Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Wakati dunia inazungumza kuhusu vita vya kisasa vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu, jeshi la Tanzania bado limebaki nyuma likifanya mazoezi yasiyo na tija.
Badala ya kuwekeza kwenye zana za kivita za kisasa na mbinu za kijeshi zinazolingana na zama hizi, mara nyingi wanajeshi huonekana wakitumia muda katika nyimbo za hamasa, gwaride, na mazoezi ya heshima.
=============
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kupitia Brigedi ya Faru, limehitimisha zoezi la medani Pima Uwezo 2025 lililofanyika mkoani Shinyanga.
Akimwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob Mkunda, katika kilele cha kuhitimisha zoezi hilo, Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu, Meja Jenerali Fadhili Nondo, amewataka maafisa na askari kuwa tayari nyakati zote kulinda mipaka ya nchi kwa njia ya ardhi, anga na maji dhidi ya uvamizi wa adui.
"Mazoezi ni sehemu ya kutufanya wanajeshi tuwe tayari nyakati zote katika kutekeleza majukumu ya ulinzi wa taifa. Hivyo, wakati wa amani tunapaswa kuvuja jasho jingi ili wakati wa vita tutekeleze majukumu yetu kwa ufanisi mkubwa," amesema Meja Jenerali Nondo.
Aidha, amesema mazoezi hayo yataendelea kufanyika kwa nyakati na maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa na askari wa JWTZ.
Kwa upande wake, Kamanda wa Brigedi ya Faru, Brigedia Jenerali Gabriel Kwiligwa, amesema zoezi hilo limefanyika kwa siku 12 likiwa na lengo la kupima utayari wa vikundi katika kukabiliana na matishio mbalimbali ikiwemo ugaidi, uvamizi kutoka ndani na nje ya nchi, pamoja na kuzuia uhamiaji haramu.
Zoezi la medani Pima Uwezo 2025, lenye kaulimbiu isemayo “Pima Uwezo, Kaa Tayari Tuilinde Tanzania”, pia limeshirikisha askari wa Jeshi la Akiba (Mgambo)