ANGUKO LA UCHUMI KWA TAIFA LA MAREKANI (1929~1933)
Aliyeitwa Herbert hoover aliyekuwa na miezi nane tu kwenye uongozi wake kutokana na kutokujuwa vema nini maana ya urais wa marekani uchumi ukaanguka, siku ambayo wao waliyoitaja kama jumanne nyeusi hali ilikuwa mbaya zaidi 0.75 walipoteza ajira.
Sababu kubwa ya Herbert Hoover kushindwa ni kufa kwa ununuzi wa hisa (New york stock exchange) ambayo ilipelekea watu kuchukuwa pesa zao kwenye mabenki na kufirisika kitendo ambacho kilipelekea wamerikani kumkataa rais HERBERT HOOVER.
Utawala wa herbert hoover ni wazi mambo yalionekana kuwa mabaya katika maeneo mengi muhimu kwa uchumi wa Marekani. Ni wamarekani ndio waliyofahamu kuwa Hoover mambo kwake alikuwa mabaya lakini kwa Tanzania mambo tofauti sio kama watu makini hawapo la, ni wajinga wengi sana kuliko watu makini na ndio sababu kubwa ambayo CCM wanayotumia.
Rais Herbert Hoover.
Mwaka 1929 akaja mkombozi wa uchumi wa marekani rais Franklin Delano Roosevelt na kauli yake "The only thing we have to fear is fear itself".
Mipango madhubuti ya rais Franklin delano roosevelt baada ya kuwa rais mwaka 1929
1. Nafuu(Relief): Alitoa pesa kusaidia wazee wasio na ajira.
2. Akafanya mabadiliko katika sector tofauti tofauti miongoni ni mabenk akazipa mitaji ili kurejesha matumaini kwa wananchi kutunza hela zao kwenye mabenk.
3. Rais franklin alitoa ajira kwa vijana.
4. Kutengeneza uhusiano mzuri wa wafanya kazi na waajiri wao ili kuteta ufanisi wa kazi hatimae marekani ikawa kubwa tena kwa uchumi.
The only thing we have to fear is fear itself.
It is common sense to take a method and try it. If it fails, admit it frankly and try another. But above all, try something.
RAIS JOHN POMBE MAGUFULI.
Utawala wa rais John Pombe Magufuli una zaidi ya mwaka moja na miezi kadhaa madarakani. Kama taifa, hatuwezi kuendelea na fungate (honeymoon) ya utawala wake wakati ni wazi mambo yanaonekana kuwa mabaya katika maeneo mengi muhimu kwa uchumi wa Tanzania.
Ufike wakati sasa tuanze kizungumzia mambo mazito yanayotukabili kama taifa.
Magufuli atambue kuwa hata Mungu mwenyewe alianza na mwanga
"Mungu akasema, iwe nuru, ikawa nuru. Mungu akaiona nuru na giza. Mungu akaiita nuru mchana, na giza akaiita usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya kwanza"
Ni maneno kutoka katika kitabu cha mwanzo(1: 3~5)
Tunatakiwa kufikiria kwamba tunaweza kuumizwa na tunaweza kujiumiza wenyewe, Magufuli anatakiwa kuambiwa kuwa safari yake ni ngumu katika uchumi.
Note: Magufuli utashi wa kisiasa ni muhimu katika kuendesha taifa.
Mipango ya rais Herbert ni sawa na mipango ya Magufuli.
Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu.
By mr mkiki