JWTZ kulinda amani na usalama Uchaguzi Mkuu

kangalawe

Enzi ya mwalimu askari alikuwa anachunguzwa na jeshi mienendo yake wakati yuko uraiani. Nina maana kulikuwa na kitengo cha military civialian inteligence ndani ya military police.

Lakini leo sijui kama kipo au la...maana wanajeshi wetu ndio wengi vijana(baadhi yao)ndio wavaa milegezo mitaani.
 
Last edited by a moderator:
kulichi

Wewe tulia nikwambie. Ni kawaida yenu kuishi kwa upotoshaji tu. JWTZ ni jeshi lenye wajibu wa kulinda usalama wa nchi yetu,na kuhakikisha mipaka ya nchi yetu haaingiliwi na adui yeyote kutoka nje.katika kipindi chote cha uhuru wetu. Pia linawajibika na kukabiliana na uasi wowote unaoweza kutokea ndani ya nchi.

Na haiishi hapo tu,pia linahusika na utoaji wa misaada ya dharura katika uokoaji na majanga ya kiasili.iwe katika ujenzi wa miundombinu ya dharura au uokoaji wa maisha ya binadamu. Iwe kimbunga,mafuriko au mioto mikubwa yenye kuhofiwa kushindikana kudhibitiwa na mamlaka husika na kwa wakati husika.

Sasa wewe unakurupuka na kusema tunapost bila kujua wajibu wa jeshi letu. Je unafikiri wote tuna fikiri kwa upande mmoja tu kama wewe?

Tunaweza kukupa mfano wa nchi kama Rwanda ambako jeshi hufanya doria mitaani nyakati za usiku nchini kote sambamba na polisi.
Na hii ni kwa kuwa nchi ile bado iko latika hali ya tahadhari kijeshi kwa kuhofia waasi wa kihutu wa NFDLR walioko kwenye misitu ya virunga kule goma DRC mpakani na Gisenyi nchini rwanda.

Lakini wanapokuwa wana patrol wako makini sana.tukio lolote la kiraia la kihalifu huwa hawaingilii bali huwaachia polisi wafanye kazi yao.wao hubaki wakiendelea mbele.

Sasa hapa kwetu ni lipi linalowafanya hawa makamanda kuanza mazoezi ya pamoja as if tuna tishio la kivita na nchi jirani?
Na kwa nini iwe sasa na si wakati mwingine hapo awali?
 
Last edited by a moderator:
Tatizo tumejiandaa kukataa matokeo ndio maana hofu iko,kama ukipiga kura yako kisha ukarudi kwenye shughuli zako ha wakifanya mazoezi ya kivita mbona hamna shida.

Tuwaachie kama hapo awali ili muibe?
Kwani kuna ubaya gani sheria ya uchaguzi ikifuatwa.maana inasema ni ruhusa kukaa mita mia moja kutoka kituo cha upigaji kura mradi usivunje amani.
 
ni kawaida mtu yeyote mwizi jambazi mfanyabiashara ya magendo mfanya fujo akiona polisi au jeshi anakuwa mwoga

Kweli kabisa,wezi ccm wanaogopa raia kuwepo eneo la upigaji na uhesabu kura maana watashindwa kuiba.
Sasa wanataka kutisha raia wema.
 
mkuu msamehe bure mtoa uzi hata hajui anachokisema ni nini,ndo walevu tunaona kuwa ni mchonganishi tu kwa lengo la kuibua hisia za watu na kupima upepo juu ya msimamo wao.

Endelea na uzi wangu nimeisha muelewesha mwenzio aSiyejitambua kama wewe na utanielewa vizuri
Mimi si mkurupukaji kama wewe.mara nyingi nachangia au kupost kitu kinachoeleweka na si utaratibu wangu kutoa sentensi moja na kuishia.

Pia nina kuwa na uhakika na ninachokisema kwani lazima niwe na taarifa ambayo ina chanzo kamili(source).

