waziri2020
Senior Member
- May 31, 2019
- 198
- 470
Utapeli unaotishia Mustakabali wa wafanyabiashara katika Jiji la Arusha unazidi kushika kasi kwa matapeli kutumia vivuli Vya Idara nyeti ya Usalama wa taifa kuzidi kuwaliza mamilioni ya fedha watu mbalimbali .
Hivi karibuni kikundi cha watu wapatao wanne kikiongozwa na vinara wa mtandao huo ,Peter Kichonge na aliyekuwa mwandishi wa habari gazeti la Mwananchi, Mosses Mashalla(Ngosha)kimeibuka jijini Arusha na kuwa moto wa kuotea mbali kwa wafanyabiashara kulizwa kila kukicha huku waathiriwa hao wakijawa na hofu ya kutoa taarifa Polisi.
Kikundi hicho kinaushirika mkubwa na mwajiriwa wa serikali Idara nyeti ya Usalama wa taifa makao makuu ,kuwaliza wafanyabiashara wenye maduka makubwa ,wafanyabiashara Madini ,wenye viwanda na RAIA wa kigeni ambao wengi wao hukutwa na matatizo ya uraia.
Hivi karibuni umoja wa vijana wa ccm(UVCCM)wilaya ya Arusha uliingilia kati na kukemea jambo hilo ikiwemo kuanika mtandao huo wa matapeli , lakini nguvu ya matapeli hao ilipelekea mwenyekiti wa umoja huo aliyetoa tamko la kuanika maovu ma majina ya matapeli hayo kuishia kuhamishwa kituo chake cha kazi jambo lililosikitisha watu wengi.
Wengine waliotajwa na UVCCM kuhusika na mtandao huo wa uhalifu wa utapeli ni pamoja na Jimmy Wasira,Bryton Mushi (mkwe wa Askofu Issangya) na Cossen Frey.
Baadhi ya wafanyabiashara walioumizwa na mtandao huo akiwemo mfanyabiashara maarufu wa Hardware jijini Arusha jina( limehifadhiwa)alikamatwa matapeli hao wakidai wanampeleke makao makuu Dodoma kutokana na makosa yanayomkabili badala yake walimtelekeza porini baada ya kukubali kutoa kitita cha fedha walichokuwa wakihitaji.
Matapeli hao wanatumia mbinu ya kuwachongea kwenye mamlaka husika baadhi ya wafanyabiashara wanaokataa kutoa ushirikiano wa fedha na baadhi ya wafanyabiashara wamejikuta wakikamatwa na kulazwa mahabusu kwa kudhaniwa ni wahalifu wa kutorosha madini.
Afisa Usalama ambaye amekuwa akitumika kama chambo kuhalalisha maovu ya mtandao huo wa matapeli inadaiwa kuwa kikosi hicho cha matapeli pindi wafanyabiashara waathiriwa wanapolalamika huelezwa kuwa kikundi hicho husaidia kufichua watoroshaji wa Madini jambo ambalo limepelekea kutokamatika kirahisi.
Polisi mkoa wa Arusha RPC Jonathan Shanna alinukuliwa akisema tayari jeshi la polisi limepara taarifa za uwepo wa mtandao huo wa matapeli na kwa sasa wanakusanya taarifa kutoka kwa waathirika ili waweze kuzifanyia kazi na muda mfupi tutapata majibu.
Kamanda Alisema jamii inapaswa kutoa ushirikiano ili kufanikisha kukamatwa kwa watu hao ambao pia wamekuwa wakifanya uhalifu huo na kukimbilia mikoa ya Dar ,Tanga na Dodoma.
.