Jumanne nyeusi kwa Rais Magufuli inakuja

Umetumia muda mwingi kuandika mambo mengi ambayo hayana uhusiano kabisa, sasa Tanzania itakuwaje na anguko la Uchumi? Uchumi upi huo uliokuwa nao TZ mpaka ipate anguko la uchumi?

Nchi ya GDP ya chini 45 Billion (US) tu na watu zaidi ya milioni 40, halafu unaongelea anguko la uchumi kana kwamba sasa hivi kuna kupanda kwa uchumi au kumeshawahi kuwepo na Uchumi mkubwa hadi uongelee anguko la Uchumi?
1. Kwahiyo na wewe unakiri kwamba miaka 50 yote toka tupate "uhuru" chini ya CCM na uongozi wake hatuna uchumi.?
2. Na je, kumbe anayokuwa anaongea Beno Nduru, ni kuruka sarakasi tu, hatuna uchumi wowote?
3. Kwa uelewa wako, ili uchumi upande inatakiwa iweje, na ili uchumi ishuke inakuwaje pia?
 
... "We are the people of America was no thing to fear the fear is its self am care of it"...
By mr mkiki
Hicho ni Kiingereza cha bwana mkiki mkiki. Tafadhali nenda kahakiki vyeti vyako badala ya kushinda mtandaoni na kuandika pumba.
 
Ulitakiwa useme ni Mambo gani unayaona hayapo vizuri kwa utawala huu.

Kwa sababu, Mishahara analipa kama kawaida, yeye anataka kodi yake tu halali ilipwe.

Labda useme kwamba, Rais alegeze masharti ya kuweka fedha kwenye Bank Binafsi ili watu na makampuni wakope, hapa Rais anaweza kukaa na jopo lake na kuandaa utaratibu mzuri wa kuzitoa Fedha BOT na kuzipeleka kwenye Mabank binafsi huku BOT ikizi-monitor lakini Bank nazo lazima zidai kwanza madeni yao toka kwa waliowakopesha.

Mimi sioni tatizo lolote juu ya Utawala wa JPM Zaidi ya kusikia malalamiko ya watu kuwa hakuna pesa mifukoni.
hapa unaonekana unajua tatizo lilipo kwamba fedha za serikali ikikubalika kuwekwa katika mabenki binafsi kuwe na uangalizi mkubwa sana ,bot isimamie hili kwa macho makali ,benki zisiachiwe hizi pesa kana kwamba hakuna msimamizi .riba inayopatikana BOT Wajue ili iingizwe kwenye kumbukumbu za serikali,mi naamini benki zina mitaji ya kutosha
 
Umetumia muda mwingi kuandika mambo mengi ambayo hayana uhusiano kabisa, sasa Tanzania itakuwaje na anguko la Uchumi? Uchumi upi huo uliokuwa nao TZ mpaka ipate anguko la uchumi?

Nchi ya GDP ya chini 45 Billion (US) tu na watu zaidi ya milioni 40, halafu unaongelea anguko la uchumi kana kwamba sasa hivi kuna kupanda kwa uchumi au kumeshawahi kuwepo na Uchumi mkubwa hadi uongelee anguko la Uchumi?
Acha upoyoyo..!jibu kwa hoja zenye mantiki.
 
Umetumia muda mwingi kuandika mambo mengi ambayo hayana uhusiano kabisa, sasa Tanzania itakuwaje na anguko la Uchumi? Uchumi upi huo uliokuwa nao TZ mpaka ipate anguko la uchumi?

Nchi ya GDP ya chini 45 Billion (US) tu na watu zaidi ya milioni 40, halafu unaongelea anguko la uchumi kana kwamba sasa hivi kuna kupanda kwa uchumi au kumeshawahi kuwepo na Uchumi mkubwa hadi uongelee anguko la Uchumi?
KAMA HUJUI NI BUSARA KUKAA KIMYA MKUU. MDORORO WA UCHUMI SIO LAZIMA UKIDHI VIGEZO VYAKO JUST LOOK WHAT IS HAPPENING IN ZIMBABWE....
 
Kila shetani na mbuyu wake. Inawezekana huyo brgdiere ni miongoni mwa wale wanaomlinda log me in kwahiyo anao mshiko mzuri tu kutoka kwa Mr xstd7 shoe shiner v trump
 
Binafsi naiona point ya msingi sana hapa. Either mkuu wa nchi hajui gharama ya anachokifanya au anafanya kwa kujua na anazitaka hizo cost.
 
ANGUKO LA UCHUMI KWA TAIFA LA MAREKANI (1929~1933)

Aliyeitwa Herbert hoover aliyekuwa na miezi nane tu kwenye uongozi wake kutokana na kutokujuwa vema nini maana ya urais wa marekani uchumi ukaanguka, siku ambayo wao waliyoitaja kama jumanne nyeusi hali ilikuwa mbaya zaidi 0.75 walipoteza ajira.

Sababu kubwa ya Herbert Hoover kushindwa ni kufa kwa ununuzi wa hisa (New york stock exchange) ambayo ilipelekea watu kuchukuwa pesa zao kwenye mabenki na kufirisika kitendo ambacho kilipelekea wamerikani kumkataa rais HERBERT HOOVER.

