aliyetumia muda mwingi kumshukuru Rais Kikwete na viongozi wenzake wa Kiafrika kwa kusaidia upatikanaji wa amani nchini mwake alitaja changamoto kadhaa zinazokabili Bara la Afrika, kuwa ni mabadiliko ya tabia nchi, ukame, uhaba wa chakula na ukosefu wa amani kwa baadhi ya sehemu.

Mambo mtambuka
Ili kukabiliana na tatizo hilo, Rais Kikwete alitaja mambo kadhaa yanayopaswa kufanyika ikiwa ni pamoja na kukuza na kuboresha sekta ya kilimo kwa kuongeza uwekezaji na kuacha kutegemea kilimo cha mvua badala yake itumie fursa ya vyanzo vingi vya maji.

“Bara la Afrika linaweza kuzalisha mazao ya kilimo na kujitosheleza kwa chakula na kubakisha ziada ya kuuza nje hadi kuwa ghala la chakula duniani iwapo uwekezaji katika sekta ya kilimo utapewa kipaumbele,” alisema Rais Kikwete.

Kuhusu miundombinu, Rais Kikwete aliipa changamoto AfDB kuongeza juhudi katika ufadhili na udhamini wa miradi ya maendeleo barani Afrika, ikiwemo miradi ya miundombinu aliyosema ni moja ya changamoto zinazokwaza maendeleo ya Afrika.

Hayo aliyosema Kikwete yalikuwa na utangulizi wake toka kwa Gavana kaberuka. Hadi wachumi na wataalam toka nje waseme ndipo viongozi wetu wakubali? Alisema pia kuwa elimu ikiboreshwa, afya, na miundombinu, ni wazi kuwa mambo yataboreka.
 
Back
Top Bottom