Mwiba
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 7,607
- 1,764
29th April 2014
Kundi la wanajeshi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wanadaiwa wamevamia kituo cha Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU) kilichopo Kwa Mrombo na wanadaiwa kutembeza mkong'oto kwa askari kadhaa.
Baadhi ya wanajeshi wanadaiwa kukamatwa, ingawa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alipotakiwa na NIPASHE kuzungumzia tukio hilo alikanusha.
"Hakuna tukio kama hilo, wewe uliona wapi watu wa serikali wanapigana," alihoji Kamanda Sabas na kuongeza: "Sisi tulikuwa kwenye vikao vyetu vya kawaida.
Hata hivyo, msemaji wa JWTZ, Luteni Kanali Eric Komba, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo wakati akizungumza na NIPASHE kwa njia ya simu jana jioni.
Hata hivyo, alisema polisi na JWTZ wanafanya uchunguzi wa tukio hilo na taarifa zikishawasilishwa makao makuu watatoa taarifa.
Lakini baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo walisema tukio hilo lilitokea majira ya saa tano au sita asubuhi jana, baada ya wanajeshi kuvamia kituo hicho kwa nyakati tofauti.
Inadaiwa wanajeshi hao walikuwa kati ya 50 hadi 60 hivi na haikufahamika mara moja walikuwa wametokea kambi gani ingawa baadhi ya watu walidai walitokea Monduli.
Shuhuda mwingine alisema aliwaona wanajeshi wanne wakiingia kwenye lango kuu la kuingilia kituo hapo na kutembeza kichapo kwa askari aliyekuwapo.
Hata hivyo, habari zingine zinasema hakuna polisi aliyepigwa na hakuna mwanajeshi aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Baadhi ya wakazi jirani na eneo hilo walisema waliwaona kundi la wanajeshi wakiwa katika eneo hilo na wengine wakikimbilia kwenye mashamba.