bushland
JF-Expert Member
- Mar 6, 2015
- 7,016
- 4,961
Wanajamii sijui tunaelekea wapi katika maisha haya?
Kanisa Katoliki tumezoea kuwa na Jumuiya ndogo ndogo kwa ajili ya kusali pamoja na kushirikiana mambo mbali mbali ndani na nje ya kanisa. Zamani tulizoea kutoa sadaka tu kila tunapokutana katika jumuiya hizi zetu na sadaka hizo hupelekwa kanisani.
Lakini siku hizi mambo tofauti michango imekuwa mingi mno tena michango hiyo huanzia elfu kumi kwa kila kichwa.
Mfano, sisi katika jumuiya yetu msalaba ukilala kwako yani siku jumuiya ikisali kwako unatakiwa utoe shilingi elfu kumi, sadaka iliyopangwa kutolewa kila Jumamosi ni shilingi elfu moja na mia tano kila kichwa, pia kuna mchango wa ujenzi wa kanisa kila mtu elfu 30.
Kuna mchango wa familia ya mtoto Yesu kila mmoja anatakiwa kutoa elfu kumi ili tuitimize laki tatu kwa kila jumuiya, mbali na hiyo kunakuwa na bahasha ya zaka zinakuwepo.
Yaani kwa kifupi kila wiki tunaposali kunakuwa na michango karibu 8 na yote inaanzia elfu kumi.
Tatizo linakuja usipolipa hiyo hela jumuiya inakutenga hadi ulipe madeni yote ndIo unaruhusiwa tena kuingia kwenye jumuiya. Kwa sasa jumuiya yetu imevunjika kwa ajili ya michango kuwa mingi ukizingatia hali halisi ya maisha ya sasa.
Kweli wakristo wenzangu hapa ndipo tulipofikia? Tunaelekea wapi kanisa katoliki la leo?!