JWTZ nako kunahitajika reforms

Unaona nini hapa...?
1. Rear Admiral Ameir Hassan aliteuliwa kuongoza Kamandi ya Jeshi la Wanamaji kuanzia Okt 2023 hadi sasa.
2. Kwa sasa Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu ipo chini ya Meja Jenerali Fadhili Omary Nondo kuanzia tarehe 28 Disemba 2022 akipokea kijiti hicho toka kwa Meja Jenerali Antony Chacha Sibuti (Mstaafu).
3. Meja Jenerali Shabani Mani aliteuliwa kuwa Kamanda wa Jeshi la Anga kuanzia tarehe 23 Aug 2021 hadi sasa..
4. Mkuu wa Kamandi ya Vikosi Chini ya Makao Makuu ya Jeshi Meja Jenerali Iddi Nkambi
5. Meja Jenerali Rajabu Mabele Mkuu wa JKT kuanzia tarehe 19 May 2021 hadi sasa

Jeshi lina kamandi 5 na jeshi la kujenga taifa.
 

There you go!
 
Umenikumbusha huyu member kavulata simuoni sijui yupo
 
Nakubaliana na wewe kuhusu Gen Z; lakini hilo la akina Mulilo, hapana.

Sasa hivi watakuwa wanajipongeza kwa kazi waliyofanya, na kutegemea kuwa matokeo yake yatakuwa ni fundisho kubwa la kuzuia hali ya namna hiyo isitokee tena. Na watahakikisha kila mara wanakumbushia.

Hili ndilo tegemeo lao kubwa la kuendelea kuwa na hali ya uoga miongoni mwa wananchi,... AMANI itatamalaki kila mahali Tanzania kwa miaka mitano ijayo!
 
Umenikumbusha huyu member kavulata simuoni sijui yupo
Siyo yeye tu, akina Tlatlaah' unawaona tena?
Kuna kundi kubwa sana la watu hao waliingia humu JF kwa lengo maalum; na ninakisia kuwa mambo yatakapoanza kutulia kidogo tena chini ya ngwe hii mpya baada ya kuapishwa; utawaona tena kwa wingi kuja kujipongeza kwa kazi kubwa iliyo fanyika.

Hatupo salama tena kama tulivyokuwa tukifikiri. huko siku za nyuma.
 
Hii mipango yao Kikwete, Samia, Rostam ya kuweka watu wao sehemu zote nyeti na muhimu kama jeshini, wizarani, kurugenzi, usalama wa Taifa, Polisi, TRA, TCRA, TPA, TCAA, inaonekana ilipangwa hata kabla JPM hajafariki au siku ya kwanza baada ya Samia kushika madaraka ukiangalia teuzi zote Samia alizofanya.

Kama Kikwete alivyopanga na kumpendekeza Samia awe makamu ili awe anampa taarifa na maamuzi na nini kinaendelea ikulu awamu ya tano ndivyo alivyopanga kuwa na watu wake sehemu zote muhimu awamu ya sita na sasa hivi.
 
Mh 🤔
 
Nenda kaifanye hiyo reforms mzee kama mlivyofanya hiyo nyingine
 
Axheni kujifariji hakuna mlichonadirisha hadi sasa mlisema patachimbika na hataapishwa imekuwaje mbona ameapishwa?
 
Mashaka ya nyerere yanai licost jeshi letu hadi leo, hofu ya kufanya mabadiliko bado inatanda sababu ya mtu ambae aliipamda kwa sababu zake binafsi
 
Kwa kilichotokea, Tanzania ndio basi tena hakuna mahala pana afadhali. Inasikitisha ila tumeanguka pakubwa sana, Mungu atusaidie
 
CC Lwiva
Unasemaje kuhusu hiyo list....
Usipige makelele ukianza kulia, lia kimya kimya.....
 
Kilichofanyika si cha kujipongeza..mwena wazimu ndio anaweza jipongeza bila kujua kwamba hakuna udhalimu unapita bila malipo yake..!
 
Lakini na Kiongozi wa juu awe wa kwanza kuonyesha uongozi bora, na hawa wenye akili za kichalamila , bashite waache hizo akili za kitoto hazi wasaidi kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…