Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,242
- 34,917
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tarehe 12-09-2016
Ndugu wanahabari,
Napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutukutanisha sisi wanajumuiya wa vyuo vikuu - CUF tawi la Mlimani (UDSM) na nyinyi wanahabari, lakini pia napenda kuwashukuru kwa kuitikia wito wetu, nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya ya kutupasha habari mbalimbali zinazohusiana na hali ya kisiasa inavyoendelea nchini. Lakini pia kuwapa pole kutokana na namna mnavyotekeleza majukumu yenu katika mazingira magumu ya hofu na vitisho vinavyofanywa na watendaji wa serikali ya awamu ya tano, tunaomba muendelee na moyo huo kwa maslahi mapana ya taifa letu.
Ndugu wanahabari,
Tumewaiteni kuzungumza na nyinyi ili mtufikishie taarifa yetu kwa wana-CUF na watanzania kiujumla dhidi ya mambo yafuatayo:-
1. Kuunga mkono maamuzi ya baraza kuu la CUF ya tarehe 28-08-2016.
2. Kulaani kauli za ubaguzi na vurugu zinazolenga kuvuruga chama zinazofanywa na Prof. Ibrahim Lipumba.
I. KUUNGA MKONO MAAMUZI YA BARAZA KUU
Ndugu wanahabari,
Mnamo tarehe 28-08-2016 Baraza kuu la CUF lilikutana Zanzibar na kufikia maamuzi ya kuweza kuwavua uongozi aliyekuwa Naibu katibu mkuu bara Mh. Magdalena Sakaya(MB) na Naibu Mkurugenzi wa habari na uenezi Mh Abdul Kambaya, lakini pia baraza kuu lilichukua uamuzi wa kusimamisha uwanachama viongozi hao pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahimu Lipumba, Mbunge wa Mtwara Mjini Mh. Maftaha Nachuma na wanachama wengine huku katibu mtendaji wa Jumuiya ya wazee Taifa mh Shashu Lugeye akivuliwa uwanachama. Kitendo hicho kinaonesha kuwa CUF ni taasisi inayoendeshwa kwa mujibu wa katiba na Sheria wala si fikra na matakwa ya mtu binafsi.
Tunaliomba baraza kuu na mamlaka nyingine ndani ya chama kuendelea kufanya maamuzi magumu ya kukijenga chama pale inapobidi kwani misingi na taratibu za chama lazima zifuatwe (kwa mujibu wa katiba ya cuf ya 1992 toleo la 2014 ibara 9(1)).
II. KULAANI KAULI ZA UBAGUZI NA VURUGU ZINAZOLENGA KUVURUGA CHAMA ZINAZOFANYWA NA PROF. IBRAHIM LIPUMBA.
Ndugu wanahabari,
Ikumbukwe kwamba Prof. Lipumba alikuwa mwenyekiti wa CUF kwa mujibu wa katiba ibara ya 91(1), na kwa kuheshimu na kutambua umuhimu wa katiba Prof. Lipumba aliweza kutumia katiba ya chama ibara 117(1) inayompa uhuru kiongozi yoyote kujiudhuru wadhifa wake na yeye alifanya hivyo kama katiba inavyoelekeza. Pia ibara 117(2) inaelekeza kiongozi wowote atakayejiuzulu lazima barua yake ipelekwe kwenye mamlaka iliyomteua au kumchagua ili kukubali au kukataa kujiuzulu kwake na ndivyo ilivyokuwa katika mkutano mkuu uliofanyika tarehe 21-08-2016 Blue Peal Hotel na kukubali kujiuzulu kwake.
Ndugu wanahabari, katiba hii ndio iliyomuweka madarakani kwa muda wote Prof Lipumba na ndiyo iliyompa yeye haki ya kujiuzulu na ndio inayoelekeza namna gani ya kuwapata viongozi ndani ya chama kwa ngazi zote, pia ibara 9(1) inaelekeza kuwa mtu yoyote anayehitaji kuwa mwanachama lazima afuate utaratibu na maamuzi halali ya chama. Kutokana na kauli na fujo zinazofanywa na Prof.Lipumba na kikundi chake za kupinga maamuzi halali ya chama ni wazi kabisa kuwa Prof Lipumba hana nia njema na CUF, bali anania ya kukigawa chama.
Ndugu wanahabari,
Kutokana na hali hii Jumuiya ya vyuo vikuu CUF Tawi la Mlimani(UDSM) linalaani vikali fujo na kauli za kibaguzi zinazoendelea kutolewa na Prof. Lipumba na baadhi ya wafuasi wake kama ile iliyotolewa na aliyekuwa naibu katibu mkuu Mh. Magdalena Sakaya kuwa chama kina mpasuko wa bara na visiwani kama alivyonukuliwa katika moja ya magazati hapa nchini.
HITIMISHO
Ndugu wanahabri,
Chama cha wanachi CUF Mlimani ikiwa sehemu ya wanazuoni tunapenda kumshauri Prof. Lipumba kuachana na mpango wake wa kuvuruga chama kwani kinachoendelea anajidhalilisha na kujishushia heshima aliyojijengea miaka mingi katika jamii ndani na nje ya nchi.
Kuendelea kufanya hivyo sio tu anajidhalilisha au kujifedhehesha pekee bali anaidhalilisha jamii nzima ya wasomi wenye hadhi kama yeye. Inasikitisha sana kuona mtu kama Prof.Lipumba aliewahi kushika wadhifa wa uenyekiti wa chama Taifa kuwa leo eeti!! Anakuwa mstari wa mbele kukivuruga na kukigawa chama.Tunamtaka Prof.Lipumba aheshimu maamuzi halali ya chama na afuate katiba kwa maslahi ya chama na siyo kwa maslahi yake binafsi.
Wito kwa wanachama.
Tunatoa wito kwa wanachama kuwa hivi sasa ni muda wa kujenga chama na kujipanga kuelekea kwenye changuzi za serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu 2020 na kuachana na propaganda zinazofanywa na maasimu wetu kutugawa.
Ahsanteni,
Jidawi Chande
Mwenyekiti
Jumuiya ya vyuo vikuu CUF Tawi la Mlimani