Mimi sijafungiwa ndani katika maisha yangu.
Nimetembelea nchi nyingi kidogo.hivyo nina mengi niliyojifunza.na pia ni msomaji mzuri na mfuatiliaji wa mambo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi yetu.
Karibu kwa hoja na si sentensi moja moja
 
commonmwananchi

hizo ni military drills za kawaida tu na huna cha kuhofia kwani hata mwanaume hutakiwa kupiga kwanza punyeto kabla ya kukandamiza beibe.
 
Last edited by a moderator:
MazoeZ n sehem ya kaz yao we jiandae kupiga kura na kulinda matokeo mbona mwanza kuna lamb nyng na nzito but ccm waliangushwa vbaya, acha watimize wajib wao cc tutatimizia kwenye poll station
 
commonmwananchi

Kijana elewa kuwa kisu usipokinoa mara kwa mara kitapoteza makali yake, ondoa shaka hao wanajikumbusha mambo yao tu
 
Last edited by a moderator:
yaani wakifanya mazoezi ya jeshi ni kujiandaa kuvunja aman ya nchi? hujui km ni wajeshi?
 
Siku zote walikuwa wapi hadi leo ndiyo wafanye mazoezi. Ni mara ngapi mabasi yametekwa mbona wasifanye mazoezi ya kusaka majambazi. Watu wakidai haki zao ni vurugu kwa upande wenu? Wapi watu wamepatia haki wanayoitaka pakatokea fujo
We mazoezi yote unayajua kiongozi??!!
Kama ingekuwa jambo la mficho hakika usingesikia wala nchi kubwa sana hii na sehemu za mazoezi.zipo nyingi!!!
We andaa vitu vya kupigia kura fanya yako sio kuanza kutishana humu jeshi this jeshi that, jeshi likamua wala halihitaji hayo unayoyaita mazoezi ili kutimiza adhma yake yeyote ile!!!

Tuendelee kuishi kuheshimu sheria huku tunaomba tuepushwe na machafuko
 
yaani wakifanya mazoezi ya jeshi ni kujiandaa kuvunja aman ya nchi? hujui km ni wajeshi?

Hivi jeshi linaloaminiwa kulinda nchi kama kweli wanataka kufanya yao wanahitaji mazoezi, kwa resistance gani haswa???!!
Polisi tu wakishuka "half of a length" watu kelele kila media mpaka bungeni halafu chokochoko za jeshi zinaongelewa kiuwepesi tu . . . . . .eti wanajiandaaa!!!

Mungu atuepushe sana!!
 
Kama ni jeshi letu hakuna kuogopa.....cha msingi utafiti wa kina ufanyike hao wanaofanya mazoezi wasijekuwa wafuasi wa ccm.
 
OLESAIDIMU

Wewe niambie ni nani katika watawala wetu anayeheshimu sheria. Kama kila polisi anayeua raia mwema, ndiye anayepandishwa cheo!
Machafuko yatasababishwa na watawala watakaoshindwa kuhakikisha haki inatendeka katika mambo muhimu kitaifa kama uchaguzi huru na wa haki.


Tusitumie machafuko kama kinga ya kutisha raia wasijitokeze kupiga kura ya kuchukua maamuzi magumu.
 
Last edited by a moderator:
Mbona jwtz wakitoa msaada kwenye majanga mfani, mafuriko Hulalamiki?

Huo haswa ndio wajibu wao.
Narudia tena kukuelimisha na wewe mimi silalamiki,ninachofanya ni kutimiza wajibu wangu kama raia mwema.
Sipaswi kukaa kimya wakati katiba ikichezewa.
 
yaani wakifanya mazoezi ya jeshi ni kujiandaa kuvunja aman ya nchi? hujui km ni wajeshi?

Wewe si muelewa pia..mimi nimesema kwamba ni polisi,jwtz,na magereza jambo ambalo si la kawaida kwani kila jeshi lina wajibu na mamlaka tofauti kikatiba.
Pia kamanda wao amehojiwa na kunukuliwa akisema ni mazoezi ya kujiandaa na rabsha zinazoweza kujitokeza wakati wa uchaguzi.
Je hii si dhahiri kwamba ccm wana uhakika watafanya mbinu chafu wakati huo wa uchaguzi?
 
Back
Top Bottom