JWTZ yawapiga wananchi Ngara!

JWTZ yawapiga wananchi Ngara!

mjsimon

Member
Joined
May 11, 2009
Posts
5
Reaction score
1
JWTZ yafanya kufuru Ngara.

Wanajeshi wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika wilaya ya Ngara, kata ya Mrusagamba wamewapiga vibaya wananchi 17 wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kwa madai kuwa wamekata bomba ya maji yanayopeleka maji Jeshini.

Kipigo hicho kimewakumba wananchi wa vitongoji vya Nyawela na Runyago ambao wako karibu na eneo ambalo bomba hilo limekatwa. Viongozi wa CCM kata ya Mrusagamba walipeleka majina ya wanachama wa Chadema na Viongozi wa kata hiyo kwa maafisa wa jeshi holo na bila uchunguzi wowote wananchi hao walianza kupewa mkongoto ambapo baada ya taarifa kufikia DAS, aliwapigia simu nao kusitisha kipigo na kuwabeba mzobemzobe hadi kituo cha polisi Mrusagamba ambako walifunguliwa mashtaka na kuzuiwa dhamana.

Jana Jumatatu jioni, walisafirishwa mpaka kituo cha polisi Benako ambako waliachwa hapo wala hawakufikishwa kituo kikuu cha polisi Ngara mjini. Pia dhamana zao zimezuiliwa.
Swali: Je bomba moja laweza kukatwa na watu 17? Je Tanzania inaweza kuendeshwa kwa mabavu kiasi hiki? :angry:

Maoni: Vurugu nchi hii zitaletwa na CCM

Ewe mwananchi chukua hatua kulinda amani ya nchi hii.
 
Waundieni zenngwe hao waliowaletea fitna...

"Dawa ya moto ni moto, yaani mtu akiwasha moto upande huu wewe kawashe upande mwingine wa pili. Mioto hii ikikutana katikati ni lazima izime."

Usemi huo alipenda sana kuutumia Albert Msando akiwa shule...
 
Last edited by a moderator:
Hivi ninyi mnakaatia mabomba wanajeshi, hamjui kuwa akili zao hawa jamaa ziko kwenye mabuti yao??
 
Hao wanaweza kuwa jamii kutoka nchi jirani tunaoishi nao hapa. Hata hivyo CDM kwa tabia wanafanana nao. Wamekiona walichokitaka, waandamne waone! Waichezee Serikali walivyozoea lakini siyo JWTZ. Nadhani huo ni mwanzo tu kubwa itaguatia. Huku kwetu hatutaki unafiki wala kuiikweza. Wana CDM wanatafuta umaarufu wa kupigwa. Chezea JTWZ wewe!
 
Mimi bado sijaelewa maana ya hii habari, kwani CHADEMA wana mradi wa maji huko Ngara? Na wakate kwa madhumuni gani? CCM ina uhakika gani kuwa hao ndio waliokata hayo maji? Jeshi pamoja na Intelijensi yake imeshitwa hata kufanya utafiti na kwenda kutoa kipigo kwa hao vijana 17? Mimi sidhani kama kuna ukweli hapa.
 
Mimi sidhani kama kuna ukweli hapa.

Nadhani hujawahi kushuhudia JWTZ au JKT wakitoa mkong'oto kwa raia wewe...

Kama kuna mkazi yoyote wa Duka Bovu kule Arusha wa miaka hiyo anaweza kukueleza walichofanywa na mandata wa TMA...
 
Mimi ninajua askari wanakiapo cha utii. Utii wa askari wote umegundishwa kwenye utashi wa mwajiri wake ambaye ni serikali. Serikali ikiamuru vita ama operation fulani, askari hatakiwi kuhoji, wajibu wake ni kutii. Serikali ikiacha suala la nidhamu jeshini kwamba si suala la lazima, askari atabehave vile.

Pamoja na maisha ya askari kuwa mikononi mwa mwajiri kuliko idara zote, bado hawa ni binadamu wana utashi, dhamira na hisia. Sihitaji kusema mengi lakini tumeona serikali nyingi zimetumia askari kinyume na raia na zimefanikiwa sana kwa kuua na kutishia. Lakini kwa kuwa askari hawa ni watu, mara zote huishia kuasi mmoja mmoja. Wanavua kombati, wanatupa ama kuondoka na silaha, anakwenda kujiunga na ndugu zake. Askari hawa wanafahamu kabisa wanapoua ama kunyanyasa raia, wanakumbukaga ndugu zao raia ambao nao wananyanyaswa ama kuuliwa na askari wengine sehemu zingine kama ndio mfumo wa watawala.

