JWTZ yaapa kupambana na majambazi wanaopora silaha za askari

Vituko ni kaporwa Vituo Vya Polisi ni uzembe na itabidi Polisi iangalie mfumo wa mafunzo na ajira zake ....hata Siku Moja haiwezekani Askari wakae mahala bila kupeana cover ...yaani kituo Kina Askari 10 na wote walaleee au wote WAWE ndani wanapiga stori bila kuweka security ring ...at least Kama wanalala kibinadamu ...basi ...angalau wanne wa form security KUZUNGUKA kituo kwa Zamu ......
askari hufunishwa kuwa angalau wawili MAHALI ....ili ikitokea kulala ...analala mmoja na mwenzake anamlinda ...au Kama wanatembea basi wanatembea kwa kupeana ulinzi na sio wanatembea kizembe wote wametazama sehemu Moja hadi wanatekwa Kama Kuku ...
 
Kazi hasa ya usalama wa nchi na wananchi ni wale jamaa wa usalama wa taifa na sio JWTZ wala police ingawaje police wana kitengo cha CID.

Halafu hao jamaa mbona bunduki wameshika tofauti, kofia wamevaa tofauti, kweli wameiva hawa?!

Mwanamayu hao ni wazalendo wa kozi ya ukomandoo bado hawajanza hata ukuruta wa hiyo kozi.
 
Inaweza isiwe salama hii mambo tutajuaje km ni njia ya chama kinachotoa majambazi magereza kuja umiza wapinzani ,ndio kinajikusanyia silaha kuja zitumia ktk vurugu za uchaguzi?Si habari nzuri sana kwa usalama wa taifa.
 
Very unfortunate jeshi la polisi limebaki na intelijinsia ya matukio yatakayoambatana na events za vyama vya siasa tu especially wapinzani, lakini mambo ya wizi wa mali ya umma ni WEUPE. Kila polisi anatakiwa kuandika barua akieleza ni kwa nini asifukuzwe kazi kwa uzembe huo?
 
Wapi jwtz wametoa tamko kama kichwa cha habari kinavyonadi?mods futeni uzi huu

Umeambiwa ni Katibu Mkuu! Kwani unafikiri Katibu Mkuu ni mdogo? Akiamua akijadiliana na Mkuu wa Majeshi wazee wa kaz wakiingia mtaani,hilo linawezekana if and only if kama Polisi wakikiri kuelemewa!
 
Nimewahi kusema kwamba ujinga wa serikali ya CCM uraligharimu TAIFA KWA KIASI KIKUBWA.Wamelichezea jeshi la POLISI mpaka wamefanikiwa sasa limeoza,Wameanza kuhamia,na kujisogeza taratibu ndani ya jeshi la wananchi,ingawa nalo sijui Kama bado ni la wananchi maana mambo tunayoyaona ktk nchi yetu ni yakusikitisha sana,maana tunayoyaona SASA NDIO MATOKEO YA KUKATAA AZIMIO LA ARUSHA na kuyatupilia mbali MAADILI.NCHI HII TUNAKOKWENDA TUNAHITAJI MTU MWENYE AKILI TIMAMU KUWA RAIS WETU na sio kundi hili la wajinga la akina KIKWETE na wenzake.WANAJESHI JWTZ na POLISI WANAJUA NCHI YETU INA WIZI Unaotishia AMANI YA NCHI lakini wanautetea.Sisi WAAFRIKA TULIOTESEKA KWA UTUMWA DUNIANI HATA KUPELEKEA KUKOSA MAENDELEO TUNAPASWA KUJITAFAKARI KWA MANUFAA YETU NA KILA MTU AWE NA UCHUNGU JUU YA MWENZAKE KWA MAANA YA UZALENDO.
 
JWTZ(1).jpg






Jeshi la wananchi nchini (JWTZ) kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama nchini limeahidi kukabiliana na makundi ya watu wanaodaiwa kuwa majambazi sugu ambao wanapora silaha za askari huku wengine wakiuawa hatua ambayo imeanza kutishia usalama wa nchi.


Akizungumza na jijini tanga kufuatia hivi karibuni makundi hayo kupora silaha na kisha kuua askari huko rufiji mkoani pwani na wengine wakipora askari wawili silaha nyakati za usiku jijini tanga na kisha kuwadhuru hatua ambayo imesababisha kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa tanga bombo,katibu mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa JOB MASIMA amesema vyombo vya ulinzi vitakaa na kuhakikisha kuwa mtandao huu unapatikana ili kurejesha silaha hizo.

Hata hivyo katibu mkuu amekana vikali kuwa huenda makundi haya ya uhalifu yanayojihusisha na kupora silaha askari kwa na wahitimu waliopitia mafunzo ya jeshi la kujenga taifa JKT ambao baadhi yao hawakupata ajira baada ya kurudu uraiani na kuongeza kuwa hata wanaojihusisha na ugaidi sio wote ambao wamepitia mafunzo ya kijeshi.


Sina hakika na hilo kama wataweza. Siku hizi hawana tena ule ujasiri wa Mwalimu....!!!!
 
Watanzania watu wa ajabu sana, jeshi linataka kusaidia upatikanaji wa silaha kwa kutambua kwamba kuna uwezekano wahusika wa tukio ni watu ambao wamepata mafunzo ya kijeshi, ni vigumu kwa afisa wa polisi kudhibiti. Mnataka kuleta siasa.

Kwanza wakarudishe wanyama hai waliopelekwa Doha-Qatar, wakishindwa wahakikishe pesa za Escrow zinapatikana kwakuwa wahusika wote wanafahamika, wakimaliza huko hao JWTZ ndio waje na huo upuuzi wanaotaka kutuletea!
 
Kwanza wakarudishe wanyama hai waliopelekwa Doha-Qatar, wakishindwa wahakikishe pesa za Escrow zinapatikana kwakuwa wahusika wote wanafahamika, wakimaliza huko hao JWTZ ndio waje na huo upuuzi wanaotaka kutuletea!

Mmechoka amani, subiri watupe zile za kukaa ndani miezi mitatu kutuliza machafuko. Halafu muendelea kudai pesa za escrow mkiwa majumbani. Tupeane muda tushuudie kiongozi
 
Back
Top Bottom