JWTZ wakanusha taarifa ya Mabeyo kuingilia suala la Spika

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Siku za hivi karibuni kumekuwepo na taarifa za kupotosha ambazo zimekusudia kuwahadaa Watanzania kupitia mitandao ya Kijamii hususan YouTube, kwamba Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Salvatory Mabeyo anaingilia kati sakata la Mhe. Rais na Spika. Jambo ambalo siyo la kweli.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika na linawaomba wananchi kuzipuuza taarifa zilizowekwa kwenye mtandao huo kupitia kwenye channel inayojiita NEWS 24 zenye kichwa cha habari ‘‘KIMENUKA MKUU WA MAJESHI MABEYO ATOA AMRI NZITO KUJIUZULU KWA NDUGAI’’ na ‘‘MKUU WA MAJESHI MABEYO AINGILIA KATI SAKATA LA RAIS NA SPIKA’’.

Ukweli ni kwamba, kikundi cha watu wachochezi kimetoa taarifa za uongo na uzushi kwa kutumia sauti isiyo ya Mkuu wa Majeshi huku wakiwaaminisha Umma kuwa ni sauti ya Jenerali Mabeyo kwamba aingilia kati sakata la Mhe. Spika.

JWTZ linawaomba Umma wa Watanzania kutoziamini taarifa hizo na wazipuuze kwa kuwa ni taarifa za uzushi na uchochezi zinazotungwa na kusambazwa na kikundi cha watu wasioitakia mema nchi yetu kwa maslahi yao binafsi.

Mkuu wa Majeshi hajatoa taarifa yoyote kuhusiana na yaliyozushwa kwenye mitandao kwa kuwa JWTZ halijihusishi kwa njia yoyote ile na masuala ya kisiasa na kamwe halitafanya hivyo.

JWTZ linatoa onyo kwa wale wote wanaotumika kumchafua Mkuu wa Majeshi, kwa lengo la kutaka kuliingiza Jeshi kwenye siasa. Kamwe watu hao hawatafumbiwa macho na pindi watakapobainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ili liwe fundisho kwa wengine.

Tunawaomba watanzania wote kuungana kwa kuendelea kupuuza na kukemea vikali taarifa hizo ambazo hazilitakii mema Taifa letu.

Nitumie fursa hii kuwahakikishia Watanzania wote kwamba JWTZ lipo imara, linaendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na kwa mujibu wa Katiba kulinda na kuimarisha mipaka ya nchi yetu. Aidha, JWTZ linatekeleza majukumu yake ya msingi na lina mipaka yake kama yalivyoainishwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Daima JWTZ litamlinda na kumtii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu.
 

Attachments

  • PRESS RELEASE.pdf
    169 KB · Views: 26
Mambo kama haya yanadhihirisha kuwa tuna kiongozi dhaifu sana, mda utaongea zaidi
 
Hahhahha hao makanjanja wanalo hua wanaandika takataka kwenye vi chanel vyao uchwara
Wapigwe tu maana hakuna namna
24news Mnalo pumbaf zenu!
😁😁😁
 
Mambo ya jeshi bhana...

Usikute huku wanatoa taarifa ya kukanusha, kumbe jamaa wa Dar24 na wenyewe usiku kucha hadi sasa wamelazwa kwenye bwawa la maji machafu kambini!!

Kwa nini wasishitakiwe na kufikishwa Mahakamani ? Jeshi linaapa kulinda raia na siyo kutesa!
 
Hii channel inamilikiwa na nani, kwa nini wasiadabishwe kwa uzushi?

Leo nimeona wameandika WAZIRI MKUU KUONDOLEWA....Ingawa huwa sihangaiki kupoteza MB kwa Channel kama hizi unless nikiona taarifa kama hiyo kwenye Channel kama Ayo n.k.
 
Sasa kwani umeambiwa wamewatesa hao watu?!

All in all, kazi ya jeshi ni kulinda mipaka ya nchi... hayo ya kulinda raia ni kazi ya polisi ambao hata hivyo ndiyo wanaoongoza ku- harass raia!

Siyo kweli, kazi ya kwanza ya Jeshi lolote Duniani kwenye nchi ya kidemokrasia ni kulinda raia wa nchi yao, mipaka hata polisi wanalinda ukivuka mipaka kuna Polisi wanalinda boda, isitoshe nchi nyingi Kikatiba kabisa inakatazwa Jeshi kupiga raia hata kama kuna fujo maadamu fujo hiyo siyo ya foreigners Jeshi halipaswi kuingilia ni mwiko Jeshi kupiga raia wake wenyewe, ni kuwalinda tu!
 
hawa jamaa akili zao wanazijua wenyewe kuna siku niliona wa mepost kuwa waziri mkuu kafumaniwa dah hafu wameweka na kapicha kake wa meediti nchi ina vijana wa ovyo sana hii.
 
Back
Top Bottom