Hakuna askari atakayeendelea kuwa royal kwa majilir wakati mwajiri huyo anaua wadogo zake, wazazi wake, wajomba, shangazi dada n.k. Watanzania, ni suala la muda tu. Mbinu ya ccm kuwatumia askari kinyume na ndugu zao, wananchi wenzao, haina muda mrefu mtaniambia. Hawapendi ila wanalazimika kutii lakini kwa kuwa wana mioyo, kunasiku nguvu ya dhamira na hisia itashinda nguvu ya kiapo cha utii. Na hapo mtaona. ccm wakiliona hil mapema, hawatacheza na askari.
 
Mimi ni mwandishi wa blog maarufu ya wahangaza blog ya wilayani ngara nimefatilia habari hii baada ya kuiona humu maana nipo ngara kwa sasa tena kwa kutumia reporter wangu aliyepo mrusagamba majibu ni kwamba habari hii sio ya kweli ns hakuna kitu kama hicho kilichotendeka wilayani ngara. Naomba jamii forum tulinde taaluma ya utoaji habari
 
Askari hawatakiwi kuchukua sheria mkononi..ila ndio hivyo tena...na kwanini watu wakate bomba la maji? Siasa gani hizo?Ndio zile za maji taka?
 
Zaidi habari hii ingekuwa sahihi endapo ingetolewa kwamba mabomba yamekatwa na watu kupigwa lkn sio kuhusisha vyama vya siasa. Ni kweli bomba zimekatwa na vijana ila sio chadema wa ccm haijurikani ni chama gani. Uchochezi haufai tutoe habari kama zilivyo
 
juzi nimeandika uzi kukemea ubabe wa wanajeshi watu wanawatetea. unaona wanaanzza kutumika na wanasiasa. jeshi likikosa nidhamu huwa dhaifu.
 
Wanajamii jeshi halijapiga mtu zaidi ya vijana kukamatwa na sio wa chadema kama alipost habari anavyodai . amelipaka matope jeshi ni bora arudi afute kauli
 
JWTZ yafanya kufuru Ngara.

Wanajeshi wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika wilaya ya Ngara, kata ya Mrusagamba wamewapiga vibaya wananchi 17 wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kwa madai kuwa wamekata bomba ya maji yanayopeleka maji Jeshini.

Kipigo hicho kimewakumba wananchi wa vitongoji vya Nyawela na Runyago ambao wako karibu na eneo ambalo bomba hilo limekatwa. Viongozi wa CCM kata ya Mrusagamba walipeleka majina ya wanachama wa Chadema na Viongozi wa kata hiyo kwa maafisa wa jeshi holo na bila uchunguzi wowote wananchi hao walianza kupewa mkongoto ambapo baada ya taarifa kufikia DAS, aliwapigia simu nao kusitisha kipigo na kuwabeba mzobemzobe hadi kituo cha polisi Mrusagamba ambako walifunguliwa mashtaka na kuzuiwa dhamana.

Jana Jumatatu jioni, walisafirishwa mpaka kituo cha polisi Benako ambako waliachwa hapo wala hawakufikishwa kituo kikuu cha polisi Ngara mjini. Pia dhamana zao zimezuiliwa.

Swali: Je bomba moja laweza kukatwa na watu 17? Je Tanzania inaweza kuendeshwa kwa mabavu kiasi hiki? :angry:

Maoni: Vurugu nchi hii zitaletwa na CCM

Ewe mwananchi chukua hatua kulinda amani ya nchi hii.

ccm ni janga la kitaifa
 
jwtz waoga tu nilimpiga 1 wakaja 20 nikatokomea.wanajivunia uwingi wao
 
Mjsimon hii habar haina ukweli wowote kuhusisha vyama siasa ,jeshi la wananchi na idara ya maji Kwa kupgwa watu hapana nenda FB kadanganye uko!
 
Back
Top Bottom