Mwakitobile
JF-Expert Member
- Oct 4, 2012
- 452
- 120
Ili kurudisha uzalendo na uadilifu.Jwtz sasa linajikita kuajiri vijana waliopitia mafunzo ya Jkt tu,sasa kwa wale ndugu zangu wanaojiita wenye professional na waliokosa ajira na kudhani kuwa Jwtz ndiyo mkombozi wao,kwa sasa mambo yamebadilika kabisa,lazima kwanza usote Jkt ndiyo unaweza kubahatika kuajiriwa na Jwtz.Hivyo basi kwa wale wanaosubiri nafasi za professional kwa miaka zaidi ya mitatu sasa,habari rasmi ndiyo hiyo,ingama najua itawashtu sana.Haya yote yamethibitishwa na msemaji wa Jwtz,kanali Kapambala Mgawe leo asubuhi kupitia kipindi cha kumepambazuka(Radio One) au katika gazeti la nipashe la leo january 17 ukurasa wa 8.