Kaa mbali na plan B ya mwanamke

Kaa mbali na plan B ya mwanamke

seyayi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
683
Reaction score
821
Habari za muda huu wanajamvi.Poleni na hongereni kwa mihangaiko ya hapa na pale katika kulijenga Taifa letu pendwa.

Naomba niende moja kwa moja kwenye mada husika.Jamani eee,kumekuwa na vilio humu kila uchwao juu ya wanaume kutendwa,kusalitiwa na wenzi wao katika hatua ya uchumba ame ndoa kabisa.
Malalamiko mengi yanayoletwa humu ni juu ya ma "x" wa wake zao kwamba wao ndio wamekuwa chanzo cha migogoro ama kuvunjika kwa ndoa.Swali,inakuaje na kwanini huyu "x" apewe nafasi tena kuuteka moyo wa mke wako ilihali walishaachana miaka,sita,saba mpaka kumi iliyopita?,tena kwa mke ambaye umezaa nae watoto?

Katika fikra zangu binafsi nilicho baini ni kwamba wanaume wengi hujikuta wakiangukia katika "plan b za wanawake".

Kwa kawaida mwanamke hupenda mala moja tu,narudia tena mala moja tu,sasa inapotokea yule mtu aliyemkabidhi moyo wake,maisha yake,mwili wake akamuumiza na kumsaliti,hapo ndipo mwanamke hufikiria plan b ambayo ni kumkubali mtu mwingine ambaye aliwahi kumtaka akamsumbua sana kwa miezi kadhaa hata miaka bila mafanikio.

Bhagosha mpooo?nauliza mpooo?.Sasa sikia hii,"hakuna kazi ngumu kama kuurejesha moyo wa mwanamke aliyeumizwa katika ukawaida wake",kama hujui kucare,kubembeleza,kusamehe kaa mbali nae.

Kwa kawaida mwanamke humithilisha mahusiano yake ya kwanza na yale ya plan b yake na huwa hawafichi hisia zao na ndio maana hawasiti kukwambia huniridhishi,hunifanyi vizuri,sifiki mwisho nk.HII YOTE NI KWA SABABU WEWE NI PLAN B yake,maneno haya hawezi kuyatamka kwa mtu wake wa kwanza.

Hitimisho:Vijana tafuteni wanawake wenu acheni kuingilia mahusiano ya watu,acha kubeba mke wa mtu karma never forgets!
 
Kuliko kuwa plan b ya mwanamke ni bora mwanaume awe na plan b.
 
Mahusiano hayana Formula....
Muhenga mmoja alinambia.
 
mkuu unaumiza kichwa kwa mambo yasiyo na suluhu??
now hata uoe bikra utachapiwa tu....
tumuombeni tu mungu atupe wepesi coz hakuna njia yakuepuka huu msala
 
Mleta mada uko sahihi 100%, mimi limenikuta baada ya kuishi maisha ya mwanzo kuwa na mwenza yule binti nilizaa nae ila kwa kweli tulipendana sana, ila mpaka leo sifahamu hasa kwa nini tuliachana, ila ndugu zake walichangia kiasi kikubwa utengano wetu, hasa ukizingatia ule umri tuliokua nao..,
Anyway, alikuja kuishi na jamaa mwingine ili anikomoe au aniumize roho, sijui.
Nafikiri ndio hiyo plan B, unayozungumzia.kwa kweli alianza kunifuatilia huku akiwa anaishi na jamaa mwingine, na wakikorofishana nasikia huwa anamwambia jamaa usinitishe wala kunibabaisha, baba watoto wangu yupo saa yoyote ninaweza kwenda na akanipokea.
Ila hata hivyo, daaaah..!! Ni kweli muda wowote nimwita anakuja kwa kasi ya dramliner..[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Sasa wakati unatongoza utajuaje wewe ni plan B?

Nafikiri tuishini tu hivi hivi......
 
Mleta mada uko sahihi 100%, mimi limenikuta baada ya kuishi maisha ya mwanzo kuwa na mwenza yule binti nilizaa nae ila kwa kweli tulipendana sana, ila mpaka leo sifahamu hasa kwa nini tuliachana, ila ndugu zake walichangia kiasi kikubwa utengano wetu, hasa ukizingatia ule umri tuliokua nao..,
Anyway, alikuja kuishi na jamaa mwingine ili anikomoe au aniumize roho, sijui.
Nafikiri ndio hiyo plan B, unayozungumzia.kwa kweli alianza kunifuatilia huku akiwa anaishi na jamaa mwingine, na wakikorofishana nasikia huwa anamwambia jamaa usinitishe wala kunibabaisha, baba watoto wangu yupo saa yoyote ninaweza kwenda na akanipokea.
Ila hata hivyo, daaaah..!! Ni kweli muda wowote nimwita anakuja kwa kasi ya dramliner..[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hawezi kukusahau amebeba nafsi yako
 
Mambo mengine ni ya kuachwa Kama yalivyo.
 
Mkuu bora uhai tu ago mengine mtaumiza vichwa vyenu bure....
Tangu nilipogundua neumbwa mwanaume nikasema yatosha. Niwe Plan B au hata C sijali. Mimi ni kiongozi na sijali namwongoza nani, ukikubali kuongozwa twende, ukigoma nenda. Siwezi kuhangaika na kiumbe kisa mapenzi, najali watoto wangu, the lest will feed itself.
 
Sio kweli kwamba mwanamke hupenda mara Moja..nakataa
 
Tangu nilipogundua neumbwa mwanaume nikasema yatosha. Niwe Plan B au hata C sijali. Mimi ni kiongozi na sijali namwongoza nani, ukikubali kuongozwa twende, ukigoma nenda. Siwezi kuhangaika na kiumbe kisa mapenzi, najali watoto wangu, the lest will feed itself.
[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Hakuna cha Plan B wala nn, ni wanaume tu tumekuwa penda penda. Kujiliza Liza sababu ya mapenzi. Miaka ya mbele tutaanza kupewa sisi talaka.
 
Back
Top Bottom