Bi. Kiroboto
Member
- Dec 22, 2011
- 36
- 6
Kuna kakitu kanaitwa Banjuka kwenye matumizi ya internet ya TTCL kamenifanya niibiwe mchana kweupe na kampuni hii. Wanasema wanatoa unlimited bundles: Tsh 1000/hr kuanzia saa 12 asbh - 12 jioni, Tsh 800/hr saa 12j ioni - 3 usiku na Tsh 500/hr kuanzia saa 3 usiku - 12 asbh. Kiukweli nilivutiwa sana, nikanunua modem yao nakuanza kutumia. Wizi ulianzia pale nilipoanza kudownload nikakuta speed inashuka hadi 0.15kbps wakati waliniambia speed yao inafika 3Mbps. Kiukweli max. downloading speed niliyoona hapa ni 70kbps tena mara chache sana. Kiukweli saa inakatika ukiwa hujafanya lolote la maana.
Sijaona issue yoyote. Nadhani unalenga kuichafua ttcl. Tuambie basi unatushauri tutumie mtandao upi?
Ha ha haaa...werevu ndio waliwao...Hamia Airtel...
Ni sahihi. Na kwanza haifiki hiyo 3Mbps, huwa ni hadi 1.4 ikijitahidi sana. Lakini mara nyingi sana pia huwa ni 0.00, na kujikuta hauwezi kabisa kutumia internet. Lakini kwa matumizi ya downloading, bado ni package superior to all.
ID yako na Picha imeniacha hoi
Tatizo nchi yetu ni shamba la mwendawazimu ambalo kila mjanja hupita kuvuna atakacho bila ya hofu ya kushughulikiwa kisheria. Huu ni mmojawapo tu ya wizi unaofanywa na makampuni ya mawasiliano kwa hila mbalimbali bila kukemewa na mamlaka zilizowekwa na zinazoshamiri kwa kodi yetu. Hivi ni nini majukumu ya Tume ya Mawasiliano kama si pamoja na kuhakikisha makampuni haya yanacheza "fair play"? Karibu makampuni yote hayatoi huduma kadiri ya matangazo yao, wanawaibia wananchi serikali ikibaki inachekacheka tu, hayalipi kodi, bado tunawachekea tu! Hivi Tanzania tumerogwa na nani? ichezo michafu wanayoicheza hapa kamwe wasingethubutu kuicheza Ulaya na Marekani; je ni nani anabisha kwamba wanatufanya sisi ni shamba la mwendawazimu? Wenzetu Kenya na Uganda Makampuni ya Safaricom na MTN, pamoja na kwamba hayana wateja "wa kumwaga" kama hapa kwetu yamezipiku kampuni za pombe katika uchangiaji wa pato la mataifa hayo, sisi makampuni hayo hayako hata kati ya walipaji kodi wakubwa ishirini! Na bado tunategemea makampuni ya pombe na sigara kama walipaji kodi wakubwa!Kuna kakitu kanaitwa Banjuka kwenye matumizi ya internet ya TTCL kamenifanya niibiwe mchana kweupe na kampuni hii. Wanasema wanatoa unlimited bundles: Tsh 1000/hr kuanzia saa 12 asbh - 12 jioni, Tsh 800/hr saa 12j ioni - 3 usiku na Tsh 500/hr kuanzia saa 3 usiku - 12 asbh. Kiukweli nilivutiwa sana, nikanunua modem yao nakuanza kutumia. Wizi ulianzia pale nilipoanza kudownload nikakuta speed inashuka hadi 0.15kbps wakati waliniambia speed yao inafika 3Mbps. Kiukweli max. downloading speed niliyoona hapa ni 70kbps tena mara chache sana. Kiukweli saa inakatika ukiwa hujafanya lolote la maana.
unalipia kwa msaa kama internet cafe banaKuna kakitu kanaitwa Banjuka kwenye matumizi ya internet ya TTCL kamenifanya niibiwe mchana kweupe na kampuni hii. Wanasema wanatoa unlimited bundles: Tsh 1000/hr kuanzia saa 12 asbh - 12 jioni, Tsh 800/hr saa 12j ioni - 3 usiku na Tsh 500/hr kuanzia saa 3 usiku - 12 asbh. Kiukweli nilivutiwa sana, nikanunua modem yao nakuanza kutumia. Wizi ulianzia pale nilipoanza kudownload nikakuta speed inashuka hadi 0.15kbps wakati waliniambia speed yao inafika 3Mbps. Kiukweli max. downloading speed niliyoona hapa ni 70kbps tena mara chache sana. Kiukweli saa inakatika ukiwa hujafanya lolote la maana.