Jumanne Kishimba alishapatikana?

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
7,002
9,987
Ndugu wana jamvi naomba kupata ufafanuzi,kwa mtu yeyote anayeelewa kuhusu mtu anayeitwa Jumanne Kishimba.

Mwaka 2006 serikali kupitia Jeshi la Polisi,walitangaza kumtafuta kwa udi na uvumba na zawadi nono kwa mtu au kikundi cha mtu atakayefanikisha kupatikakana kwa mmiliki wa kampuni iitwayo IMALASEKO,Kufuatia meli yake iitwayo MV. NYAMAGENI,kuzama na kuua mamia ya abiria wakati meli yake haikuwa na kibali cha kusafilisha abiria kutoka kwa mamlaka husika.

Sasa napenda kujua,huyu Kishimba ndio huyu Mbunge wa KAHAMA au majina yanafanana?

Je, kama ndiye kesi yake iliishia wapi?
Kama siye Kishimba wa ukweli alishapatikana?
Kama hajapatikana Jeshi la polisi limefikia wapi katika jitiahada zake za kumtafuta ?
 
Kaua yeye au meli?Kuna nahodha na watu wa usalama,hao ndio wa kubanwa ndio mana yupo huru na ni mbunge
 
Wakati wanatangaza kumtafuta hawakujua kuwa yeye ndo kauwa?
 
Katika siasa siku zote ukitaka kuishi salama kuwa upande wa alie madarakani. Upande huo hata sumu yaweza badilishwa kuwa sukari. Na hakikisha siku zote unapiga wimbo aupendao aliekukodi kuimba.
 
Baada ya kuupata Ubunge kupitia CCM polisi wamenywea. Ndio maana wanabandikwa majina ya utani kama PoliCCM.

Vv
 
Kaua yeye au meli?Kuna nahodha na watu wa usalama,hao ndio wa kubanwa ndio mana yupo huru na ni mbunge

Upo sahihi kiongozi!Hata meli zinazomilikiwa na katibu mkuu wetu ziliwahi kukamatwa zikisafirisha meno ya tembo na mheshimiwa hakufanywa lolote hadi leo,ccm hoyeeee!
 
Katika siasa siku zote ukitaka kuishi salama kuwa upande wa alie madarakani. Upande huo hata sumu yaweza badilishwa kuwa sukari. Na hakikisha siku zote unapiga wimbo aupendao aliekukodi kuimba.
Nimeupenda sana ujumbe wako!
 
Ndugu wana jamvi naomba kupata ufafanuzi,kwa mtu yeyote anayeelewa kuhusu mtu anayeitwa Jumanne Kishimba.

Mwaka 2006 serikali kupitia Jeshi la Polisi,walitangaza kumtafuta kwa udi na uvumba na zawadi nono kwa mtu au kikundi cha mtu atakayefanikisha kupatikakana kwa mmiliki wa kampuni iitwayo IMALASEKO,Kufuatia meli yake iitwayo MV. NYAMAGENI,kuzama na kuua mamia ya abiria wakati meli yake haikuwa na kibali cha kusafilisha abiria kutoka kwa mamlaka husika.

Sasa napenda kujua,huyu Kishimba ndio huyu Mbunge wa KAHAMA au majina yanafanana?

Je, kama ndiye kesi yake iliishia wapi?
Kama siye Kishimba wa ukweli alishapatikana?
Kama hajapatikana Jeshi la polisi limefikia wapi katika jitiahada zake za kumtafuta ?
Unamkumbuka yule aliyekamatwa kwa kishindo Masaki yeye na dereva wake wakidaiwa kumpiga askari , leo in mkuu wa mkoa, alikubali kurudi kundini wakayamaliza kimyakimya, bado Sugu na Lema, wakikubali haya, kwishneiii.
 
Back
Top Bottom