View attachment 441037
Utawala wa herbert hoover ni wazi mambo yalionekana kuwa mabaya katika maeneo mengi muhimu kwa uchumi wa Marekani. Ni wamarekani ndio waliyofahamu kuwa Hoover mambo kwake alikuwa mabaya lakini kwa Tanzania mambo tofauti sio kama watu makini hawapo la, ni wajinga wengi sana kuliko watu makini na ndio sababu kubwa ambayo CCM wanayotumia.

View attachment 441038
Rais Herbert Hoover.

Mwaka 1929 akaja mkombozi wa uchumi wa marekani rais Franklin Delano Roosevelt na kauli yake "The only thing we have to fear is fear itself".

View attachment 441043

Mipango madhubuti ya rais Franklin delano roosevelt baada ya kuwa rais mwaka 1929

1. Nafuu(Relief): Alitoa pesa kusaidia wazee wasio na ajira.

2. Akafanya mabadiliko katika sector tofauti tofauti miongoni ni mabenk akazipa mitaji ili kurejesha matumaini kwa wananchi kutunza hela zao kwenye mabenk.

3. Rais franklin alitoa ajira kwa vijana.

4. Kutengeneza uhusiano mzuri wa wafanya kazi na waajiri wao ili kuteta ufanisi wa kazi hatimae marekani ikawa kubwa tena kwa uchumi.

View attachment 441059
The only thing we have to fear is fear itself.

View attachment 441060
It is common sense to take a method and try it. If it fails, admit it frankly and try another. But above all, try something.

RAIS JOHN POMBE MAGUFULI.

View attachment 441063

Utawala wa rais John Pombe Magufuli una zaidi ya mwaka moja na miezi kadhaa madarakani. Kama taifa, hatuwezi kuendelea na fungate (honeymoon) ya utawala wake wakati ni wazi mambo yanaonekana kuwa mabaya katika maeneo mengi muhimu kwa uchumi wa Tanzania.

Ufike wakati sasa tuanze kizungumzia mambo mazito yanayotukabili kama taifa.

Magufuli atambue kuwa hata Mungu mwenyewe alianza na mwanga

"Mungu akasema, iwe nuru, ikawa nuru. Mungu akaiona nuru na giza. Mungu akaiita nuru mchana, na giza akaiita usiku. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya kwanza"

Ni maneno kutoka katika kitabu cha mwanzo(1: 3~5)

Tunatakiwa kufikiria kwamba tunaweza kuumizwa na tunaweza kujiumiza wenyewe, Magufuli anatakiwa kuambiwa kuwa safari yake ni ngumu katika uchumi.

Note: Magufuli utashi wa kisiasa ni muhimu katika kuendesha taifa.

Mipango ya rais Herbert ni sawa na mipango ya Magufuli.

Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu.

By mr mkiki

Unamuombea mabaya Magufuli hayato mpata

Ataendelea kunyoosha mpaka nchi itakapokaa sawa

Maana umeandika mambo meeeengi America kwa wakati huo ilikuwa ina wasomi zaidi ya asilimia 50

Mwaka huu 2016 Tanzania ina wasomi wasiozidi asilimia 12 wapi na wapi

Acha Raisi ajenge nchi
 
Duh!!! Kuna watu kwa kweli hawajielewi wanasimamia wapi hasa katika suala zima la matumizi ya ubongo wao na mmoja wapo ni huyu aliye andika huu upuuzi.
Acha uccm kubali kukoselewa na kubali ushauri kama unafaa tatizo lenu mnajifanya mnajua kila kitu gavana wa bank kuu anasema hamna tatizo yeye anasema kunatatizo ivi mananiya gani na hili taifa
 
Umetumia muda mwingi kuandika mambo mengi ambayo hayana uhusiano kabisa, sasa Tanzania itakuwaje na anguko la Uchumi? Uchumi upi huo uliokuwa nao TZ mpaka ipate anguko la uchumi?

Nchi ya GDP ya chini 45 Billion (US) tu na watu zaidi ya milioni 40, halafu unaongelea anguko la uchumi kana kwamba sasa hivi kuna kupanda kwa uchumi au kumeshawahi kuwepo na Uchumi mkubwa hadi uongelee anguko la Uchumi?

Sasa kama una akili zinazotosha kuvukia barabara tu utaelewaje mambo yaliyo juu ya uwezo wako wa kuelewa?
 
Umetumia muda mwingi kuandika mambo mengi ambayo hayana uhusiano kabisa, sasa Tanzania itakuwaje na anguko la Uchumi? Uchumi upi huo uliokuwa nao TZ mpaka ipate anguko la uchumi?

Nchi ya GDP ya chini 45 Billion (US) tu na watu zaidi ya milioni 40, halafu unaongelea anguko la uchumi kana kwamba sasa hivi kuna kupanda kwa uchumi au kumeshawahi kuwepo na Uchumi mkubwa hadi uongelee anguko la Uchumi?
Mtu anakua kama dodoki kulinganisha vitu hata havifai kulinganishwa utafikiri ametumwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom