Jumla ya watu 329 wapoteza maisha kutokana na kipindupindu tangia Agosti mwaka jana

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Wagonjwa wapatao 20,882 wamebainika kuwa na ugonjwa wa kipindupindu huku kati yao 329 wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo nchini Tanzania tangu kuripotiwa kwa ugonjwa huo mwezi Agosti mwaka jana.

Akitoa taarifa ya wiki ya ugonjwa huo nchini Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto nchini Tanzania, Mhe. Ummy Mwalimu amesema kwa sasa kasi ya ugonjwa huo imeendelea kupungua ambapo wagonjwa wapya waliobainika wiki iliyopita ni 212 ikilinganishwa na 368 wa wiki iliyotangulia.

Mhe. Ummy amesema mikoa ya Morogoro, Mara, Kilimanjaro, Pwani na Tanga bado ni miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi pamoja na halmashauri za Tarime Mjini Mvomero na Kinondoni zikiwa bado na wagonjwa wengi.

Aidha taarifa hiyo ya Waziri imeitaja mikoa ambayo bado imeendelea kuripoti ugonjwa wa kipindupindu ni 10 ambapo mikoa iliyopata wagonjwa wengi zaidi ni Morogoro (wagonjwa 51 na Kifo 1), Mara (45), Kilimanjaro (31), Pwani (24), na Tanga (24). Aidha hakuna Mkoa mpya uliotoa taarifa ya kuwepo kwa wagonjwa wa Kipindupindu.

Pia katika wiki hii halmashauri zilizoongoza kuwa na wagonjwa wengi ni Morogoro vijijini (23), Same (20), Tarime mjini (20), Mvomero (wagonjwa 18, na Kifo 1) na Kinondoni (16). Vile vile, katika wiki hii Mikoa ambayo haijapata mgonjwa wa Kipindupindu ni Kigoma, Dodoma, Singida, Shinyanga, Tabora, Lindi, Kagera, Rukwa, Katavi, Mbeya, Simiyu, Iringa na Mtwara.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Mohamed Bakari Kambi amesema imani potofu miongoni mwa wananchi zinachangia kuendelea kuwepo kwa ugonjwa huo nchini.
 
Back
Top Bottom