JUMIA Tanzania huduma tata

JUMIA Tanzania huduma tata

kichema

Senior Member
Joined
Mar 31, 2015
Posts
137
Reaction score
39
Ndugu, tukiwa tunaingia ulimwengu wa kidigitali si kwa pesa na mitandao tu, ni pamoja na huduma za kijamii na kibihashara.
Napenda kuwajuza ndugu zetu wa Jumia kuwa wakati wanaendelea kutoa huduma ni bora wakajipanga kwa kuhakikisha wanatupatia bidhaa zinazokidhi matakwa ya ubora si bora bidhaa peleka.
Unapompatia bidhaa yako mteja wako, akikwambia umenipatia bidhaa mbovu, husimlazimishe kukaa nayo au kununua tena bidhaa kupitia kwako. Mlipe hela zake na atafute ufumbuzi mwingine.
Nawapa mfano wa eBay. ukinunua bidhaa kwao na ukalipa kupitia Visa Card au master Card au njia yoyote hile inayokubalika kimtandao, ukisha pokea bidhaa na hujalidhika nayo ni ndani ya saa 24 hela yako inarudi. Jumia mnamlazimisha mteja kununua bidhaa nyingine ambayo hana shida nayo.
Na kwasababu hiyo hiyo mnaogopa kuwaelekeza wateja wenu ofisi zenu zinakopatikana kwani mnajua mnaweza kupigwa.
Je, mnatuambia nini kuhusu hili........
Kumbuka kuna mkataba wa walaji,
Kumbuka TFDA
Kumbuka kuna mamlaka ya ushindani wa kibihashara
 
Back
Top Bottom