Jumanne nyeusi kwa Rais Magufuli inakuja

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,581
11,658
ANGUKO LA UCHUMI KWA TAIFA LA MAREKANI (1929~1933)

Aliyeitwa Herbert hoover aliyekuwa na miezi nane tu kwenye uongozi wake kutokana na kutokujuwa vema nini maana ya urais wa marekani uchumi ukaanguka, siku ambayo wao waliyoitaja kama jumanne nyeusi hali ilikuwa mbaya zaidi 0.75 walipoteza ajira.

Sababu kubwa ya Herbert Hoover kushindwa ni kufa kwa ununuzi wa hisa (New york stock exchange) ambayo ilipelekea watu kuchukuwa pesa zao kwenye mabenki na kufirisika kitendo ambacho kilipelekea wamerikani kumkataa rais HERBERT HOOVER.

herbert hoover.jpg

Utawala wa herbert hoover ni wazi mambo yalionekana kuwa mabaya katika maeneo mengi muhimu kwa uchumi wa Marekani. Ni wamarekani ndio waliyofahamu kuwa Hoover mambo kwake alikuwa mabaya lakini kwa Tanzania mambo tofauti sio kama watu makini hawapo la, ni wajinga wengi sana kuliko watu makini na ndio sababu kubwa ambayo CCM wanayotumia.

heho_hoover_london_treaty_1930.jpg

Rais Herbert Hoover.

Mwaka 1929 akaja mkombozi wa uchumi wa marekani rais Franklin Delano Roosevelt na kauli yake "The only thing we have to fear is fear itself".

32_franklin_d_roosevelt.jpg

Mipango madhubuti ya rais Franklin delano roosevelt baada ya kuwa rais mwaka 1929

1. Nafuu(Relief): Alitoa pesa kusaidia wazee wasio na ajira.

2. Akafanya mabadiliko katika sector tofauti tofauti miongoni ni mabenk akazipa mitaji ili kurejesha matumaini kwa wananchi kutunza hela zao kwenye mabenk.

3. Rais franklin alitoa ajira kwa vijana.

4. Kutengeneza uhusiano mzuri wa wafanya kazi na waajiri wao ili kuteta ufanisi wa kazi hatimae marekani ikawa kubwa tena kwa uchumi.

Franklin_D_Roosevelt_Quotations.jpg

The only thing we have to fear is fear itself.

Quote-Franklin-D.-Roosevelt.png

It is common sense to take a method and try it. If it fails, admit it frankly and try another. But above all, try something.

RAIS JOHN POMBE MAGUFULI.

bot7.JPG

Utawala wa rais John Pombe Magufuli una zaidi ya mwaka moja na miezi kadhaa madarakani. Kama taifa, hatuwezi kuendelea na fungate (honeymoon) ya utawala wake wakati ni wazi mambo yanaonekana kuwa mabaya katika maeneo mengi muhimu kwa uchumi wa Tanzania.

Ufike wakati sasa tuanze kizungumzia mambo mazito yanayotukabili kama taifa.

Magufuli atambue kuwa hata Mungu mwenyewe alianza na mwanga

"Mungu akasema, iwe nuru, ikawa nuru. Mungu akaiona nuru na giza. Mungu akaiita nuru mchana, na giza akaiita usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya kwanza"

Ni maneno kutoka katika kitabu cha mwanzo(1: 3~5)

Tunatakiwa kufikiria kwamba tunaweza kuumizwa na tunaweza kujiumiza wenyewe, Magufuli anatakiwa kuambiwa kuwa safari yake ni ngumu katika uchumi.

Note: Magufuli utashi wa kisiasa ni muhimu katika kuendesha taifa.

Mipango ya rais Herbert ni sawa na mipango ya Magufuli.

Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu.

By mr mkiki
 
Attachments

  • 1966 Family Photo Bladhs 001.jpg
    1966 Family Photo Bladhs 001.jpg
    20.4 KB · Views: 368
  • Franklin-Roosevelt-Quotes.jpg
    Franklin-Roosevelt-Quotes.jpg
    9.7 KB · Views: 380
Umetumia muda mwingi kuandika mambo mengi ambayo hayana uhusiano kabisa, sasa Tanzania itakuwaje na anguko la Uchumi? Uchumi upi huo uliokuwa nao TZ mpaka ipate anguko la uchumi?

Nchi ya GDP ya chini 45 Billion (US) tu na watu zaidi ya milioni 40, halafu unaongelea anguko la uchumi kana kwamba sasa hivi kuna kupanda kwa uchumi au kumeshawahi kuwepo na Uchumi mkubwa hadi uongelee anguko la Uchumi?
 
Ulitakiwa useme ni Mambo gani unayaona hayapo vizuri kwa utawala huu.

Kwa sababu, Mishahara analipa kama kawaida, yeye anataka kodi yake tu halali ilipwe.

Labda useme kwamba, Rais alegeze masharti ya kuweka fedha kwenye Bank Binafsi ili watu na makampuni wakope, hapa Rais anaweza kukaa na jopo lake na kuandaa utaratibu mzuri wa kuzitoa Fedha BOT na kuzipeleka kwenye Mabank binafsi huku BOT ikizi-monitor lakini Bank nazo lazima zidai kwanza madeni yao toka kwa waliowakopesha.

Mimi sioni tatizo lolote juu ya Utawala wa JPM Zaidi ya kusikia malalamiko ya watu kuwa hakuna pesa mifukoni.
 
