Jumba bovu linaweza kumuangukia mtu yeyote

General mex

Senior Member
May 1, 2011
158
185
Sio kila mtu anaweza kuwa na uelewa wa masuala yote, unaweza kufanya jambo kwa nje likaonekana zuri sana ila kwa ndani kumbe lina shida kubwa. Unaweza kufanya jambo lenye matokeo chanya au hasi kwa siku za usoni ila kumbe kwa siku za baadae likawa na matokeo tofauti.

nitajikita kwenye kutoa ushauri kwa serikali ya sita ya kipindi cha awamu ya tano. Yamkini kuna mambo mengi ambayo ni mazuri yamefanywa na serikali ya tano, kuna mengine kwa siku za usoni yanapendeza na kuonesha matumaini, ila ni muhimu kuangalia mambo yote hayo na kuyapima kwa siku za mbeleyatakuwa na matokeo gani.

Suala la shirika la ndege linafungua macho, tunapenda sana kuwa na ndege zetu na ni fahari ila ni muhimu kuangalia kwa muda mrefu itakua ni faida au ni hasara.

Kuna mambo mengi yanaweza kufanyika wataalamu wapo na wakipewa nafasi ya kutumia utaalamu wao pasipo kuambiwa matokeo yanayotakiwa wanaweza kutoa ushauri mzuri na tukasonga mbele.

Kwa nini ni muhimu zaidi kwa serikali ya sita hii kuhakikisha mambo kama hayo yanawekwa wazi mapema? Ni kwa sababu tayari Hayati Dr. JPM amekwishatangulia mbele za haki na kizuri zaidi matokeo ambayo watu waliyatarajia wameyaona na walio wengi wameipenda kazi iliyofanyika.

Sasa itakapokuja kutokea kwamba matokeo ya kazi ya serikali ya tano yanabadilika au yanaanza kubadilika kwenye serikali ya sita ya bi mkubwa. Moja kwa moja kwa walio na uwezo wa kawaida watasema si unaona kazi hii alikua anaiweza mtu mmoja tuu.

Hili linapaswa kuangaliwa kwa makini sana kwa sababu kazi inaweza kufanywa na mtu mwingine ila lawama zote zikaenda kwa mtu mwingine.

Hii ipo kwenye sehemu mbalimbali kama ilivyooneshwa kwenye shirika la ndege ambalo hakuna aliweza kuwa na uhakika kua ni hasara inapatikana badala ya faida, vilevile ifanyike kwenye miradi mbalimbali, iangaliwe hela imetoka wapi na utendaji wa miradi hiyo ili kama ni ya hasara ifahamike wazi ni hivyo kuliko kuja kumlaumu mtu au watu ambao itakua ni kama kuwaonea.

Kuna mambo ya deni la taifa na vitu kama hivyo, sawa maendeleo tumeyaona ila ni muhimu kujua kama kuna mahali panatakiwa pakazwe nati ifanyike hivyo ila yote kwa yote upembuzi yakinifu ufanyike kujua hali halisi ya kila kitu.

Nimalizie kusema tena kua jumba bovu linaweza kumdondokea mtu yeyote, awe mpita njia, au jirani au hata aliyejenga kama yupo, kwa hiyo kama ikifahamika ni jumba bovu lawama zitaenda kwa mafundi na sie litakayemwangukia japo lawama haziwezi kubadili chochote kama likidondoka.
 
Hata hiyo reli ya Mwendokasi nayo itazalisha hasara tu. Maana ujenzi wake sidhani kama ulifanyiwa utafiti wowote ule wa maana.
 
Hata hiyo reli ya Mwendokasi nayo itazalisha hasara tu. Maana ujenzi wake sidhani kama ulifanyiwa utafiti wowote ule wa maana.
Kimei alisema wamefungua CRDB branch Chato kutokana na 'utafiti' uliofanywa na rais wa wakati huo.

Ikabidi nichekee tumboni tu, yaani rais anaifanyia benki utafiti wa wapi wafungue branch!! Hii awamu ilijaa vituko sana, anayepaswa kushauriwa ndio alijifanya kuwa mshauri mkuu.
 
Back
Top Bottom