Juu ya ajali mbaya ya maskini_jeuri

MJ,

POle sana.. ni kweli kwamba una wakati mgumu sana lakini cha maana ni wewe kuvaa ujasiri, kuface kila kilicho mbele yako na kuomba nguvu za mungu.. saidia familia ya merehemu na saidia jamhuri, ila cha maana kuliko vyote.... weka karibu familia yako

Tuko pamoja na nadhani utapata msaada zaidi (hali na mali) kutoka JF kwani sisi ni familia
 
Wapendwa sana!

Ndio nimeingia Dodoma; kuiweka sawa familia ambapo muda wote tangu juzi nimekuwa nkiwasiliana nao kwa simu! kweli tumesawijika lakin pia kwa niaba ya familia nawashukuru wote kwa faraja zenu! kwa kweli kwa sasa ni kitu tunachokihitaji sana!

Kijana aliyefariki ndio alikuwa sababu kuu ya mimi kuwapa lifti wapiganaji wale yaani yeye pamoja na wenziwe kwa kuwa alikuwa na undugu na mtu ambaye aliwahi kunifundisha kazi huko miaka ya nyuma! kwa kweli huwa sitoi lifti na asilani kwa watu nisiowafahamu kabisa!

Lakini ndo hivyo yametokea;

Nawasiliana na wadau wangu wa kazi hapa Dodoma na pia familia kwa chochote kinachoweza kutokea! Woga upo siwezi kukataa.......ni kwa mara ya kwanza najikuta katika situation hii.........sina xperience ya chochote hivyo mawazo mliyotoa na mtayoendelea kutoa hapa nitayafanyaia kazi.

Labda nisahihishe kidogo kuwa kesi itaendeshwa katika mahakama ya wilaya ya Kilosa; hivyo nitasafiri kuelekea Mkikumi na hatimaye Kilosa katika tarehe zilizotajwa.

Asanateni sana

maombi yetu yako pamoja na wewe hili lipite kwa salama
 
ooooo pole sana MJ maisha ndivyo yalivyo naamini kila kitu kitakwenda sawa pia usimwache Mungu atakutetea kwani yeye ni Hakimu wa haki.

RIP aliyetutangulia
 
Guys sio pole nyingi zinatolewa hapa,yeah nakubali kutoa pole kwa marehemu na pia hata bwana M_J ila pia mwishoni ni kuangalia njia gani ya kuweza kumsaidia bwana M_J kwa ushauri au hata kwa lolote lile ambapo ataweza kufanikiwa huko mahakamani maana mahakamani sio sehemu ya kuchezea isitoshe imetokea ajali na mtu kafa so tujaribu kuangalia kama kuna njia yoyote ya haraka haraka ya kumsaidia jamaa.Hapa sasa ndio ubinadamu unapoonekana sio kwenye raha tu kusifiana bila mpango wowote........Nawakilisha!!
 
asante sana kwa mawazo yako tukianza na wewe unatoa mchango gani kimawazo ?
 
Guys sio pole nyingi zinatolewa hapa,yeah nakubali kutoa pole kwa marehemu na pia hata bwana M_J ila pia mwishoni ni kuangalia njia gani ya kuweza kumsaidia bwana M_J kwa ushauri au hata kwa lolote lile ambapo ataweza kufanikiwa huko mahakamani maana mahakamani sio sehemu ya kuchezea isitoshe imetokea ajali na mtu kafa so tujaribu kuangalia kama kuna njia yoyote ya haraka haraka ya kumsaidia jamaa.Hapa sasa ndio ubinadamu unapoonekana sio kwenye raha tu kusifiana bila mpango wowote........Nawakilisha!!

ukiona mdau kaishia kutoa pole tu ujue huo ndio mchango wake na
angekuwa na la zaidi angeandika hapa jukwaani au angetuma
pm.

poles sana mj Mwenyezi Mungu akulinde na akuongoze katika kutatua
hili tatizo
 
Back
Top Bottom