Masikini akifilisika anakuwa fukara.
 
Duh!!! Kuna watu kwa kweli hawajielewi wanasimamia wapi hasa katika suala zima la matumizi ya ubongo wao na mmoja wapo ni huyu aliye andika huu upuuzi.
 
Ulitakiwa useme ni Mambo gani unayaona hayapo vizuri kwa utawala huu.

Kwa sababu, Mishahara analipa kama kawaida, yeye anataka kodi yake tu halali ilipwe.

Labda useme kwamba, Rais alegeze masharti ya kuweka fedha kwenye Bank Binafsi ili watu na makampuni wakope, hapa Rais anaweza kukaa na jopo lake na kuandaa utaratibu mzuri wa kuzitoa Fedha BOT na kuzipeleka kwenye Mabank binafsi huku BOT ikizi-monitor lakini Bank nazo lazima zidai kwanza madeni yao toka kwa waliowakopesha.

Mimi sioni tatizo lolote juu ya Utawala wa JPM Zaidi ya kusikia malalamiko ya watu kuwa hakuna pesa mifukoni.

Ukiwa muajiriwa una uhakika wa mshahara na hautoona utofauti wowote. Kwa wafanya biashara ndio wanajua hali halisi ya uchumi.
Mfanyabiashara ndio anajua hali ya uchumi wa nchi ukoje na sio muajiriwa anaetegemea mshahara wa mwisho wa mwezi.
Nenda kariakoo ukaulize hali ya biashara ikoje ndio utajua.
 
Umetumia muda mwingi kuandika mambo mengi ambayo hayana uhusiano kabisa, sasa Tanzania itakuwaje na anguko la Uchumi? Uchumi upi huo uliokuwa nao TZ mpaka ipate anguko la uchumi?

Nchi ya GDP ya chini 45 Billion (US) tu na watu zaidi ya milioni 40, halafu unaongelea anguko la uchumi kana kwamba sasa hivi kuna kupanda kwa uchumi au kumeshawahi kuwepo na Uchumi mkubwa hadi uongelee anguko la Uchumi?
Hana akili vipi...???
Acha kutumia lugha za maudhi...mbona jamaa katiririka vizuri acha wivu na uvivu wa kufikiri... Suala la uchumi kushuka/kupanda ni la kutafakari binafsi sio kusingizia GDP....
Wajinga ni wengi na watu makini ni wachache.. Suala la kushuka au kupanda kwa uchumi ni kujumlisha/kutoa na kulinganisha tuu sio mpaka mzungu aje akufundishe ndo uelewe.. Ndo maana jambo la msingi ww unaleta mzaha...
 
Kumlinganisha Rais Hoover na kuanguka kwa uchumi wakati wa kipindi chake na Rais Magufuli katika kipindi chake hiki cha kurekebisha uchumi ni kutoitendea haki historia.

Nina mashaka inawezekana mtoa post hukusoma somo la Historia katika elimu yako. Kama ungelisoma, ungelijua sababu za kuanguka uchumi enzi za Hoover.

Vilevile, ungelijua na kuoanisha hatua alizochukua Rais Roosevelt kupitia kauli mbiu yake ya 'NEW DEAL' kufufua uchumi zinafanana na za Rais Magufuli kupitia kauli mbiu yake ya 'HAPA KAZI TU'.
 
Hashim Rungwe : "Tatizo la Rais ni kuonyesha tabia zake kuliko utendaji wake, kuna mambo ambayo anatakiwa kuyafanya na familia yake au rafiki zake yeye anayafanya kwenye taasisi ya Urais"
Sitashangaa kuwa wewe ni mmoja wa wanaomuunga mkono Trump, au siyo?
 
Hii ni analogy nzuri sana. Kuweka kumbukumbu sawa ni kwamba Rais Rooservelt aliingia madarakani mwaka 1933.

Rais Rooservelt ndiye alikuwa muasisi wa utaratibu wa tathmini ya siku 100 za rais kukaa madarakani. Katika siku zake 100 madarakani, Rooservelt alipeleka miswada 13 ya sheria bungeni.

Mabadiliko makubwa aliyoyasimamia Rooservelt aliyapa jina "The new deal", ikiwa ni pamoja na kuachana na sera za uchumi zilizotokana na nadharia za Adam Smith (Classical Economic Theory) ambazo zilikiwa zinajali tu matajiri na wawekezaji na akakumbatia nadharia za kiuchimi za John Keynes zilizosisitiza serikali kuratibu shughuli za kiuchumi ili manufaa ya kustawi kwa uchumi yawanufaishe wote.

Ni wakati wa urais wa Rooservelt ndipo taasisi imara za kiuchumi (kama CMSA, FCC, nk) zolipoanzishwa huko Marekani na kuliwezesha hili taifa kuwa kinara duniani kiuchumi.

Haya yaliwezekana kwa Rooservelt kwa kuwa alikuwa na muongozo wa imani ya kiikadi kisiasa, pamoja na mrengo wa kiuchumi, ambavyo vilimpa dira ya kufanya aliyoyafanya na kufanikiwa.

Hizi sifa Magufuli hana. Ni vyema akatumia zaidi washauri wake wa kiuchimi na kuachana na kutafuta umaarufu. Awe strategist zaidi.
 
Similar Discussions

64 Reactions
Reply
Back
Top Bottom