Just follow dialectic pattern na fikra zetu zitakuwa chini yako

einstein newton

JF-Expert Member
Oct 18, 2015
1,969
2,672
Hegelianism ni mbinu iliyogunduliwa na mwanafalsafa wa kijerumani,Georg.w.hegel

njia hii hutumiwa na nchi zenye ushawishi mkubwa duniani pamoja na mitandao mingi ya siri

msingi mkubwa wa mbinu hii ni huu;'akili ya mwanadamu haiwezi kutambua kitu,mpaka kitu hicho kigawanywe katika sehemu kuu mbili,'wema na uovu''
mbinu hii ina hatua kuu 3;

hatua ya 1;unatengeneza tatizo fake au propaganda,kisha unatumia mass-media kuisambaza

hatua ya 2;unasubiri mwitikio kutoka kwa watu ambao wewe uliutegemea

hatua ya 3;unatoa suluhisho ambalo uliliaanda kabla ya tatizo ili kutimiza lengo lako

mf;tunataka kuiba mafuta iraq,tukisema directly dunia itatushangaa,hivyo basi tunatengeneza propaganda mf;iraq wanatengeneza silaa za nyuklia kwa lengo la kuiangamiza dunia(propaganda inasambaa)

watu wana pata hofu na kuiomba marekani(mwenzetu)kutatua tatizo(mwitikio)

marekani inasema njia pekee ya kutatua tatizo ni kuivamia iraq(suluhisho)

lakini agenda iliyo nyuma ya suluhisho letu ni kuiba mafuta

asanteni!
 
hegelianism ni mbinu iliyobuniwa na george wilhelm friedrick hegel,mwanafalsafa wa kijerumani katika karne ya 19,msingi mkubwa wa mbinu hii ni huu;"akili ya mwanadamu haiwezi kuelewa kitu mpaka kitu hicho kigawanywe katika sehemu kuu mbili,wema na uovu"...mbinu hii ina hatua kuu tatu,(1)unatengeneza tatizo (fake),(2)kisha unasubiri mwitikio ambao wewe unahuhitaji kutoka kwa watu,(3)baada ya watu kureact kama ulivyotaka unatoa suluhisho ambalo ulikuwa nalo kabla ya tatizo...mf;tunataka mafuta iraq,tukisema directly kuwa tunataka mafuta hayo,jamii na nchi nyingine zitapinga wazo letu,hivyo tunatengeneza tatizo..mf;"iraq wanatengeneza silaha za nyuklia na wana lengo la kuuangamiza ulimwengu(tatizo),watu wanapata hofu na kuiomba marekani(mwenzetu)kutatua tatizo hili(muitikio tulioutaka),marekani inasema "njia pekee ya kutatua hili tatizo ni kuivamia iraq"(suluhisho tulilolipanga kabla ya tatizo).lakini agenda iliopo nyuma ya suluhisho letu ni kuiba mafuta iraq...hii ndiyo mbinu inayotumika kutawala fikra za watu!

N kweli
 
Mbona hiyo ni confession of an economic hitman.
kuna mbinu nyingine nyingi chafu zinatumika...soma kitabu utaelewa
 
Hata Paris unaweza kuta walijifanya ni ugaidi ili wapate sababu ya kuivamia Syria

Mkuu unaposikia shambulizi lolote la kigaidi,katika nchi za magharibi haswa france,britain,au marekani,lengo huwa ni moja tu;kutengeneza hofu kwa watu wa magharibi na kuwafanya wao kuuchukia uislam!..chuki hii inatengenezwa kidogokidogo ili baadae watumie advantage hii kutriger vita ya tatu ya dunia kama ilivyotabiliwa na Albert pike!
 
Sasa mdau kama unajua si utuambie nasi tujifunze

Iko hivi:

Kabla nchi zetu maskini kukopeshwa zinafanyiwa study ya nguvu na wataalam wa uchumi kutoka IMF, WORLD BANK and the so wakopeshaji wakubwa. Lengo lao hasa ni kujua unexplored resources zilizopo.

1. Sasa hayo mataifa makubwa yanatoa the so called MIKOPO au MISAADA ya ujenzi ai Ufadhili wa Mradi fulani lakini sharti kubwa ni kuwa main contractor anatoka kwao. Lets say anayoa pesa ni IMF au world bank so most likely contractor atakuwa kampuni ya kimarekani. Anakuja anapiga kazi analipwa huko huko kwao ila nyie mnabeba deni tu. Yaani mnaishia kuona barabara au daraja au umeme au chochote lakini pesa hampewi na deni linakuwa la taifa. (Hapa local contractors hawapati hizi tender kubwa)

2. sasa wakisha wakopesha sana then the next move ni kuomba Access kwenye natural resource mlizonazo kama nchi. Kwa sababu mnadaiwa na hawa jamaa inawawia vigumu kuwanyima fursa hiyo adimu na adhim. (Mfano hai upo hapa kwetu..wakopeshaji wetu wapo kwenye madini na gesi yetu. Hata wachina nao wametumia same technic na wapo)


3. mkiwakatalia Access ya natural resource zenu kisa deni wanalilowakopesha next move ni ku create propaganda kama alivyosema mdau hapo juu. Kumbuka hapa Tanzania ile issue ya mikataba ya madini ya URANI kupewa kampuni za urusi (NMZ) kulianza kuzuka propaganda eti inatumiwa na Magaidi. Sijui wakubwa wetu walili solve vipi. Niliishia kusikia kampuni husika iliuza hisa zake ulaya.

4.Next move ni kutumia "The Jackals" ku create movement within a country ya kuleta "ukombozi" kwa wananchi...hii hujumuisha kuzuka ghafla kwa kikundi cha waasi wenye silaha kali wanaopigana na serikali ili kuitoa madarakani....hupewa support ya fedha na silaha na hao hao jamaa. Hapa ghafla huzuka vita ya wenyewe kwa wenyewe...Refer Syria, Libya, Congo etc. kwa mifano hai.


5.Hiyo hapo juu ikishindikana ndiyo propaganda inazidishwa na kuonesha nchi fulani inahatarisha "Amani" ya dunia hivyo kuleta ulazima wa kushambuliwa na mataifa makubwa ili kuondoa utawala Hatari kwao. Hapo utaona majeshi yao yakika kupigana na nchi husika kwa kisingizio hicho na Finally wanashinda.

NB:
nimejitahid kueleza kwa kifupi kitabu hicho. Wengine wataongezea.
 
Back
Top Bottom