nzalendo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 12,683
- 14,066
Naam katika maisha kuna kupanda na kushuka.
Sasa moja na mbili kwa wenye kuutambua mguu wa Yesu pamoja na makandokando yetu huwa tunazingatia ibada.
Kwa imani yangu binafsi kanisa ni kwa ajili ya watu aina yangu ambao si watakatifu.
Naamka alfajiri kujiandaa kwenda ''Church'' ,,,kila nguo ninayo iangalia naona imechakaa vya kutosha,,,
Naingia bafu maji nayo mtihani,,,natumia nusu ndoo,,,
Najisachi nagundua nina buku,,,sasa niitoe sadaka au niibane ili baadae ninunue japo mboga za majani nije nitoe dongo?
Huku na kule naona hili buku ngoja nilibane manake kuamka na kwenda church ni sadaka tosha Mungu anaona moyo,
Chap kwa haraka nakaribia kuingia nyumba ya ibada kila ninaye msabahi naona kama ananikataa au kunikwepa labda kwa muonekano wa kuchoka pia mavazi,,
Naingia ndani ibada inaendelea Muhubiri anatoa neno.....ambalo kimsingi linanifariji na kusikia nguvu fulani ndani yangu na kunipa muamko kwamba one day YES..Yesu atasaidia.
Muda wa kutoa sadaka unafika watu wananyanyuka benchi kwa benchi kwenda mbele kutoa sadaka,,,sasa mie sina kitu,,nawapisha waungwana wanakwenda mbele,,,najikuta peke yangu kwenye benchi,,..
Unafika muda wa kutoka ibadani nje kuna mnada unaendelea,,,watu wameleta vyakula mbali mbali vinapigwa mnada...kuku ameuzwa laki....mie nyumbani nikila leo kesho sijui nitakula nini...mwingine kanunua viazi kama debe moja hivi kwa elfu sabini,,,ni vizuri ni sadaka,,,lakini wengi tuna njaa na kanisa halina utaratibu angalau wa siri wa kuwajulia waumini wake nini kinawasibu hasa njaa,,,,,
Mnada unakwisha watu wanaingia kwenye magari yao..... najaribu kuangalia wale wanaoelekea mtaani kwetu angalau niombe lifti,,, naona kabisa wananikwepa waziwazi,,,,na wote tulikuwa tunasali pamoja.
Nashukuru Mungu najikongoja tartiibu naingia kona ya kwanza ya pili nanunua mboga .....kufika home kumbe mkaa umeisha,,naenda kukopa kumbe pale nina deni,,,,,naenda sehemu nyingine wananielewa.....
Najipikia,,,,,,baada ya kula nachukua mkeka naenda kivulini halafu nasikiliza wimbo huu,,,,,,
View: https://youtu.be/cnEdbTqAAJo?si=WhBpl2FMePFJjADl