Jumuiya ya wazazi CCM Kahama, mlichofanya kwa walimu hawa ni unyama

monjozee

Senior Member
Sep 19, 2016
115
297
UONGOZI WA JUMUIYA YA WAZAZI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) WILAYA YA KAHAMA,MLICHOKIFANYA KWA WALIMU HAWA NI UNYAMA WA HALI YA JUU.

Itakumbukwa kwamba mwezi wa pili mwaka huu niliwahi kuandika hapa kuhusu malalamiko ya Walimu wa Shule ya Sekondari WIGEHE, iliyopo wilayani Kahama inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi wa CCM Wilaya ya Kahama.

Uongozi wa shule hiyo tangu mwezi November mwaka jana (2016), haukuwahi kuwalipa mishahara walimu wa shule hii mpaka hivi sasa ninanvyoandika,pamoja na kufanyika kwa jitihada mbalimbali za walimu kufanyika,pamoja na migomo ya Wanafunzi waliokuwa wakishinikiza walimu wao walipwe pesa zao ili waendelee kufundisha.

Kwa bahati mbaya sana,walimu walioonesha juhudi za kudai fedha zao, wamekuwa wakifikishwa mara kadhaa polisi huku wakilala central kwa siku moja mpaka mbili na uongozi wa shule hiyo ya CCM ukiwatuhumu kufanya "uchochezi" shuleni hapo.Walimu hao wamekuwa wakitoka polisi kwa kujidhamini wenyewe.

Kuna baadhi ya walimu kufikia mwezi April mwaka huu, waliamua kuandika barua za kuacha kazi kutokana na dhiki waliyoipata katika kudai haki zao za mishahara, licha ya kuwa barua zao hazikuwahi kujibiwa (mpaka kufikia May 7,mwaka huu).

Siku ya May 7 mwaka huu, bodi ya Shule hiyo inayomilikiwa na CCM,katika kikao chake kilichofanyika katika ofisi za CCM (W), iliamua kuwafukuza shule baadhi ya walimu hao walioonekana kudai fedha zao, huku wale pia walioandika barua wakiomba kuacha kazi wakipewa "notice" ya kukabidhi Nyumba na kuondoka maeneo ya shule kufikia May 10 (leo), bila kupewa hata senti moja.

Kwa mujibu wa maelezo ya miongoni mwa Walimu waliofukuzwa kazi, amesema jumla ya waliofukuzwa ni walimu wanne (04), huku kila mmoja akiidai shule hiyo fedha zisizopungua shilingi mil.1, lakini wameambiwa watoke nje ya maeneo, watadai wakiwa nje.
Licha ya kulipwa mishahara midogo sana,ambapo Basic Salary ni Tsh.350,000/= huku, Take Home ikiwa Tsh.295,000/=

[HASHTAG]#Mytake[/HASHTAG]; huu ni uonevu mkubwa na muendelezo wa serikali hii na chama chake cha CCM,kuendelea kuwakandamiza na kuwatumikisha Watumishi kama Watumwa,pasipo kuwalipa stahiki zao.

Fikiria unamfukuza mtu kazi, tena kwa kuvunja mkataba, halafu unampa siku mbili atoke kwenye nyumba aliyokuwa anakaa (mtu na familia yake), wakataabike huko mitaani kutafuta sehemu za kujistili kisa tu wamedai fedha zao!!
Huu ni ukatili usiovumilika,tena unaokiuka sheria na kanuni za watumishi katika nchi hii.
Nawashauri Walimu hawa wakaitafute haki yao kwenye chombo cha sheria (Mahakama),ambapo tunaamini kuwa kwa mujibu wa sheria watasikilizwa pengine watafanikiwa kuipata haki yao.

Joseph Mohonia Politician
 
CCM Mbona kuna mambo mengine mnafanya ni unyama sana,huu sio ubinadamu nyie binadamu gani msio na huruma hata kidogo!!!!!!!
Ni kwamba mmelewa madaraka kiasi hicho cha kufika uko kuwa wanyama kiasi hicho hao walimu wangekuwa ni watoto wenu mngewafanyia hayo mnataka kupandikiza roho za ajabu sana mki ambiwa amuishi kuongea kelele nyingi ugomvi au ishi nyie mna nini?
Viongozi gani mmekaria kugombana na mnao waongoza kila siku atukatai changamoto zipo kupishana kupo ila mnapishana kwa masirahi ya nani ya nchi ya wananchi au ya kwenu,kama mmeshindwa kueni wazi watu wawasaidie la kufanya sio kulazimisha na kupingana na ukweli.
Kaeni mkijua muda utaongea tu na akuna lenye mwanzo lisilo na mwisho
 
CCM ni walaghai...Kama wamemgeuka mpiga zumari wao wa kipindi cha kampeni za uchaguzi ambaye ni Diamond kwa kumdai kodi ya jumla ya Tsh. 400,000,000 wakati anachoingiza ni chini ya mil 600, itakuwaje kwa hao walimu ambao hata Katibu wao wa Itikadi na Uenezi (Humphrey Polepole) hawajui?
 
Huu uzi unaweza kuchangia kwa mapovu kisa tu unahusu CCM, lakini ungepata taarifa ya upande wa pili ungeweza kushangaa!
 
MBONA WAMEZOEA KUFANYA UANIMOL,LEO TUNASHANGAA NINI?HAKUNI MTANZANIA WA KAWAIDA ATAKAYEPATA HAKI CHINI YA GUDUDU HUGU GU CCM.
 
Na kwao hii hawawezi kuiona ni dhambi kabisa kwani kama nidhambi wamefanya nyingi sana hadi zile za kukufuru!.
 
CCM wameua wazee na vijana wasio na hatia kwa presha,mawazo,kudhulumu,kubambikia kesi na hata kupora kisicho chao
 
Back
Top Bottom