JWTZ: Tanzania haipigani na M23

JWTZ: Tanzania haipigani na M23

G.Jacob

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2013
Posts
3,617
Reaction score
3,484
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) limesema
Tanzania haipigani na waasi wa
M23 na haina tatizo na Rwanda
kuhusu Operesheni ya Ulinzi wa
Amani inayoendelea katika
Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo (DRC).
Ridhaa ya kikosi hicho kwenda
DRC ilitolewa pia na Rwanda,
nchi ambayo ni mwanachama
wa nchi za Ukanda wa Maziwa
Makuu ambayo imesaidia sana
kwa kuruhusu kikosi cha
Tanzania kupitisha watu, vifaa
na zana kwenda DRC.
Msemaji wa Jeshi hilo, Meja Erick
Komba alisema hayo jana
kutokana na habari za
kupotosha zilizotolewa na
baadhi ya vyombo vya habari
kuhusu kikosi cha jeshi hilo
kupigana na M23.
Alitaka ieleweke kuwa kikosi cha
Tanzania kilicho DRC ni sehemu
ya Brigedi ya Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika
(SADC) iliyotoa mchango katika
Kikosi Maalumu cha Kulinda
Amani cha Umoja wa Mataifa
(MONUSCO).
"Kwa kuzingatia kuwa kikosi
chetu kiko chini ya majeshi ya
MONUSCO, inamaanisha kuwa
operesheni hiyo ni ya Umoja wa
Mataifa,” alisema. Alisisitiza
kuwa kikosi hicho kinafanya kazi
chini ya MONUSCO kikiwa na
majukumu ya kuzuia waasi,
kuvunja nguvu za waasi na
kupokonya silaha makundi yote
ya waasi.
"Kwa mantiki hiyo ieleweke
kuwa ushiriki wa Tanzania katika
operesheni unatokana na
mgogoro kati ya Serikali ya DRC
na waasi, hususan kikundi cha
waasi cha M23," alisema Komba.
Alisema mgogoro huo ulianza
Aprili mwaka jana baada ya
kikundi cha M23 kujitoa kwenye
Jeshi la DRC na kuanzisha
mapigano, hali iliyofanya
usalama DRC kuwa mbaya.
Komba alisema kutokana na hali
hiyo ya usalama, wakati wa kikao
cha viongozi wa Nchi za Maziwa
Makuu cha Julai 12, mwaka jana
Addis Ababa, Ethiopia, Rais
Joseph Kabila aliwasilisha ombi
kwa wakuu wa nchi za Rwanda,
Uganda na Tanzania zisaidie
kuwapokonya silaha waasi wa
M23.
Alisema wakuu wa nchi hizo
walikubaliana na ombi hilo na
kutoa maelekezo kwa mawaziri
wa ulinzi kuyajadili. Alisema
mawaziri walikubaliana kuwa ni
muhimu kwa vikundi vyote vya
waasi (ADF, FDLR na M23)
kushughulikiwa na waliwasilisha
mapendekezo yao kwa wakuu
hao.
Alisema baadaye taarifa hiyo
iliwasilishwa kwa wakuu hao
ambao waliagiza kushirikishwa
kwa nchi wanachama wa SADC,
Umoja wa Afrika (AU) na Umoja
wa Mataifa (UN) ili kufanikisha
mkakati huo.
Komba alisema nchi za SADC na
za Maziwa Makuu kwa pamoja
zilikubaliana na kupendekeza
Brigedi ya SADC ipelekwe DRC
kama Kikosi Maalumu cha
Kulinda Usalama (NIF).
"Kutokana na ridhaa hiyo nchi
wanachama wa SADC ziliombwa
kuchangia na kukubali, lakini UN
ilipitisha nchi za Tanzania, Afrika
Kusini na Malawi kuchangia
askari na kuunda NIF ya
MONUSCO.
Aidha, UN mwaka huu iliridhia
mapendekezo ya wakuu wa nchi
za Maziwa Makuu na
wanachama wa SADC kuundwa
NIF na kupelekwa DRC.
Kwa idhini hiyo, Machi 28 Baraza
la Usalama la UN lilipitisha
Azimio namba 2098 (2013) na
kutoa jukumu maalumu la ulinzi
wa amani DRC, likijumuisha
ushiriki wa NIF kama sehemu ya
MONUSCO na kuitwa Brigedi ya
Majeshi ya Kulinda Amani ya UN
(FBI) yenye mamlaka ya kujibu
mapigo ambayo kikosi cha
Tanzania ni sehemu ya Brigedi
hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-
Maelezo, Assah Mwambene
alisema hakuna ugomvi wowote
kati ya Tanzania na Rwanda na
kuasa baadhi ya vyombo vya
habari hasa magazeti, kuacha
kuandika habari za uchochezi.
Alitaka magazeti yasiwe sehemu
ya kuchochea uwepo wa
majeshi ya Tanzania Mashariki
mwa DRC kama ni majeshi
yanayojitegemea bali yako chini
ya UN.
"Kwa kuandika habari hizo,
inaleta taswira mbaya na
kuchanganya wananchi kwa
kuandika hasa vichwa vya habari
vya uchochezi," alisema.
 
tulikuwa tunajua ila Manyerere alikuwa hajui alidhani adui yetu ni rwanda
 
Back
Top Bottom