Jumuia ya Wazanzibar Canada yatowa Logo Mpya.

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=3]Zacadia yatambulisha Logo mpya[/h]


Asalaam alaikoum Wazanzibari wote popte walipo duniani.

Kwa niaba ya Interim President na Katibu wa Zanzibar-Canadia Diaspora Association, chini ya usajili rasmi katika serikali ya Ontario kama Zacadia Foundation, nachukuwa fursa hii kuiwasilisha na kuitambulisha LOGO yetu mpya ya Jumuia yetu hapa Toronto na Canada kwa jumla.

Baada ya proposal mbali mbali zilizofanywa na kufanyiwa uhakiki, kwa msaada wa ndugu yetu ambaye ni msanii wa mambo ya Graphic, hatimaye nimeweza kufanya Logo hii ambayo itatumika rasmi kama alama ya Zanzibar-Canadian Diaspora Association (ZACADIA) na Zacadia Foundation.

Baada ya mafanikio hayo, htauna budi kutoa shukrani zetu za dhati kwa msanii wetu huyu, ndgu Mohammed Khamis kwa kazi yake nzuri, kwa kushirikiana na mmoja wa volunteer wa ZACADIA hata kufikia kupatikana kwa logo hii ambayo tunahisi ni nzuri zaidi ya zile za nyuma.

Wakati huo huo, tunapenda kuwaarifu Wazanzibari wote duniani kwamba, ZACADIA Foundation imebuni mradi wa kijamii kwa ajili ya kuwasaidia watoto mayatima na masikini wa vijijini Unguja na Pemba kwa kuwapatia nyenzo muhimu za maisha kama vile nguo, chakula, vifaa vya skuli usafiri kwa wale walio mbali na skuli kama baiskeli pamoja na huduma za kuangaliwa kiafya.
Mradi huu umekusudiwa kuwashirikisha Wazanzibari walio nje na ndani ya Zanzibar kwa kuchangia kwa njia moja au nyengine katika kufanikisha kuwasaidia watoto hao ambao tayari tunao kumi kwa sasa, watano kutoka kila kisiwa, Unguja na Pemba.

Mbali na michango mbali mbali ya kawaida, ZACADIA imekusudia kuwatafuta wadhamini wa watoto hao kila mmoja mtoto mmoja au zaidi ya mtu mmoja kumdhamini mtoto mmoja kwa kutoa mchango wa dola 30 kwa mwezi ili kudhamini motto kufaniksha kupatiwa huduma hizo tulizozitaja hapo juu.

Pamoja na Sponsorship hiyo, ZACADIA itafanya juhudi ya kutafuta fedha zaidi ili kuongezea kuwahudumia watoto hao kumi wa kuanzia mpaka motto huyo atakapomaliza sekondari.

Ikiwa wakiristo wanatoa misaada kama hii kwa watoto wa wenzao katika nchi zinazoendelea, kwa nini sisi Wazanzibari tushindwe kuwasaidia watoto wetu wenyewe kwa kupitia njia kama hizo ambazo ZACADIA inataka kuzianzisha kwa jamii za Wazanzibari.

Kwa wle ambao watakuwa tayari kuanza kutoa michango yao kwa ajili ya mradi huu, watuandikie infozacadia@gmail.com ili tuanze kutayarisha mipango kabambe ya namna ya kutuma michango yao kwa njia ya salama kupitia PayPal. Mpango mzaima umi mbioni kutayarishwa ili kukamilisha website ambayo itarahisisha Mradi huu kuanza na wachangiaji kuweza kusaidia.

Nimeshuhudia Wazanzibari wakitoa dola 30 kila mwezi kupitia World Vision ili ku sponsor mtoto. Sasa tushirikiane sisi wenyewe tuweze kuufanikisha mradi huu kwa ajili ya watoto wetu ambao hawajawahi kupatiwa misaada ya aina hii ambayo huishia Tanganyika.

Ni matumaini yetu kwamba Wazanzibari, pamoja na marafiki zao, watautangaza mradi huu na watajitokeza kwa wingi kuchangia na ku sponsor watoto hawa kumi tulionao kwa sasa.

ZACADIA inakusudia kumuunganisha mtoto Nairat katika mradi huu mara mipango itakapokamilika.

ZACADIA inatoa shukrani kwa wale Wazanzibari waishio Toronto na viunga vyake (GTA) kwa michango yao ambayo waliitikia wito wa wa ZACADIA katika kumchangia NAIRAT na dada yake Bisambe ili waokolowe kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu kutokana na maradhi yaliyowakumba.

Mwisho, hatuna budi kutoa shukrani kwa ndugu Othman Maulid na Blog yake ya ZANZINEWS, Bi. Salma Said na uongozi wa MZALENDO.NET kwa juhudi zao walizozifanya katika kuwaelimisha na kuwapa taarifa mbali mbali za Wazanzibari duniani kote.

Nwasilisha kwa niaba ya:

President na Katibu

ZACADIA





Imewekwa na MAPARA at 6:06 PM
 
Zanzibari-Canadians (note, not Zanzibar-Canadian, which is a meaningless mongrel in the context of a diaspora organization's name, mnakaa nchi za watu hata lugha hamjifunzi?) si Wazanzibar Canada, ni Wacanada wenye asili ya Zanzibar.

Natumaini mshachukua uraia, kwa sababu kama hamjachukua si Canadians, na hamuwezi kuwa Zanzibari-Canadians kama si Canadians.

Mambo madogo lakini muhimu.
 
Naona KARAFUU imepakatwa na MAPLE LEAF..........no wonder


image01.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom