Ka modem ka tigo kamenishinda

kama hauna point na haulijua swali wala kitu kilichoulizwa ni bora ukale ulojo au hizo vocha kawasiliane na mpenzi wako.. shabashi
 
kwan lazma uchakachue hyo modem, ulinunua ya nn kama huwez kuilipia? watu wengine bwana, wamekalia ufisadi tuuuu....si lazma ukombe mabilioni BOT au uchukue rushwa au utoe ushinde uchaguzi, hata huo ni ufisadi na wizi! kama huna pesa ya kulipia gharama za modem itupe tu.
Acha ujinga kwani modem ni mali ya tigo, voda, Airtel....
 
kama hauna point na haulijua swali wala kitu kilichoulizwa ni bora ukale ulojo au hizo vocha kawasiliane na mpenzi wako.. shabashi

bora umwambie mchaga wangu maana watu wengine ni kama viatu au ndala za chooni zinatembelewa na kila mtu....
 
Finally,nimepata suluhisho kwa walioniponda nimewasamehe kwa walio niunga mkono tuko pamoja na ndo natumia ku post now kwa bomba7 sasa
 
nimeanza na voda na nimeshajiunga na bomba7 spidi nzuri ngoja nione ntaanza moja baada ya nyingine
 
Finally,nimepata suluhisho kwa walioniponda nimewasamehe kwa walio niunga mkono tuko pamoja na ndo natumia ku post now kwa bomba7 sasa

Good!..Ila ungetushirikisha ulikuwa unakosea wapi ili next time mtu akipata tatizo kama hili ajue pa kuanzia....Ila ukiona inakupa ERROR kuna vitu viwili, either imeshakuwa unlocked au iko counter blocked...hiyo ya kwako itakuwa ilishakuwa unlocked ndo maana ulipoweka kadi ya Airtel ilisoma
 
kwan lazma uchakachue hyo modem, ulinunua ya nn kama huwez kuilipia? watu wengine bwana, wamekalia ufisadi tuuuu....si lazma ukombe mabilioni BOT au uchukue rushwa au utoe ushinde uchaguzi, hata huo ni ufisadi na wizi! kama huna pesa ya kulipia gharama za modem itupe tu.

Nahisi kuna haja ya wewe bosi kujua umuhimu wa kuchakachua. Hudhuria somo lifuatalo:

UMUHIMU WA KUCHAKACHUA MODEM
Kwa nini tunachakachua modem?
1.Tunachakachua modem kwa sababu mudem hizi hazigawiwi bure. Kwa hiyo kama nimeinunua maana yake ni kuwa ni yangu na kwa hiyo siyo haki ya yeyote kunipagia nitumie mtandao gani.
2.Mitandao ya simu nchini bado inafanya kazi chini ya viwango vinavyomhakikishia mtumiaji(consumer) uhakika wa huduma. Mathalan imekuwa ni kawaida kwa nyakati tofauti ukakuta internet ya mtandao fulani imekuwa nzito ghafla au imekatika kienyeji wakati mtu anafanya kazi ya muhimu sana.
3.Gharama za huduma bado ni za ki-wizi zaidi.Siyo ajabu ukinunua bundle sasa hivi kutoka kwenye mtandao wowote na mara huduma ikakatishwa bila maelezo wala kujali unafanya nini!Au sishangai kabisa pale inapotokea kwamba umelipia bundle na ghafla kila senti iliyokuwa kwenye modem au simu imetawanyikia kusikojulikana!Au hujawahi kujua kuwa hapa hapa nchini hususan Dar kuna sehemu Sasatel haifiki,au Tigo haitoi huduma ya net?Wala hujawahi kusikia kuwa huko mioani siyo makampuni yote yanayotoa huduma za internet?Sorry am I missing something?hivi wewe ni mTZ uliye hapahapa kweli? Au hujawahi kuona hii sh 1/s inavyokuwa ya ajabu siku nyingine?Sishangai kwamba kuna wewe pamoja na wenzio ambao hamjaona hilo aither kwa sababu fedha mnazotumia hamzitolei jasho kabisa au kwakuwa hata hizo modem hamjawahi kununua kwa sababu kuna internet ofisini! Huu nao ni ujinga. Na ni ujinga wa aina hii hii ndiyo unaoleta umaskini hapa Tanzania! Labda hunielewi; Vyovyote inavyokuwa kwa possibility zote wewe huwi muadilifu. Hebu cheki hizi possibility hapa chini;

Say wewe una fedha nyingi ambazo hazikuumi kwa kuwa hujazitolea jasho.Ukweli utabaki kuwa wewe ni some kind of watu wasiotakiwa na jamii hii ya watanzania ambao asilimia kubwa ni maskini haswa pale inapokuja kuwa watumiaji wengi wa modems ni wanavyuo ambao wengi wanategemea mikopo ambayo pamoja na kutofuata vigezo wakati wa kukopeshwa bado taratibu nyingi zimekiukwa na haki hazitendeki. Unaonaje wewe hivi ulifikiria vya kutosha?
Tuseme unatumia internet ya ofisi. Hii nayo inakufanya uwe binadamu wa ajabu tu. Unajua kwa nini? kwa sababu huyo mwajiri wako aliweka internet ofisini kuhakikisha mawasiliano ya ofisi yake na siyo kukurahisishia wewe kuchat ku google na kuangalia pono. So ni vizuri pia ukaanza kuangalia uwezekano wa kujiweka kwenye makundi ya Kichawi zaidi hasa pale ambapo kwa makusudi au kutojua unachangia kumrudisha nyuma mwajiri wako.(mchawi siyo lazima aruke na ungo!!!)

Kwa haraka nasema KUCHAKACHUA HAKUMAANISHI KUTOLIPIA MODEMS,La hasha! Kunamaanisha mtu kutumia modems yake aliyoinunua kwa jasho lake hata kama amehamia mikoani!Kunamaanisha kujipatia internet wakati wote kwa bei nafuu.To me This is Freedom! Huenda wewe unapenda vitu expensive...may be hii nchi haikufai.Jaribu France.

Vinginevyo hautaelewa hili mpaka uanze kutumia huduma za muhimu kwa gharama zako na siyo kuhongwa au kuiba au kupewa.Nafikiri ulisahau kufikiria mambo ya msingi kabla ya kujibu thread. Wala siyo lazima wote tujibu. Sometimes unaweza kuangalia na kusoma maoni na majibu ya wengine tu.

Kwa ufupi huu ndiyo umuhimu ,vyanzo na sababu za kuchakachua modems. Asante kwa kusoma kwa makini na karibu kwenye darasa jingine. SIKU NJEMA!

............no offense!


 
Back
Top Bottom