JWTZ na Polisi nao hupiga kura kwenye Uchaguzi Mkuu kwa Tanzania Bara?

😁😁😁 umefafanua lakini bado kuna utata...bado tu najiuliza Askari au mwanajeshi akapiga kura alafu akatangazwa magufuli mshindi wakati yeye (polisi au mwanajeshi) alimpigia Lissu, then kukatokea vurugu wao wakatumwa wakazime zile vurugu huoni kuwa kunaweza kuwa na uasi hapo hata na wao wakaungana na waandamanaji ?
Tunatazama tupo wangapi tunaomuelewa Lissu, tukiwa wengi tunawageuka wenzetu tunaungana na raia tunaamini sections zingine huko zilipo zitatuunga mkono, dikteta anatoka madarakani, hivyo yani
 
😁😁😁 haya bhana.
Hiyo rahisi ni typing error tu ngoja ni edit.
Sawa. Ila ngoja niweke hint kwa heshima yako.
Ila uwe askari ndani ya JMT lazima uwe raia wa JMT. Na kila raia wa JMT ana haki zake za msingi. Tukirudi juu tulikoanzia, kwa sababu askari tumesema ni raia wa JMT, tayari wana haki zile za msingi za raia kama wengine.
Kuna conditions nyingi zinaweza kukunyima baadhi ya haki zako kama raia mfano uchizi, kufungwa jela... Hiyo nayo ni mada nyingine. Good day.
 
Tunatazama tupo wangapi tunaomuelewa Lissu, tukiwa wengi tunawageuka wenzetu tunaungana na raia tunaamini sections zingine huko zilipo zitatuunga mkono, dikteta anatoka madarakani, hivyo yani
😁😁😁 mkifanya hivo maana yake mme asi kiapo chenu na uasi ni kosa kwa mujibu wa sheria za jeshi.
Kwa hiyo hapo itaanza vita kati ya waasi na watiifu kwa serikali iliyopo mamlakani na sidhani kama mtakuwa na silaha za kutosha kupambana na watiifu.
Zaidi hapo mtaishia kwenye magereza na kijeshi mkahasiwe huko .
 
Sawa. Ila ngoja niweke hint kwa heshima yako.
Ila uwe askari ndani ya JMT lazima uwe raia wa JMT. Na kila raia wa JMT ana haki zake za msingi. Tukirudi juu tulikoanzia, kwa sababu askari tumesema ni raia wa JMT, tayari wana haki zile za msingi za raia kama wengine.
Kuna conditions nyingi zinaweza kukunyima baadhi ya haki zako kama raia mfano uchizi, kufungwa jela... Hiyo nayo ni mada nyingine. Good day.

Noted
 
Tushapiga kura mapema sana, waliweka posho ya chakula toka juzi wakidhani itatutoa ufahamu tumpigie dikteta kumbe askari wengi tu wanajifahamu!
Maelekezo ni hakuna kuchovya kidole tukapige tena kituo kingine kumbe kote huko tunakwenda tunatia tiki kwa yule mgombea wa mwisho ya karatasi. Tayari nimepiga kura mbili kwa mgombea wa mwisho, hapa naelekea na vijana wangu kituo cha tatu kupiga kura, napo nimewaelekeza vivyo hivyo mgombea wa kupigiwa niyeye, hawa ccm mkoa walidhani wanamkomoa niyeye kumbe hawajajua ana supporters kibao tu kwenye taasisi

Hata upige kura atakae apishwa ndiye utakae mlinda
 
😁😁😁 mkifanya hivo maana yake mme asi kiapo chenu na uasi ni kosa kwa mujibu wa sheria za jeshi.
Kwa hiyo hapo itaanza vita kati ya waasi na watiifu kwa serikali iliyopo mamlakani na sidhani kama mtakuwa na silaha za kutosha kupambana na watiifu.
Zaidi hapo mtaishia kwenye magereza na kijeshi mkahasiwe huko .
Hakuna ukombozi bila sadaka mkuu!
Siku zote madikteta hutolewa kwa style hiyo.
Usichojua tu mkuu katika vita hii tutshinda maana waliomchoka huyu meko na chama chake ni zaidi ya nusu ya askari wote, JW na PT. Kinachosubiriwa ni nani tu atakayelianzisha ili aungwe mkono. Tunasubiri ma-CO wa vikosi vikubwa watoe tamko then dikteta atoke!
 
Wakuu Habarini za Asubuhi.

Nilikuwa naomba mwenye ufahamu kuhusu hiyo title hapo anijuze.

Je, Jeshi la wananchi wa Tanzania pamoja na Askari polisi nao huwa wana haki ya kupiga kura kuchagua viongozi wa nchi?

Maana kuna kazi zingine najua huwa zina miiko yake na katika hili mimi nilikuwa nadhani hawapigagi kura kwenye uchaguzi mkuu wa kitaifa, lakini nilichokiona jana huku Zanzibar kimenifanya niulize swali hapa leo.

Hao wote wanayo haki ya kupiga kura alimuradi awe mtanzania wenye umri zaidi ya miaka 18 na awe amejiandikisha kupiga kura .
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ unapiga kura umevalia kiraia alafu umepigia maalim seif then badae ZEC wanamtangaza Mwinyi mshindi wa uchaguzi.
Then baada ya siku moja Maalim anaitisha watu waingie Bara barani kupinga matokeo
Na wewe unavaa uniform kwenda kupiga watu wabomu ya machozi, vipi utapiga ama utaambatana na waandamanaji na ww kupinga matokeo 😁😁😁
Kwani unayempigia kura ni lazima ashinde. Yeye polisi au mwanajeshi si atakubali tu kuwa niliyempigia kura hajashinda so anaendelea kutekeleza majukumu yake ya kazi
 
Kwani unayempigia kura ni lazima ashinde. Yeye polisi au mwanajeshi si atakubali tu kuwa niliyempigia kura hajashinda so anaendelea kutekeleza majukumu yake ya kazi
Suala linakuja pale panapoonekana wazi kuwa kweli kulikuwa na udanganyifu ama wizi wa kura na ushahidi ukawepo.
Je na wewe utaenda kuwapiga wanaomuunga mkono mgombea wako aliyehujumiwa ?
 
Ila kwa hawa wakwetu si yanapelekwa tu kama mang'ombe yatatoa wapi jeuri ya kugoma hata kama mgombea ameibiwa kura
😁😁😁 mkuu kuwa makini, wakija hapa wakaiona hii comment watakufanyia U-spy mpaka wakupate.
Kuitwa mang'ombe siyo lugha nzuri kwa Walinzi wa nchi yetu.

Na wakikupata kweli wataenda kukuonesha kuwa wao ni mang'ombe πŸ˜‚
 
Back
Top Bottom